Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Ni lawyer, walau angekuwa na ka MD, asingezingua hivi. Ninakumbuka maneno ya Prof mmoja Muhas Enzi hizo, aliyekuwa anawashauri Madaktar kujiingiza kwenye siasa. Hii ingesaidia kuondokana na watu wasiojua medicine kuongoza wizara ya afya. Madudu kama haya yangepungua.
Nilikuwa nadhani ana hata ka MD kumbe amesoma sheria..ndo maana
 
Fuata maelekezo ya kujikinga,achana na fafanuzi utakufa wewe

Laws za probability zinaniambia kulikuwa na uwezekano mkubwa zaidi corona kuingia Tanzania kupitia kwa watalii, hasa wa kutoka nchi kama Italy na siyo hizi habari sijui za mama wa Kitanzania mara alikuwa Denmark, sijui Norway sijui Belgium, mara alikuwa anaishi na baba mwenye nyumba aliyekuwa na corona. Come on now!
 
Huu ni uzembe ambao hatupaswi kuufumbia macho na wanaohusika wote wawajibishwe. Abiria wanafika airport mnawaachia kama mbuzi bila kuwaweka karantini kwa muda ili kutambua wenye maambukizi.

Bado serikali ya Tanzania haijachukua hatua madhubuti kuhakikisha wananchi tunajua salama. Sasa endelea kujifanya haupokei ushauri ndio utaona matokeo yake.
Kwa serikali hii janga kuu kwao ni upinzani, hayo mengine wanaona ni upepo utapita tu. Kumbe ndio wanaziba shimo la panya kwa mkate.
 
yote umeandika poa, ila umeharibu ulipoingiza mambo ya vyama kwa swala la kiafya kama hili, usiweke siasa kwenye uzi mzuri kama huu uliouanzisha, ili tuchangie kuhusu hatima yetu inakuwaje kiafya...

Sent using Jamii Forums mobile app
KWani si ni kweli Serikali Iko busy kushughulika na na upinzani hasa Chadema. Sidhani kama kuna siasa hapo.

Hii ni serikali ya hovyo zaidi kutokea katika historia ya nchi yetu. Imagine mtu mpaka anajipeleka mwenyewe hospital ndio wanagundua ana Coronavirus.

Sijui angeuchuna ingekuaje sasa?!
 
Ni kweli kabisa Kila Mkoa lazima uwe na Tents, lakini nafkiri pia ni wakati sasa kwa nchi kuchukua hatua stahiki kuzuia maambukizi mapya, nahauri tena Shule hasa za Msingi zianze kufungwa, watoto wetu hawawezi kuchukua hizo tahadhari kikamilifu, ifuatiwe na Shule za Sekondari Vyuo na maeneo ya starehe, kazi za lazima zifanyike kwa njia ya kietronic, likizo za lazima kwa watumishi wote ni muhimu, na mengineyo ya tahadhari yafanyike, tusiache ugonjwa utamalaki ndo tuchukue hatua, tutakufa kama Kuku Wa Kideri
Isolation ni lazima kwa kila Mkoa na hata wilaya
Hospital zote ziwe na tents au nyumba za dharura nje ya hospitali kuzuia magonjwa kusambaa
Ni lazima wataalamu wapewe nafasi ya kuongea ukweli na waandishi wawahoji sio kukimbilia kwenye press za Waimbaji na wanasiasa
Hili ni janga la Dunia na dunia nzima iko juu juu, Viongozi wote wako live kila wakati
Chief medical officers wanatoa ushauri ila sisi tunaona kawaida sana
Mataifa mengi uchumi umeanza kuyumba haswa na hela zinaelekezwa kuokoa maisha ya watu wao
Maabara wako 24/7 kutafuta chanjo ya maradhi Haya, sisi tutasubiri tuletewe baada ya maafa makubwa?


Sent from my iPhone using Tapatalk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Manina,,,Halafu kuna usaili hapo chuga weekend hii
What a time to die bila hata kufaidi keki ya taifa?
 
Mimi nilihisi kuwa labda ni sababu Moshi kuna Joto Kali na Arusha kuna Baridi, na si unasikia kuwa Corona Viruse hawana ubavu Wa kuishi katika Joto Kali, Moshi Joto ni centigrade 32 na wako hawawezi kuishi katika note zaidi ya 20 c ,tunavyosikia. Je lina ukweli hili, wataalam tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni hivo wagonjwa wote wapelekwe Dar
 
Tuipende nchi yetu jamaaa alietulaani ni mbaya sana
 
Wanaweza ku-trace contacts wote, kuanzia kwenye ndege(walioshuka KIA) hadi alipojipeleka hospital
 
Magu hana nia njema kwa raia wa nchi hii. Anataka kuona watu wakpata tabu kwa sera yake ya "Expect No Mercy"
 
Jamani huku kukosoa kwa kutaka kukosoa tu hakuleti tija. Hivi kweli inawezekana serikali imlipe mtu kuleta ugonjwa nchini? Na kama ndivyo, inafanya hivyo ili iweje? Imeelezwa kwamba mtu huyu alikuwa exposed kwa mgonjwa, kitu ambacho kinaweza kumfanya aambukizwe au la. Mpaka alipoondoka huko alikokuwa, alikuwa hana dalili za ugonjwa na hata hapo KIA hawakuona dalili za ugonjwa na ndiyo maana akaruhusiwa kuingia uraiani. Kesho yake dalili zikajitokeza. Ndiyo maana akajitokeza hadharani kwa kuwa alijua kuna uwezekano aliambukizwa kwa kuwa alikuwa exposed kwa mgonjwa. Tumeelezwa kwamba ukiambukizwa ugonjwa huu unaweza kukaa hadi siku 14 kabla ya dalili kujitokeza na ndiyo maana watu wanawekwa karantini siku 14. Hakuna maana kuanza kuchokonoa iweje mgonjwa huyu ajitokeze baada ya siku 10(?) za exposure na kuanza kutilia mashaka kwamba mtu huyu alilipwa alete ugonjwa nchini. Huku ni kupinga juhudi za serikali kwa madhumuni ya kupinga tu. Kama una ushahidi wa habari kuwa vinginevyo basi toa ushahidi huo moja kwa moja. Siyo kutaka kutumaanisha sisi kwamba serikali imefanya njama za kulipa mtu alete ugonjwa nchini.
 
Back
Top Bottom