Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Namba za kupiga simu bure endapo utaona una dalili au utaona mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa Korona

0800110124
0800110125
Namba hizi kupiga Ni bure hata kama hauna salio kwenye simu yako.

DALILI ZA UGONJWA WA CORONA
Dalili zionekanazo mara kwa Mara:
• Homa
• Kikohozi kibichi
• Uhemaji wa tabu
• Maumivu ya mwili
• Kuuma kwa koo mfano wa
matonses (tonsillitis)
• Kukosa hamu ya kula
Dalili za mara chache:
• Kuhara
• Kutapika
• Kichwa kuuma
• Kukohoa damu
• Maumivu ya kifua
Nani hupatwa na korona?
• Watu wote (wakike kwa kiume) waweza
kudhurika na korona
• Wenye maradhi yanayoshusha kinga mwili huwa na hatari kubwa Zaidi.
• Wazee pia wapo katika hatari kubwa kupatakorona kwani wana kingamwili hafifu.
KINGA:
• Kuosha mikono vizuri kwa maji safi na sabuni
• Tumia vikinga pua na mdomo (masks) ikiwa unahudumia washukiwa wa korona.
• Epuka kugusa na kurekebisha kikinga mdomo na pua (mask) na uso.
• Zingatia walau umbali wa futi 6 kutoka kwa mgonjwa mwenye korona
• Hakuna chanjo mpaka sasa
Kirusi cha korona katika mwili wa
binadamu:
• Huchukua siku 2 mpaka 14 (wastani siku 5) kwa binadamu kuanza kuonesha dalili baada ya kuambukizwa na virusi vya korona (incubation perion)
• Huambukizwa kwa njia ya matone yatokanayo kwa kukohoa au kugusana moja kwa moja.
• Epuka kusalimiana kwa mikono
MUNGU TUSAIDIE
 
Dharau ni kitu kibaya sana katika maisha, usipokuwa makini unaweza hata kujidharau mwenyewe. Siku zote anayedharau hujiona shujaa, ila matokeo yanapotokea hubakia kuvimba macho kwa aibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KUMBE MGONJWA HAPO AIRPORT ANAPIMWA TU HOMA SIO VIRUS.

LABDA TUWEKE KANUNI, KWAMBA ABIRIA WATAWEKWA KTK UANGALIZI KWA SIKU 14 KABLA HAWAJACHANGANYIKA NA WATANZANIA WENGINE WA MITAANI.
 
Huyu mtu akifungwa afunguliwe kesi ya money laundry na uhujumu uchumi. Fikiria ndani ya muda mfupi alivyozurura, mara sweden, Mara Norway mara Ubelgiji kibaya zaidi anakwenda nyumba zenye wagonjwa, na bado akaja Tanzania, kwenye denge kasambaza, uwanja wa ndege kasambaza, hotelini kasambaza na hospital kasambaza
Kwahiyo kwanza afungwe halafu ndio afunguliwe kesi
Halafu huyu lazima atakua ni mtu anaejiweza
Labda iwe ameuleta maksudi
 
The Dark Father,
nawaza aliyemgongea pasport,
aliyegusa begi lake, aliweka mzigo kwa toroli, aliyetoa mizigo, watu wa customer wakakagua mizigo yake.

alibebwa na dereva taxi akampeleka hotelini baada yakumshusha akaendelea na hamsini zake kuwabeba abiria wengine, wengine wakakaa kiti alichokaa, kule kwenye ndege toka kote uko aligusana na watu, aligusa vifaa vingi vya kwenye ndege na maiaports, akakutana na mtu wa reception hotelini akamuhudumia, mtu wa house keeping akambebea mzigo may be.

mtu wa restaurant akampelekea chakula chumbani siajabu akagusa vitasa vya milango.

hawa wote mwisho wa siku wakarudi majumbani kwao kupumzika wakazikuta familia zao huko wakainteract.

Familia zikaamka asubuhi leo zika amka kwenda kwenye shughuli zao and the cycle continues

MUNGU NA ATUPONYE KATIKA HILI.
 
MTU akapimwa akakutwa hana ugonjwa alafu yeye hakuridhika akajiweka karantini
Hili limedhihirisha mfumo wetu wa vipimo ni ovyo kabisa
Viwanjani wanapima jotoridi LA mwili ambalo kiuhalisia MTU akiwa kwenye incubation period linakuwa normal... Inshu ulikuwa ni kuwaweka watu wote wanaoingia kutoka nchi zenye maambukizi kalantini, ila hata hili nalo bado lingekuwa gumu, unafunga tu mipaka yako baasi kama Israel, India na hata marekani.. Kupambana na COVID aise si mchezoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viwanjani wanapima jotoridi LA mwili ambalo kiuhalisia MTU akiwa kwenye incubation period linakuwa normal... Inshu ulikuwa ni kuwaweka watu wote wanaoingia kutoka nchi zenye maambukizi kalantini, ila hata hili nalo bado lingekuwa gumu, unafunga tu mipaka yako baasi kama Israel, India na hata marekani.. Kupambana na COVID aise si mchezoo

Sent using Jamii Forums mobile app
Je, vifurushi na mizigo inayoingia ndani nayo izuiwe?
 
Yote na yote hii batani imeguswa tu lazima kuna target.hakuna dawa why china italy ndo wahanga?


Urusi urusiiiii
Screenshot_20200316-164522.jpeg
Screenshot_20200316-164532.jpeg
Screenshot_20200316-164541.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tahadhari zote za muhimu zinafahamika hapa ni kila mmoja na familia yake kuweza kuilinda..... Kuanzia leo hatoki MTU ndani na bar ndiyo baasi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom