Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa

Pascal Mayalla,
Pamoja na kuongea mambo ya fursa, umekosea sana kusema hakuna mtz aiyeambukizwa hapa nchini, maana inachukua angalau siku 11 mpaka mtu kugunduika kuwa ameambukizwa, hasa baada ya kuanza kuonyesha dalili! Sijui kwa nini umeamua kupotosha hivi!

Tuombe Mungu hao wate waliokutana na wagonjwa waCovid-19 wasiwe na maambukizi! Maana kama watakuwa na maambujizi mfumo wetu wa afya hautaweza kuhimili!

Badara ya kupaka matope wenye taaluma zao, we ungeendelea na brabra zako tu na siyo kukurupuka na kutoa hitimisho kwa mambo usiyoyajua! Kosa gani aliofanya daktari juu ya mask kwa mfano?
 
Kwa hili amebwabwaja tu!
 
Usimwite binadamu mwenzio nyani tafadhali! Hata mimi kwa kuna sehemu kanikwaza...ila bado ni binadamu!
 
Paskali ww ni motivation speaker, huna fursa yoyote uliyotumia kama ww zaidi ya kushauri wengine wafanye. Vinginevyo nitajie shughuli yoyote uliyofungua nije niione ni kesho.
Mkuu Tindo asante kuniita motivation speaker, kila Jumamosi asubuhi, Saa 1:30 hadi 3:00 asabuhi, nakuwa Star TV live, kuwapiga msasa madogo kwenye fani, kupitia kipindi cha Jicho Letu Ndani Habari, esho tunazungumzia Corona.
P
 
Siyo kwamba hakuna maambukizi bali vipimo hamna/havifanyiki!
Kwenye mipaka yetu yote tunapima joto kila anayeingia, ukikutwa tuu na homa, unachukuliwa vipimo vya ziada. Hao wagonjwa wote 6 wamewekwa karantini, na watu wote waliokutana nao wamechukuliwa vipimo, hakuna aliyeambukizwa.
P
 
Mkuu kama serikali imefilisika waseme tu wananchi waichangie, umesahau jinsi wana ccm waliweza kumchangia Mashinji milioni 30 ndani ya siku mpaka akashangaa, wakiamua kuendeleza harambee kwa siku 40 mfululizo ni billioni 1.2, nchi ina hela bwana !
 
No we are very serious, tumeweka madaktari official borders zote, kila anayeingia tunampima, wageni wote kutoka nchi zenye Corona, wanaingia kwenye 14 days mandatory self quarantine.
Sasa serikali imetoa list ya official spokespersons wa kuzungumzia Corona na sio kila mtu.
P
 

Kaka Mayala, naomba niongelee kitu kimoja tu kwenye ujumbe wao: hivi vifaa/vyombo vya kunawia mikono. Pamoja na ubora wake na ukweli kwamba vinaweza kuwa msaada mkubwa kufanya usafi wa mikoni, vina kasoro kubwa kutumika kwenye muktadha wa mapambano ya Covid19. Nifafanue.
  1. Ushahidi wa kisayansi unaonesha kwamba kunawa mikono kwa maji na sabuni kwa wastani wa sekunde 20, kunaondoa virusi vya Covid19 ambayo mtu anaweza akawa amevipata kwa kushika kitu au mahali palipoangukiwa na aerosols au droplets za mtu mwenye maambikzi au kwa kushikana mkono na mwenye maambukizi.
  2. Kwenye unawaji huu, kuna maneno kama manne ambayo ni kewords za kuzingatiwa kwenye mchakato (1) MAJI, (2)YANAYOTIRIRIKA, (3)SABUNI, na (4) MUDA (sekunde 20 au ziada).
  3. Kwa nini maji yanatakiwa kutiririka na sio kunawa kwenye besini? Ni kwa sababu kunawa kwenye beseni kuna uwezekano mkubwa wa virusi kubaki kwenye chombo au maji ambayo umenawia na hivyo ukawa hujafanya lolote la kusaidia.
  4. Hivi vyombo ulivyoviweka hapa maji machafu baada ya kunawa yana virusi (tuchukulie aliyenawa kakamata virusi wa Covid19). Katika harakati za kuyamwaga hayo maji na namna ya ku-handle chombo kilichotumika kukinga (besini) kuna kila dalili vikahatarisha mtu kushika virus walewale waliootolewa kwenye mikono.
  5. Hivyo basi, iwapo vyombo hivi vinatumika kunawia mikono (kutokana na uhaba wa maji ya bomba) ni vema haya mebeseni yakatoholewa yawe kama sink ili mtu anaponawa maji yasisimame bali yakamwagike chini. Au hiyo ndoo iwekwe mahili ambapo mtu akinawa maji yanamwagika chini na sio kwenye beseni.
  6. Kinyume na hapo, hizo beseni za kukinga maji machafu zinaweza kusaidia kumbembeleza na kumsambaza Corona

