#COVID19 Corona: India kinaponuka sisi tuna cha kujifunza?

Mabibi na mabwana corona imepiga katika mataifa yote, lakini hili la India ni hatari tupu:

View attachment 1766866

Wenzetu India wananyolewa vilivyo hivi sasa. Je sisi tunatahadhari au mikakati ipi kutoangukia kwenye zahama kama hili?

Tume ya Corona ya mama iko wapi? Ina mapya yapi?

India wanakokimbilia vigogo wetu kwa matibabu, ndiyo hawa wanaochoma miili ya wafu wao leo hadi barabarani.

Tusichukulie poa wajameni. Maisha ya mtu hayawezi kulinganishwa na vitu.

Kenya wamepiga marufuku safari za ndege kati yao na India.

Vivyo hivyo kwa Malawi na hata mataifa mengine.

Sisi je?
Tusiogope, hofu ni mbaya kuliko Covid yenyewe. Mungu aliyetuokoa na wimbi la kwanza mwaka jana atatuokoa na wimbi la pili na la tatu. Tuendelee kumtumaini na kuchukua tahadhari
 
Mwalimu wa hizi propaganda zenu alishatokomea, jidanganyeni tu badala ya kuchukua tahadhari, watu laki mbili sio jambo la kufanyia mzaha hata kidogo, watu wanakosa hadi pakuwazika wapendwa wao.
Tahadhari tulishachukua na tunaendelea kuchukua kila siku yaani kumtanguliza na kumwomba Mungu. Hiyo ni silshs kubwa sana kuliko zone, na matokeo yake yameonekana, yaani Tanzania tuko salama sana mara elfu nyingi kuliko nchi nyingi zinazojidai kutumia sayansi lakini zimezika kwa malaki .
 
Watu wankufa kila siku mamilioni kwa mamilioni kutokana na sababu mbali mbali. Hili halishangazi. Kinachoshangaza ni ile speed ya vifo ndani muda mfupi kutokana na sababu moja tu.
 
Nchi kutangaza kuhusu corona sio suruhisho kabsa? Kama ingekuwa ni suruhisho basi marekani wasingekufa vile
 
Mabibi na mabwana corona imepiga katika mataifa yote, lakini hili la India ni hatari tupu:

View attachment 1766866

Wenzetu India wananyolewa vilivyo hivi sasa. Je sisi tunatahadhari au mikakati ipi kutoangukia kwenye zahama kama hili?

Tume ya Corona ya mama iko wapi? Ina mapya yapi?

India wanakokimbilia vigogo wetu kwa matibabu, ndiyo hawa wanaochoma miili ya wafu wao leo hadi barabarani.

Tusichukulie poa wajameni. Maisha ya mtu hayawezi kulinganishwa na vitu.

Kenya wamepiga marufuku safari za ndege kati yao na India.

Vivyo hivyo kwa Malawi na hata mataifa mengine.

Sisi je?
Yaani kila taarifa ya habari Aljazeera hili la covid-19 India ni habari ya kwanza au pili .Mungu awasaidie
 
Wenzetu India wananyolewa vilivyo hivi sasa. Je sisi tunatahadhari au mikakati ipi kutoangukia kwenye zahama kama hili?
Tushasahau hayo Mambo fanya kazi chukua tahadhari,dunia nzima Ina corona
 
Kwa hii rate ya maambukizi ya Watu 360000 ndani ya masaa 24 India iko kwenye hali ngumu
 
Hatukuanza Leo kuambiwa tutakufa kama KUKU.
mbinu ya kumtegemea MUNGU NI SAHIHI NA INAFANYA KAZI.
Mwalimu wa hizi propaganda zenu alishatokomea, jidanganyeni tu badala ya kuchukua tahadhari, watu laki mbili sio jambo la kufanyia mzaha hata kidogo, watu wanakosa hadi pakuwazika wapendwa wao.
 
Mabibi na mabwana corona imepiga katika mataifa yote, lakini hili la India ni hatari tupu:

View attachment 1766866

Wenzetu India wananyolewa vilivyo hivi sasa. Je sisi tunatahadhari au mikakati ipi kutoangukia kwenye zahama kama hili?

Tume ya Corona ya mama iko wapi? Ina mapya yapi?

India wanakokimbilia vigogo wetu kwa matibabu, ndiyo hawa wanaochoma miili ya wafu wao leo hadi barabarani.

Tusichukulie poa wajameni. Maisha ya mtu hayawezi kulinganishwa na vitu.

Kenya wamepiga marufuku safari za ndege kati yao na India.

