#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

Status
Not open for further replies.
Usisahau kuna $1bilion zinatolewa! Kwa taifa waathirika!
 
Mambo yakibumbuluka sijui itakuaje
Misaada ya kiafya tusitarajie kabisa Maana wenyewe wako katika kujisaidia

Ntafanya Hima niache damu yangu duniani
Nife sijaach mtoto, How comes [emoji16][emoji16]
 
Binafsi nitaivunja hiyo karantini nipe code tu itajengwa kwa chuma au aluminum...??
 
Inaonekana Tanzania tunapendwa sana na mungu kuliko nchi zote duniani,hizo nchi nyingine wakifa sawa tu mbele za mungu.acheni kujipa moyo,we subiri gonjwa lije ndio utajua jinsi la kupambana nalo..."SALINI SANA MAANA HAMJAJUA SIKU WALA MDA".
 
Habari ndiyo hiyo wazee nunueni sabuni ya dettol kwa matumizi ya kunawia mikono,uso hata kuogea kwani inaondoa kabisa virus vya Corona mwilini.

Kumbuka hii sio tiba bali ni sabuni ya kusafisha mwili,nyumba,nguo n.k
SHARE KADRI UWEZAVYO,MOD UMSIHAMISHIE HUU UZI JF DOCTORS KWA MANUFAA YA UMMA.
images.jpeg
 
Tunatakiwa kunawa kila wakati, kukaa umbali wa angalau futi 6 toka kwa mgonjwa, kufunika pua na mdomo tupigapo chafya au kukohoa.

Je matumizi ya fedha, sarafu na noti katika manunuzi ya kila siku hayawezi kusambaza Virusi vya Corona?.

Karibuni wanaJf kwa mawazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa ndio mgeni CORONA keshaingia Tanzania.Lakini nafikiri hatutakiwi kupanic.Maana HAMAKI ni mbaya kuliko ugonjwa wenyewe.Tuendelee kujikinga huku tukiomba hili nalo lipite.Mbona hata EBOLA ilitingisha lakini nayo ilipita.

Mungu ibariki Dunia
Mungu ibariki Africa
Mungu ibariki Tanzania.
 
Kwetu sisi tunaotumia usafiri wa umma tunasema serikali mnabaki kupapasa papasa vitu ambavyo ki mtizamo vina athari lakini vipo vitu vyenye athari kubwa zaidi mmekaa kimya.

msongamano wa watu kwenye usafiri wa umma ni tishio namba moja kwenye maambukizi ya Korona.

Tunaomba serikali kwa haraka sana mpunguze misongamano kwenye usafiri wa umma.

hapa mnaweza kufunga shule, mkafunga baadhi ya shughuli zisizo na ulazima na kupiga marufuku kusimamisha abiria, misongamano n.k.

Yaani kama mtu amekuja akaingia nchini hamkuona, kajiweka karantini mwenyewe akajigundua ndio karudi hospitali mwenyewe.

Je yawezekana wapo wangapi wa aina hii ambao pengine hawako makini kama huyu?.

Cha msingi tunusurie watoto kwanza maana hao kuwadhibiti shida kubwa na pia tunawathamini hao.
 
Leo kumetokea tatizo la usafiri Mbezi na watu kujazana vituoni baada ya kukosekana usafiri.

Leo pia kumethibitika kuwepo kwa mgonjwa wa Corona Arusha.

Leo pia hadi sasa ambapo kumetokea mgonjwa bado daladala Arusha, Moshi, Dar, Mwanza na mikoa mingine zinajaza abiria kiasi kwamba hata ukinawa bado siyo kinga.

Viongozi wa kisiasa bado wanaendelea na mikutano ya siasa na wananchi bila kuweka maji ya kunawa kwenye mikutano yao.

Wanafunzi bado wanasongamana mashuleni.

Bado Serikali haijasambaza vifaa vya kunawia mashulen na mahospitali

Bado Serikali inatoa maelekezo yanayohitaji fedha mfano wanaposisitiza kunawa mikono bila kusema maji na vifaa vya kunawia vinatoka wapi inakuwa ni vigumu kuamini nia ya serikali kukabiliana na tatizo.

Ni muda sasa Serikali kuweka nguvu kwenye afya za wananchi na kuachana na miradi mingine hadi tatizo lipite.

Ikiwezekana maabara zisambae kikanda kupunguza muda mrefu wa kwenda Dar kupeleka sampuli.
 
Zile gari za kubebea wanachama wa Ccm kwenye uchaguzi tunaomba tuletewe huku mbagala kwa kipindi hiki bila kusahau buza.
 
Kitu muhimu. Kwanza kila mtu ajikinge nyumbani kwake na mazingira anayoishi. Ndipo serikali nayo iweke taratibu za kupambana na hili jambo. Nje ya hapo tutaishia kuilaumu serikali.

Unakuta mtu analalamika juhudi za serikali kuzuia covid wakati mlalamikaji hata kusalimia kwa mikono bado anafanya. Au hata kunawa mikono mara kwa mara hanawi.
 
kifupi kirefu,
Hivi unafikiri wako serious. Labda baada ya mtu kufa ndiyo akili itakuja. Hukumuona Ummy anavyoongea kwa mzaha mzaha kwenye Press conference. Eti anawacheka watu wake kwa kusahau makaratasi ....

Yaani anacheka utafikiri yuko kijiweni!! God forbid.
 
Wataalam wanaamini kuwa kirusi hiki kinaweza kukaa hadi wiki 5 kuweza kutambulika.

Ndio maana huyu mama wa Tanzania wameni-scan lakini akaona mwenyewe ni busara kujitenga na watu.

Sasa ni wangapi waliopitia temperature scanning wakajiaminisha ni wazima na wako mtaani?.

Ila tuwe na amani
 
Wataalam wanaamini kuwa kirusi hiki kinaweza kukaa hadi wiki 5 kuweza kutambulika. Ndio maana huyu mama wa Tanzania wamenscan lakini akaona mwenyewe ni busara kujitenga na watu.

Sasa ni wangapi waliopitia temperature scanning wakajiaminisha ni wazima na wako mtaani?.

Ila tuwe na amani
Kikubwa kila mtu afanye jitahada zake kwanza kwa kadiri atakavyoweza kwa tahadhari,mfano jizuie mwenyewe kwenda kwenye mikusanyiko,mask puani,kutokushikana mikono,kunawa na sabuni yenye dawa n,k.

Mambo mengine ambayo sisi hatuna mamlaka nayo itabidi kupaza zaidi sauti ili mamlaka angalau zifungue macho kufanyia kazi,mfano wa kuzuia wageni ama kuwaweka karantin kwa muda,nakadhalika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa Wilaya ya Longido amesema wamepeleka watendaji wote na vifaa vya kisasa vya kuhakiki na kudhibiti Corona.

Miongoni mwa vifaa hivyo ni pamoja na kipimo kinachoweza kumtambua muathirika katika umbali wa mita 10 na Vipima joto.

Source ITV Habari!
 
Dalili zinaonekana kati ya siku 2 Hadi 14. Watapita wakiwa Carrier, watabukiza waTz. Kama kuna utashi usio na gharama ni kufunga mipaka angalau siku 14 halafu unafungua. hivyo hivyo mpaka upotee. Mipaka ikibaki wazi hakuna namna tutegemee Bwana wa Majeshi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom