Corona Virus: Rais Magufuli ahutubia Taifa - Machi 22, 2020 - Wagonjwa Tanzania wafikia 12

Sisi waislamu tuko makini sasa sijui kuhusu nyie kondoo wa Gwajima.
Kondoo wa Gwajima sio wote mkuu, ukiambiwa wewe ni kondoo wa Gwajima maana yake ; wewe ni fala, hujitambui, mjinga na limbukeni usiyejua maandiko wala dunia iendako.
 
Kaka Pascal Mayalla Najua you are being sarcastic, but it's not helping. Not this time Mkuu. Please
 
Zanzibar walichoamua ni mandatory/forced quarantine na sio self-isolation ambapo unabembelezwa kiuraini ukajiisolate mwenyewe popote upendapo. Go look for info.
Kijana usikurupuke,quarantine ni zuio la kutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine iwe kwa mnyama ambaye hana ugonjwa au anao. Ndicho kinachofanyika Italy na France. Tofauti na self isolation.
 
Ni swali fupi tu;

Je kamati ya kudhibiti virusi vya Corona iliyo chini ya Waziri Mkuu inahusisha pia wajumbe kutoka Zanzibar?

Maendeleo hayana vyama!
Huenda ikahusisha wanaccm tu ili kupambana na Chadema na mshirika wake Corona.
 
Tusitishane jamani.
P
Hatutishani mkuu, tunapeana tahadhari.

Hili la kushabikia kuwa ni ugonjwa wa kishetani na unaenezwa kishetani ni kughafiliana. Kwa nini tutumie sayansi kukabiliana na ushetani? Ukitapakaa Tanzania watakaoumia zaidi ni wazee wetu na wenye kinga hafifu, tusiwe wabinafsi.

Ni vyema kujifunza kwa wenzetu walipokosea tusijikwae. Huyu Mungu tunayemuomba alitupa akili na utashi, sasa leo tuviweke pembeni tutegemee atatufanyia miujiza tu. Leo tunazungumzia Italia, ila ukiangalia kuna nchi nyngine maambukizi yanaongezeka kwa kasi sana. Huku Afrika tuna advantage kuwa umechelewa kufika, tunamuda wakujikinga, ila huo muda unayoyoma kwa kasi sana.

Kama tunataka kuendelea na style ya mbuni kuchimbia kichwa kwenye mchanga, sawa tutavuna tunachopanda sasa.
 
Informer, Na wale wote walio kua na Maradhi haya wameonekana Negative" kwaio hatuna mgonjwa kabisa syo?
 
Tanzania tusizoee mambo ya kamati kila janga, wizara ya Afya na wizara nyingine zinaweza kutekeleza majukumu yote yenye kuhusu Corona.

Hizo kamati tutaunda ngapi jamani.
Wahuni TU hao,
Wanatafuta ulaji TU na kulipana posho.

Kuna mijitu kila janga inaliona Ni fursa za upigaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kamati zitakazo undwa ni za kisiasa zaidi, unategemea nini apo?
 
Hivi, mbona tunaambiwa mgonjwa wa kwanza kapona? Au JH wamekosea?
 
Wanasiasa wahuni sana washaigeuza Corona dili hapo mamilioni yatatumika kulipana posho wizara ya afya inatosha kabisa maana kamati yenyewe imejaa wanasiasa badala ya wataalam
 
Imeshaundwa kwani? Maana naona umeandika.wakati uliopo(inahusisha).Wewe si ndiyo ututajie na majina ya wajumbe na kule watokako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…