Ndugu yangu, mi nikiwasikiliza hawa viumbe napata hasira. Yani Mh. Na praise team hawaambiliki. Kama waziri anatamka asilimia 9% (aprox 4,500,000) ya watanzania wana kisukari na Corona imeonekana kuua zaidi ya robo ya hili kundi je tupo tayari kuzika zaidi ya watu milioni moja?!
Wanachofanya nikutuchezea physiological game, wamekazana "kila mmoja achukue tahadhari" ili mambo yakiharibika watu wajilaumu wenyewe wasilaumu serekali. Wakati huko kuchukua tahadhari ni impossible bila serekali kuingilia kati. Mfano nimeenda hotelini kula, naletewa msosi naanza kula, anakuja mteja mwingine anakaa upande wa pili tunatizimana, chances za kuambukizana zipo juu sana. Ni jukumu la serekali kuhakikisha biashara zote zinafata muongozo wa social distancing, huwezi ukamuachia mfanyi biashara ajisimamie. Hali hii ipo kwenye baa, usafiri wa umma n.k
Nasikitika sana!!