Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Naona baada ya mbowe kutangaza kufanya mikutano kibabe sasa mmekubali kutangaza uwepo wa korona ila wakati aghakan wanasema mlikuwa kimya😁😁😁😁
 
#UNAAMBIWA Waziri wa Afya Ummy Mwalimu @ummymwalimu amesema ameongea na mgonjwa aliebanika kuwa na corona Tanzania kwa njia ya simu na katika maelezo yake amesema alipokuwa Ubelgiji nyumba ambayo alifikia, Mume wa mwenye nyumba hiyo aliugua corona, itakumbukwa mgonjwa huyo alipofika Airport KIA hakubainika kuwa na homa ila alijishuku na akaenda kujifungia Hotelini asichanganyike na Watu, kisha baadae akaenda Mount Meru Hospt na sampuli ikachukuliwa hadi Maabara DSM na kuthibitika kuwa ana virusi vya corona.

Kwenda kujiweka self isolation hotelini pia amewatia watu hatarini. Kuanzia wahudumu wa vyumbani, wafua mashuka ya vitanda, wahudumu wa cafeteria, wageni wenzake etc. Kuna tv programe ikielimisha namna ya self isolation inavyotakiwa iwe na i am telling you sio tu kujifungia ndani ya chumba.

Mind you, alipojisikia kuwa anaumwa alikwendaje hospitali? kachukua taxi/uber, dala dala au katembea? hatua zote hizo atakuwa amewatia matatizoni watu wengine, ushauri wa WHO ni kutokutoka ulipo bali ni kuita ambulance/ watu wa afya ili wao ndio wakufate ulipo.
 
Mkuu bado husband and wives/boyfriend and girlfriend/ chldrens and parents wa hao waliyokutana na huyo mgonjwa

Chain ni ndefu sana na ndio maana ya Hatari yenyewe ktk hili Janga Mkuu.
 
Ivi unaamini mtu akiongea anayoongea au uharisia,
Kujifanyia isolation its impossible ata mwenyewe nikiwa nao lazima nitasema hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app

Yote yanawezekana
Malezi tunatofautiana sana
Umewaona wachina wanavyopaka kamasi kwenye mabomba ya mabasi na kwenye buttons za elevators?
Na sisi tutakuwa hivyo hivyo


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Waziri upo serous kwelii!!!!?
Kuwa mgonjwa anaendelea vizuri?
Anyway hapa kuna namna katika ugonjwa huu.

Tuambieni mgonjwa alikuwa hoteli gani na je mmechukua hatua zozote juu ya wahudum wa hoteli aliyokuwepo? maana hata kushika mlango tu ni njia ya kuambukiza je mlango alokuwa ameushika wahudum hawaushika?


Sent using Jamii Forums mobile app
Ilitakiwa Hotel yote iwe chini ya uangalizi maalumu.
 
Back
Top Bottom