#COVID19 Corona: India kinaponuka sisi tuna cha kujifunza?

#COVID19 Corona: India kinaponuka sisi tuna cha kujifunza?

Tufanyeje sasa? Kwani unazani india wamejitakia? Muhimu tuendelee kumuomba Mungu atuepushie mbali, kwani hali ya maisha yetu ni ngumu na hatuwezi kufuata masharti ya Covid-19 kwa [emoji817]%.

Mkuu cha kufanya kipo kwenye mada:

1. Tume ya mama inabeba mustakabala wa maisha yetu.
2. Kuzuia safari za anga baina yetu na India ni hatua za mwanzo serikali inapaswa kufanya.

Huo ndiyo msingi.
 
Kwanini watu wanalazimisha Serikali itangaze kuhusu corona badala ya kuchukua hatua wewe mwenyewe za kujikinga na familia yako?
Kwasababu wengine hata hawajui korona ni kitu gani,sehemu Fulani huko Kijiji sitapataja ndugu ukiona hali ilivyo utachoka, mtu hata hafamu chochote kuhusu korona yan anachojua yy ni kuwa kuna jina tu liitwalo "korona". Sasa watu Kama Hawa serikali ndo ilibidi ifanye juhudi kuwafikia huko huko kwao ndanindani ili kuwafahamisha nini cha kufanya ...
 
Hata huko India, siyo kwamba hawakuwa wanachukua tahadhari, la hasha. Wamechukua tahadhari zote dhidi ya Corona lakini bado vifo vikaendelea
Ni upotoshaji, acha kupotosha watu!
 
Mwalimu wa hizi propaganda zenu alishatokomea, jidanganyeni tu badala ya kuchukua tahadhari, watu laki mbili sio jambo la kufanyia mzaha hata kidogo, watu wanakosa hadi pakuwazika wapendwa wao.
Mbona hujiulizi kwanini kama wamechanja watu wengi na vifo ni vingi?
 
Acha nibaki kwenye kivuli cha magufuli
kinga ya mwili ya mtu hutofautiana yako haiwezi kufanana na ya mtu wa miaka 50
wapo wanaoonyesha dalili za haraka na wapo wanaochelewa
wanasayansi wanasema wapo wanaoipata corona na ikaondoka kutokana na kinga za miili yao kupambana vizri
wanasema umri ulio katika high risk 45-50 hapo
Screenshot_20210429-111122.jpg
 
Mabibi na mabwana corona imepiga katika mataifa yote, lakini hili la India ni hatari tupu:

View attachment 1766866


Wenzetu India wananyolewa vilivyo hivi sasa. Je sisi tunatahadhari au mikakati ipi kutoangukia kwenye zahama kama hili?

Tume ya Corona ya mama iko wapi? Ina mapya yapi?

India wanakokimbilia vigogo wetu kwa matibabu, ndiyo hawa wanaochoma miili ya wafu wao leo hadi barabarani.

Tusichukulie poa wajameni. Maisha ya mtu hayawezi kulinganishwa na vitu.

Kenya wamepiga marufuku safari za ndege kati yao na India.

Vivyo hivyo kwa Malawi na hata mataifa mengine.

Sisi je?
Ukimwi uligundulika mwaka 1983 lakini mpaka sasa watu wanaugua ukimwi na wanaendelea kunyanduana. Acha uoga falangundi wewe
 
Wanakera sn hawa mbwa.... Yaani wanacheka wanaoumwa eti ni wazembe hawana Mungu huku wao maccm mungu wao kafa kwa korona hiyohiyo
Kwani kucheka watu waliyokufa ni tatizo? basi kuna watu wasingefurahia alipokufa Magufuli.
 
na ma superstar wa India wamenza kusepa na private jet zao kukimbia janga!

ki ukweli, ninaona kama corona ni survival of the fittest ama chosen! tutahaingaika kushoto na kulia the best ni kuchukua tahadhari na likikukuta, basi pambana na make peace na watu maana uhakika wa maisha nani anao?

nje ya mada kidogo:

kuna sehemu marekani ambapo kuna hizi Georgia Guidestones! ni kama vile lile wazo la population ya dunia linatekelezwa. sijui baada ya corona lipi lingine litaibuka! labda nipo deep sana katika kutafakari hili! ila mwanadamu hakosi mbinu...

tembelea hapa kujifunza zaidi!
 
Usisahau kuwa uliye mwabudu katangulizwa kuzimu na korona naye alikuwa kichwa ngumu kuliko wewe.
Wengine wanasema Jiwe alichanja chanjo ya corona kisirisiri na wengine mnasema kafa kwa corona, sasa lipi sahihi?
 
Watu wankufa kila siku mamilioni kwa mamilioni kutokana na sababu mbali mbali. Hili halishangazi. Kinachoshangaza ni ile speed ya vifo ndani muda mfupi kutokana na sababu moja tu.
Hayo unayoyaona wewe hayashangazi ni kwa sababu hayatangazwi kwa hali ya kushangaza kama inavyofanyika kwenye corona, kwenye corona vinavyotangazwa sana ni vifo tu na si waliumwa na kupona ambao ndio huwa wengi.
 
Kweli watu walikuwa na tatizo na Mako kuliko hata hiyo corona, yani huu uzi sijaona milawama kwa Mama Samia ndio kwanza naona anaelezwa kwa upole tofauti na kipindi cha Meko.
 
Mwalimu wa hizi propaganda zenu alishatokomea, jidanganyeni tu badala ya kuchukua tahadhari, watu laki mbili sio jambo la kufanyia mzaha hata kidogo, watu wanakosa hadi pakuwazika wapendwa wao.
Acha story. Chukua tahadhari kivyako vyako. Wabongo mmezidi kelele
 
Back
Top Bottom