Jana Rais Magufuli alihutubia Taifa kuhusu hali halisi ya ugonjwa wa corona hapa Tanzania.
Katika mambo aliyosisitiza ni kutoa elimu kwa umma badala ya hofu na vitisho.
Lakini hali halisi Ikoje?
Jana ilikuwa jumapili ya kwanza baada ya mgonjwa wa kwanza kugundulika Tanzania.
Watu tulikusanyika kwenye makanisa yetu.
Mambo niliyogundua ambayo ni hatari kwa Taifa.
Wakristo wengi wanapuuza na hawajui madhara ya ugonjwa huu.
Pili, Hawajui kama ugonjwa ila wanajua ni mapepo au nguv za giza au kitu flani kimetoka kwa shetani.
Tatu, 90% Wanatumia sanitizer kwa wingi " japo wataalamu wengi wanasema Sanitizer inaua bacteria na sio virusi" Dawa ni kunawa maji kwa sek.40 kwa kutumia sabuni au kutumia detro ya maji ni nzuri zaidi.
Nnne. Amini Usiamini bado Wakristo wengi wanaamini Watu weusi hawapati virus hivi na wanafananisha na mafua makali.
Ushauri Kwa wenye mamlaka , Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Afya.
Fungeni mikusanyiko ya ibada makanisani na misikitini.
Nchi ya Marekani imenyoosha mikono dhidi ya ugonjwa huu kwa kuufunga kabisa jimbo la Calfonia, sio jambo dogo na ni jambo kubwa.
Napenda muwakumbushe watanzania Virusi hivi ni kama vile vya dengue, Sars, Homa ya riftvalley ambavyo vilisumbua sana Watanzania na hata tuka ogopa kula nyama, kwa hiyo virusi hivi ni hatari sana wawe na taadhali kubwa.
Pia Serikali isikae kimya. Kutoa up to date ya ugonjwa huu unawafanya wananchi kuwa na taadhari zaidi, hasa kujua sehemu gani kuna shida kubwa kama mtu amepanga kwenda asiendi na hii inasaidia sana kama serikali itakuwa imeweka ka a karantini ya mkoa gani na wilaya gani kuna shida kubwa. na watu wachukue taadhali zipi.
Msiwalaumu wananchi hata mara moja msipo wajulisha watajijulisha wenye.
CHUKUA TAADHALI CORONA NI UGONJWA HATARI SANA. NAWA MIKONO MARA KWA MARA, BAKI NYUMBANI KAMA HAKUNA ULAZIMA WA KWENDA POPOTE, TUWATUNZE WATOTO, NA WAZEE WETU WABAKI NYUMBANI WASIENDE KWENYE MIKUSANYIKO YA WATU WENGI.