Vivyo hivyo kwa Malawi na hata mataifa mengine.

Sisi je?
Mkuu 'brazaj'

Kusema kweli, hii Corona inachanganya sana, kiasi kwamba hata ni vigumu kuelewa na kukieleza kinachotokea duniani kote juu ya ugonjwa huu.
Tunajua 'strains' hizi mpya zinazoibuka, n.k., na kuchochea milipuko sehemu mbalimbali, lakini kwingine unakuta bado kumepoa kiasi, hata kama imekwishajulikana hakuna nchi ambayo haina corona.

Afrika, kwa ujumla wake, hali haijawa ya kutisha sana, pamoja na kwamba, kuna nchi zinazofanya jitihada mbalimbali kuudhibiti, lakini bado hali zao ukilinganisha na wasiofanya kitu, tena nchi hizo zikiwa majirani; hapo inakuwa mchanganyiko usioelezeka.

Kwa mfano: Kenya wamehangaika mno na huu ugonjwa toka mwanzo, lakini ni kama juhudi zao hazizai matunda kama inavyotegemewa. Lakini kwa upande wa pili, hapo mpakani mwao tu, kusini, Tanzania wao ni kama hawatambui kabisa kwamba kuna ugonjwa wa hatari.

Hata kama Tanzania wameacha kupima na kutangaza maambukizi, hali iliyoko Kenya ingekuwa ipo hapa, sidhani kuwa hawa viongozi wetu wangepuuza kama wanavyopuuza sasa hivi!
Hivi umewaona leo kwenye picha ndani ya mkutano wao wa CCM?
Ni kama hawa watu hawajawahi kabisa kusikia kwamba upo ugonjwa unbaoitwa COVID-19, unaoua watu.
Jamaa zetu hawana habari kabisa

Kwa hiyo, sisi sasa tusemeje, tuendelee kuamini kwamba Magufuli na maaskofu na mashehe wake waliomba sana?

Kwa nini India kumelipuka sana sasa hivi, na sisi tungoje zamu yetu?

Viongozi wetu hawasomi wala kusikia yanayotokea huko kwingine, na wakajiachia bila hata kufanya juhudi kidogo za kujikinga wasiambukizane?
Hata akina Philip Mpango waliokwishaonja joto ya jiwe, hawawezi kutoa ushuhuda kwa wenzao?

Bado wanaogopa Magufuli asiwakaripie wakifanya juhudi za kujikinga?

Bado kuna mambo mengi yasiyofahamika kuhusu ugonjwa huu...tuombe tu usije ukalipukia hapa hata kabla ya hiyo timu iliyoundwa haijatoa mapendekezo yake.
 
Mabibi na mabwana corona imepiga katika mataifa yote, lakini hili la India ni hatari tupu:

View attachment 1766866

Wenzetu India wananyolewa vilivyo hivi sasa. Je sisi tunatahadhari au mikakati ipi kutoangukia kwenye zahama kama hili?

Tume ya Corona ya mama iko wapi? Ina mapya yapi?

India wanakokimbilia vigogo wetu kwa matibabu, ndiyo hawa wanaochoma miili ya wafu wao leo hadi barabarani.

Tusichukulie poa wajameni. Maisha ya mtu hayawezi kulinganishwa na vitu.

Kenya wamepiga marufuku safari za ndege kati yao na India.

Vivyo hivyo kwa Malawi na hata mataifa mengine.

Sisi je?
Cha kujifunza ni kwamba zamu yetu yaja kama tutaendelea na ujinga wa kutegemea sala na uongo mwingine bila kuchukua hatua.
 
Kwanini watu wanalazimisha Serikali itangaze kuhusu corona badala ya kuchukua hatua wewe mwenyewe za kujikinga na familia yako?

Unadhani wahindi wanaopukutika hivi sasa hadi mataifa mbali mbali wakiwamo mahasimu wao wakubwa Pakistan na China, wamekuwa wakipeleka mitungi ya oxygen yamekuwa ni makosa yao ya kutokuchua tahadhari, ila sisi?
 
Cha kujifunza ni kwamba zamu yetu yaja kama tutaendelea na ujinga wa kutegemea sala na uongo mwingine bila kuchukua hatua.

Hii tume ya mama na mama kutochukua hatua hata za kuzuia madege baina yetu na India mama asipoangalia hatakuja kwepa lawama.

Ni mawazo finyu sana kudhani hili ni la wahindi peke yao.
 
Corona ya India ni level ya juu Sana tusubiri ya kwetu naona zinatofautiana kwa rangi na lugha
 
Back
Top Bottom