    Ni muhim pia kukumbuka kunawa na kujifuta na tissue na kuzitupa. Kwa kuwa sio kila mtu anaweza kupata tissue maalumu za kufutia mikono, taulo inaweza kutimika ila mhusika awe na uhakika anaitumia yeye mwenyewe kwa kazi hiyo tu na hakuna mtu ataigusa. Hayo yakishindikana, basi ni vema kunawa, kung'uta mikono hewani na uache ikauke yenyewe.

    MM togolani
 
Mkuu Tindo asante kuniita motivation speaker, kila Jumamosi asubuhi, Saa 1:30 hadi 3:00 asabuhi, nakuwa Star TV live, kuwapiga msasa madogo kwenye fani, kupitia kipindi cha Jicho Letu Ndani Habari, esho tunazungumzia Corona.
P

Hamna shida kaka, nitakua mbele ya TV nipate hayo madini. Uzungumzie pia na tume shirikishi ya uchaguzi, huenda huku jukwaani unashindwa kuielezea.
 
Tangu mwezi wa 11 mkuu, na waliokufa ni wengi sana, unasikia mtu wako wa karibu kafa ghafla ukiuliza unaambiwa pneumonia
Ila kiukweli watu wame-panic tu.

Huku mtaani kwetu watu wanavaa gloves na masks bila hata kuzingatia utaratibu.

Huu ugonjwa tunao tangu December na hakuna aliyekufa, labda awe immunocompromised.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanufaika wa hizo pesa za WB, watakuwa wanachama dola, muuza ndoo na maji ya chumvi kamwe huo msaada hautomfikia...

Everyday is Saturday.................... 😎
Kwa vyovyote vile, sio kila mmoja mmoja atafaidika;
Kama ambavyo ikitokea leo Wizara ya Fedha akifanikisha zoezi la kuipata hiyo grant na ikawa kwenye account za BoT, si kila mmoja anauwezo wa ku-develop business plan ya kuomba mkopo wa machinery, purchase of raw materials ambavyo in turn tutapunguza imports ili kusambaza kwa soko la ndani na hizo fedha zikabakia ndani na baadhi ya Watanzania wakapata ajira na TRA ikaongeza tax base kutokana na uwekezaji huu.

Ngoma ipo kwenye how quick as a nation we'll be proactive to seize such an opportunity kwa faida ya mama Tanzania.

Bahati mbaya, baadhi ya walio kwenye authority ambao ni jukumu lao kuomba, jambo kama hili they feel ni kama haliwahusu maana pay-check yake ipo tu mwisho wa mwezi. Aki-facilitate mtonyo uje, au asipofanya hivyo, haoni kama ina athari kwenye nini atavuta mwisho wa mwezi.

To be honesty, we have very few people who thinks in big picture.

Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote
 
Siyo kweli! Kama ni kweli mbona mwanaFA hakuwekwa karentini siku 14 alipotoka south Afrika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…