Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa hizo za kuhuzunisha kuhusu kuwepo kwa mgonjwa wa Corona nchini kwetu .

swali la kujiuliza kwanini serikali haikuchukua hatua za haraka kudhibiti ugonjwa huu ikiwa no pamoja na kufunga mipaka kuzuia ndege na magari yote toka nje ya nchi ?serikali inawezaje kukwepa lawama hizi
Tumelipigia kelele sana hawatakuwa na cha kujitetea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binadamu wabinafsi sana Dunia Ina watu zaidi billion 5, Corona inataka kuchukua watu milion 50 tu ili ibalance ecosystem na kufanya depopulation, binadamu wa Duniani hawataki.

Karibu Tanzania Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajuwa kuwa na ww unatakiwa uwe mmoja wapo ili utuache sisi wengine tukimalizia kuweka sawa mambo yetu...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Corona ilishaingia Tanzania ilikuwa swala la muda tu kutangaza sisi sio Kisiwa.

Hizi nchi za kijamaa zina Siri sana, Mungu atunusuru isisambae zaidi.
Nami nasadiki hilo, serikali ya awamu ya tano huwa ni ngumu sana kuukubali ukweli, yawezekana wahusika walitishiwa kutokusema haraka haraka, na umaskini wetu huu imefika wakati wa kuwapigia magoti mabeberu tuliokuwa tunawananga.
 
Nimeshangaa kuona hospitali ile ile iliyotajwa na Kigogo ndiyo ile ile imetangazwa kua mgonjwa yupo apo.Mwisho kwanini serikali iliendelea kupokea ndege zinazotoka kwenye nchi zenye huu ugonjwa.Mwisho ,CCM na serikali yake ebu acheni kungangia vitu
 
Na mimi nilishangaa sana. eti bado tulikuwa tunapokea ndege kutoka katika nchi zenye wagonjwa wa Corona.

Huu ni uzembe mkubwa.

Wizara ya afya imeweka maisha yetu rehani eti kwa sababu ya utalii nk.


Wanapaswa kuwajibika kwa kujiuzuru mara moja.

Wiki zima tuliona ni siasa tu zikiendelea.
 
Hii nchi Kuna Mambo hatuko serious,yani ingetakiwa tufunge mipaka na kuzuia wageni walotoka nchi za ulaya ambayo ndio kitovu Cha corona sasaivi kutokuingia nchini mpaka pale hali itakavyotengamaa,yani hata Kama ww ni mtanzania na ulikua huko ulaya unataka kurudi Tz hairuhusiwi mpaka pale hali itakavyokua shwari Sasa sisi tumekalia kusema tuchukue tahadhari wakati watu walotoka bara la ulaya wanazidi kumiminika kia!! Serikali ijaribu kua serious.
 
Msiwe na presha, huyo ni moja aliyepimwa, Corona probably iliingia Tz wiki zilizopita, we unadhani wachina walioachiwa kuingia ovyo wote walikua safe?

Ni ka mafua tu unaipata unadhohofika siku chache unapona msiwe na presha hata mimi huku nje nahisi nilipata maana nilikua na dalili almost zote sijatoka nje mwezi mzima sasa hivi dalili zimepotea zote naendelea kawaida tu, sikwenda kupima maana walisema si lazima kama haupo critical.

Wazee na watu wenye magonjwa makubwa au kinga ndogo ya mwili ndiyo watapata shida sana na hii kitu, ila kama watoto wapo safe sana wao ni 0.2% wanapata serious complications. Mkipanic mtaongeza tatizo badala ya kulipunguza, na Tz huwezi mwambia mtu akae ndani huku wengine wanategemea kazi za buku mbili tatu kila siku.
 
Sikio LA kufa halisikii dawa

hata Umii anatangaza kimasiharamasihara...hayuko serious na wanyonge anaowaongoza juu ya afya zao!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom