Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

We aren't serious! Ukinawaga mikono kishaa ukashikiaga kikapu ile ile unakua umefanyanga Nini?
IMG-20200316-WA0029.jpeg
IMG-20200316-WA0024.jpeg
IMG-20200316-WA0025.jpeg


Don't make a promise you can't fulfill...
 
Taarifa ya Ummy ina kasoro na haijitoshelezi, au kuna upindishaji wa maksudi.

Mgonjwa aliingia nchini, akapimwa joto uwanja wa ndege KIA akaonekana yupo vizuri, akaruhusiwa kuondoka, tena bila ya maelekezo yoyote ya kumfuatilia.

Mgonjwa, hakupokelewa na ndugu au jamaa yeyote hapo uwanjani, kwa hiyo kaamua mwenyewe kwenda hotelini? Alisafiri vipi toka hapo uwanja wa ndege hadi hotelini?

Utashi wake mwenyewe, akaamua akae hapo hotelini, huenda kwa kujishuku kuwa anao ugonjwa.
Kwa nini alijishuku. Taarifa hii aliwaeleza watu wa hapo uwanja wa ndege?

Akiwa kajiweka karantini, palikuwepo na tahadhari ya kutoeneza ugonjwa kwa wahudumu hapo hotelini?
Hawa waliomhudumia katika maeneo yote haya, dereva na hotelini wamekwishatambulika na kupimwa kama hawakuambukizwa?

Alipotoka hotelini kwenda hospitali, hapakuwepo na uwezekano wa kueneza ugonjwa?

Wizara imefanya juhudi zipi kuwatafuta watu aliokaribiana nao toka kwenye ndege hadi alipokwenda hospitali. Hawa hawawezi kuwa nao sasa wanaeneza ugonjwa huko mitaani?
 
UZEMBE + MZAHA + KUTOKUJALI ...KAMA KIPIMO KINAWEZA KUONYESHA MTU MZIMA ILIHALI NI MGONJWA BASI WENGI WAMEPITA AIRPORT NA WAKO MITAANI/ NA INAKUWAJE MGONJWA YUKO ARUSHA MPAKA SAMPULI ZITUMWE DAR? NIONAVYO SASA TUMEKWISHA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna vaccination na watu wengi hawajawahi kuugua huu ugonjwa kwa hiyo hakuna kabisa herd immunity. Watu vichwa ngumu wakileta kiburi kwenye hili, nawambieni na wao watakwenda na maji. Iran na Australia, wabunge na mawaziri wameupata.
 
Tanzania imethibitisha kisa kimoja cha virusi vya corona. Mgonjwa ni mwanamke wa miaka 46 raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji kwa ndege ya shirika la ndege la Rwanda Air.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy Mwalimu, Mwanamke huyo alitoka Ubelgiji na alikuwa anaishi kwenye nyumba ambapo kuna mwanaume alipata virusi vya corona, baadae aliamua kurudi nchini na alipopimwa uwanja wa KIA alionekana mzima hana maambukizi kisha akaamua kujitenga na kujiweka karantini yeye mwenyewe na kukaa hotelini.

Baadae mwanamke huyo alianza kujisikia vibaya na kuamua kwenda hospitali ambapo alipopimwa akathibitika kuwa na virusi vya Corona.
Duh...!.
P
 
Yes hili linawezekana sio wengine wanavyoandika wanafikiri nchi ni kama kuongoza familia ya mke aliyeishia la saba na mtoto wa miezi mitatu.
So ulivyosikia kufunga mipaka akili yako ilikuwa inawaza kufukuza watu wote hata raia wa nchi?
Unatumia Nini kufikiri? Mbona akili nyepesi kabisa kuwa unapofunga mipaka maana yake aliyeenda kuzurura akirudi awe tayari kuswekwa karantini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom