Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.
Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?
Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?
Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.
Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?
Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.
Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.
Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.
Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?
Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.
Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?
Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?
Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?
Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?
Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?
====
Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya
Kwani kwa maoni yako wewe korona imeletwa na nani?
Virus asiyeonekana ila kwa darubini,amesababisha ulimwengu kusimama,na wajuzi wote na wenye nguvu wameweka silaha chini na kutii amri kwa kiumbe huyu.,
Hivi hapa hatupati swali la kujiuliza ,Uhodari wetu,akili na maarifa vimekwamia wapi?
Je Iko nguvu ya kuitegemea ya kutuokowa na Janga hili endapo juhudi zetu zote zitashindikana?
Mashirika ya ndege yamesimamisha safari
Usafiri wa umma umesimama,
Biashara zimeanza kufungwa.
Mashule na Vyuo vimefungwa.
Magereza nayo yanafungwa kwa baadhi ya nchi.
Hatimae kambi za jeshi zitafungwa na wanjeshi kurudi majumbani kwao.
Mikutano ya Bunge,Mahakama, na Mwaziri wa serikali mbali mbali watabaki majumbani.
Uchumi utakufa na kuleta shida ya chakula na mahitaji.
ikiwa hali itazidi kuwa tete,kila binadamu atabaki kwake ,na mahospitalinayo yanaweza kufungwa.
Tukibakia wote tukiukubali ubinadamu wetu kuwa sote tuko sawa mbele ya shida na Maradhi,na kila mmoja wetu hataki afe.
Hapo ndipo tutakuwa tumejifunza jambo .
KUWA HUU ULIMWENGU YUKO ANAYEUDHIBITI NAKUUENDESHA
TUKIMJUWA HUYO!
HAPO TUTAKUWA SALAMA
NA WOTE TUTAPOROMOKA NA KUTII NA KUSUJUDU.
Huyo ndie mwenye dunia yake, na kila kitu ni chake.
Mungu Mkuu Muumba,asiye hitaji lolote kwa viumbe,na hakerwi na vilio vyenu anapo waadhibu kwa utovu wa nidhamu.