Unaruka sana.
Nakuambia unipe maana ya ubaya kwa mujibu wa maelezo ya Mungu,wewe unadai hatujathibitisha kama yupo.
Ulisema kwa mujibu wa mungu hukusema kwa munibu wa maelezo ya kuhusu mungu, see the differ
Sasa wewe unathibitisha vipi kama hayupo kama sio kupitia maandiko yake ambayo unayatia yaonekane kama yana contradictions kutimiza matakwa yako ya kumkana ?
Kwani spiderman utamthibitishaje kua hayupo nje ya masimulizi yake?
Namna ambayo unaweza kupinga kua spiderman hayupo ndio hiyo hiyo ambayo unaweza kuitumka kupinga kua mungu hayupo
Ni kama nikuambie kua kuna post ya 5000 kwenye huu uzi, vigezo utavyotumia kupinga kua post hiyo kwenye hu haupo unaweza kuzitumia kuonesha mungu na spiderman hawapo
Bas na sisi hapa tunataka kuthibitisha yupo kupitia maandiko kama ambayo wewe unampinga kupitia maandiko.
Utakubali kua apiderman yupo kupitia maandiko ambayo wewe na mwenzako mmepinga kua hawezekani kuwepo?
Kwa hivyo unapodai tuthibitishe kuwa yupo huko tunakoenda na ulichoulizwa ndo kinatupeleka kwenye kuthibitisha kama unavyotaka.
Mnakoenda wapi?
Alafu unaposema hata yako yanaweza kuwa mabaya hiyo bado haijawa kwa mujibu wa Mungu.
Hapa umerudia kosa tena lile lile ambalo umekua ukikosea
Ulitakiwa useme kwa mujibu wa habari zilizoandika kuhusu mungu, na sio kwamba kwa mujibu wa mungu.
Nimekujibu kwa mujibu wa ulimwengu ambao umeelezwa na vitabu kua umeumbwa na mungu ambao na mimi niko ndani yake, sasa ukisema hayo mabaya ni kwa mujibu wako inatakiwa ujue kua niko ndani ya ulimwengu ambao haukutakiwa kua na mabaya.
Kwa sababu wewe unaweza kuona jambo fulani baya na mwingine akaona zuri na yule akaona zuri pia.kwa hiyo jambo moja linaweza likawa na mitazamo mbali mbali.
Sawasawa cha msingi pointi ya ubaya bado ipo, mtu akiona jambo fulani baya halafu mwingine akiona jambo fulani ni zuri huwezi kusema ulimwengu hauna mabaya.
Lakini hapa tunamzungumzia huyu Mungu unaesema ana sifa ya ubaya.
Huu ubaya tukisema tuufasiri kwa kila mmoja anaivyoona bado haitakuwa sawa kwa sababu wapo watakaoona kuwa huu ubaya na wapo watakaoona kuwa huu ni uzuri,kwa hiyo haiwezekani mtazamo wako binafsi ukaunasibosha na makusudio ya Mungu.
Katika ulimwengu ambao ungeumbwa na mungu ambaye hana sifa ya ubaya ambaye hawezi kuumba ulimwengu wenye mabaya, kusingekua na jambo lolote ambalo lingeonekana ni baya hata kama maelfu ya watu wataliona zuri ila endapo kuna mmoja kati yao akaliona jambo hilo ni baya tu kunafanya ulimwengu huo uwe na ubaya
Watu fulani fulani kutofautina kimtazamo kati ya ubaya na uzuri hata kwa uchache huo huo tu kunatosha kuthibitisha kua mabaya yapo
Nataka uniambie kwanza kwa mujibu wa huyo Mungu ameeleza vipi juu ya makusudio ya ubaya yeye mwenyewe ?
Kwanza usirudie tena kusema kwa mujibu wa mungu, ulitakiwa kusema kwa.mujibu wa vitabu vya mungu vimeelezea vipi
Vitabu vilivyoandika habari za mungu hazijaeleza kimantiki kwanini mungu mjuzi wa yote, mwenye uoendo wote na uwezo wote asiye na sifa ya ubaya kaumba ulimwengu wenye kuruhusu mabaya
Unaweza kujibu hilo swali hapo juu?
Nataka Mungu huyo unayempinga kasemaje kwanza,maelezo yako yatakuja baadae.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Hakuna mahali mungu huyo kasema chochote, bali vitabu ndio vimeandika habari kwa ku-refer mungu kama ilivyo spiderman book na finctional characters wengine ambao hawathibitishiki kihalisia