Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Mkuu MArekani mwenyewe hajiwezi kwa janga hili.Huyu Mzee ni masikini jeuri !! Msimamo wake unatesa raia wake, hizo propaganda za kirusi kutengenezwa Marekani angezipumzisha wakati huu wa dharura.
Anakataa msaada wakati raia wake wanataabika kwa ugonjwa na madaktari wameishiwa mpaka vifaa tiba huku wengi wakiambukizwa wakati wakitoa huduma.
Kama anataka kuwasaidia Irani yeye apunguze vikwazo walivyo iwekea Iran kiasi wanashindwa kuagiza baadhi ya madwa na vifaa au malighafi za kutengeneza madawa na vifaa tiba.
Msaada wa kinafiki sana huu, siku tatu au tano zilizopita kawaongezea vikwazo Iran mbele ya ombi la Iran kuondolewa baadhi ya vikwazo vinavyo husu huduma muhimu za kibinadamu waweze kupambana na COVID-19.