Kwetu sisi tunaotumia usafiri wa umma tunasema serikali mnabaki kupapasa papasa vitu ambavyo ki mtizamo vina athari lakini vipo vitu vyenye athari kubwa zaidi mmekaa kimya.
msongamano wa watu kwenye usafiri wa umma ni tishio namba moja kwenye maambukizi ya Korona.
Tunaomba serikali kwa haraka sana mpunguze misongamano kwenye usafiri wa umma.
hapa mnaweza kufunga shule, mkafunga baadhi ya shughuli zisizo na ulazima na kupiga marufuku kusimamisha abiria, misongamano n.k.
Yaani kama mtu amekuja akaingia nchini hamkuona, kajiweka karantini mwenyewe akajigundua ndio karudi hospitali mwenyewe.
Je yawezekana wapo wangapi wa aina hii ambao pengine hawako makini kama huyu?.
Cha msingi tunusurie watoto kwanza maana hao kuwadhibiti shida kubwa na pia tunawathamini hao.