joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
- Thread starter
- #221
Kitendo cha mkulima wa Tanzania kuuza Kenya haimaanishi kwamba Tanzania hakuna soko, je China, USA, Japan wanapoleta Mali zao kuuza Africa inamaana kwamba Afrika ni soko kubwa kuliko kwao?.Mambo yangu na swaumu niachie mwenyewe, hapa tujadili mada.
Elewa Concept yangu katika kilimo na biashara. Wakulima wa Tz wako kufanya biashara na wakenya, sio kutoa msaada. Kama mkulima wa Tanzania anaweza kuuza mazao yake mpaka Kenya, maana yake Kenya kuna soko lenye faida kubwa kwake otherwise mkulima wa Tanzania asingepoteza muda wake kumuuzia Mkenya.
Fahamu hili, Mkulima huwa hakuangalii wewe ni nani, uraia wako hauna maana yoyote mbele ya mkulima, yeye anaangalia mfukoni una nini, ukiwa na pesa za kumpa faida mkulima yuko tayari kukuuzia hata mazao yakiwa shambani hayajakomaa.
Tunapowauzia wakenya, maana yake ni kwamba tinazalisha zaidi na tunachokihitaji, kwahiyo hapa nyumbani "Supply is more than demand" kwahiyo bei hapa lazima iwe chini. Qatar wanazalisha mafuta mengi kuliko wanayohitaji, ndio sababu bei ya Petrol na Diesel kwao ipo chini kuliko huku kwetu.
Jambo muhimu lazima ujue ni kwamba, Chakula kinahitajika sana, WFP wapo tayari kununua chakula chetu chote cha ziada, nchi za DRC, Rwanda, Zambia, Zimbabwe, Malawi na Msumbiji, zote wanahitaji chakula chetu, Kenya sio soko muhimu sana, Kenya inahitaji Chakula chetu zaidi kuliko sisi tunavyohitaji soko lao.
Sent using Jamii Forums mobile app