#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

Status
Not open for further replies.
Hakuna njia mbadala zaidi ya kutengeneza mazingira ya joto( kujifukiza ni moja wapo) .joto huwa linaharibu kabila structure ya protein hivyo corona ni protein ataharibika kwa njia za joto.maendezo ingia wikipedia
 
Rais wetu alitumia neno mafuta baada ya GLYCO PROTEIN . Ili aweze kueleweka kwa watu wengi neno glycoprotein coat of coronavirus ni gumu kueleweka. Ndio maana akaweka neno mafuta, concept ni denature au kuharibika kwa coronavirus. Njia ya joto. pia njia ya acid si kunywa asidi bali kujisafisha kwa chemical za asidi .eg SABUNI YA OMO Au Dentergent inaua virus kwa kihaibu layer yake nje
 
Expanded signs and symptoms of Covid- 19

1: Chills
2:repeated shaking with chills
3:loss of sense of smell
4: Loss of sense of taste
5:Sore throat
6:Muscle pain
7: fever
8: Nausea
9😀ifficulty in breathing
10: chest tightness
11: Dry cough.

#chukua tahadhari Corona IPO ni hatari inaua
.
# Epuka kutembelea wazazi na ndugu zako hasa wazee hasa kipindi hiki

#wanafamilia wako wakae nyumbani kama hawana kazi maalumu ya kuwatoa nje

#Epuka mikusanyiko isiyo ya lazima hasa baada ya kazi zako

#Zingatia social distance, kunawa mikono, kujipaka sanitizers, Vaa barakoa zinasaidia

#Jitahidi kutumia juisi ya Machungwa na limao ni muhimu sana

#Machungwa na limau ni muhimu sana kipindi hiki

#Supu ya maharage ni bora sana kwa kipindi hiki

#Mboga za majani ni muhimu

#Fanya mazoezi kama unaenda sehemu ambayo hauna haraka usipande daladala tembea kwa muda mrefu kama hauwezi kufanya mazoezi ya kukimbia

#Epuka kutumia pombe, Sigara kama hautaweza punguza matumizi yake.

#Usisahau kujifukiza asubuhi mapema na jioni ni muhimu sana.

~#VITA DHIDI YA CORONA INAANZA NA WEWE
 
🚙🚙🚙🚙🚑🚑🚔🚔🚔 ukiona msafara wa Toyota Land Cruiser nyeupe, zenye msalaba wa kijani na gari ya polisi wenye silaha Kali, jua wanaenda kupiga ambush mahali, Kuna mgonjwa mwenye dalili za Corona, mnakamatwa wote mliopo eneo hilo na kupelekwa jela iitwayo karantini
 
Je tiba asili, mimea na chakula yaweza kuongeza kinga ya mwili dhidi ya virusi vya Corona?
 
Kunawa mikono pekee haitoshi jamani, nimeangalia hii video nikasema tusipochukua hatua tutateketea kwa wingi.

Naomba kila mmoja aangalie japo maudhui yapo kwa lugha ya kiingereza lakini kila mtu anaweza elewa kinachoonyeshwa kuhusu usambaaji wa corona kwa njia ya hewa.

 
Utamtemeaje mtu mate
Nimecheka saaana, kumtemea mtu mate (kurusha mate)
kuna jamaa ngazi za juu kuliko alikuwa lecture Mlimani, akiongea mate huruka mita 3 sasa hizo microphone zitaacha kulowana?
 
Wakuu.
Poleni sana na mihangaiko pamoja na hili janga la covid 19 lililozua taharuki duniani kote na kusababisha maafa na vifo katika nchi nyingi.Ama kweli litakumbuka daima vizazi na vizazi.Mungu atuepushe na mabaya yatokanayo na janga hili pia tuzidi kufuata maagizo yatolewayo na wataalamu wa afya.
Ni wazi kuwa kwa sasa kirusi kipo ndani ya 18 zetu;nikimaanisha kipo mtaani.Kuna wagonjwa kadhaa wapo karantini na wengine wapo majumbani wasijue wanacho.Wapo wanaoonyesha dalili na wengine hawaonyeshi.Dalili za mara kwa mara ni: 1.Homa
2.Kikoozi kikavu
3.Upumuaji wa shida.
Pia zipo nyingine minor ambazo hazitokei mara kwa mara kama mafua n.k
Sababu pia na ugonjwa wenyewe ni mpya na unazidi kufanyiwa uchunguzi miongoni mwa wagonjwa,kuna dalili pia zingine zimeonekana kwa wagonjwa kama vile: Kupoteza uwezo wa kunusa au kusikia/kuhisi ladha ya chakula mdomoni au uchovu.
Hivyo basi kama wewe ulithibitishwa kuugua ugonjwa huu ama ulipata dalili tajwa hapo juu au zingine zilizoongezwa na wataalamu wa afya na ukapona basi usisite kupitia hapa na kutueleza mbinu ulizotumia.Hii itawasaidia wengine wanapokumbana na hali kama hii.Ni vizuri ukaeleza clearly ili kuwapa mwanga watu wengine.
Karibuni.
Ila ningeomba watu kutoingizia siasa au kutumia sehemu hii kukumbishiana mabifu yao waliyowekeana nyuzi zingine huko.
#UtaniUsizidiKipimo
Karibuni tena.
 
Asante kwa elimu hii konki kuhusu virusi wa korona. Mungu akubariki sana mkuu
 
Habari za muda huu waungwana na poleni na majukumu ya kila siku.

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada au swali ambalo limenifanya niandike uzi huu. Kuna maumivu napata juu ya tumbo langu ambayo sijawahi kuyapata kabla ni chini ya kifua na ni kwa upande wa kushoto na kulia sio maumivu makali bali ni jambo geni katika mwili wangu na hali hii ina siku ya sita tangu nianze kuiskia.

Ila sina dalili nyingine yoyote ya coronavirus kama vile homa mafua kifua mwili kuchoka yani nipo fresh kabisa nilikuwa naomba kujua hapa panaponiuma ndo kwenye mapafu? Au hii ni shida nyingine. Nauliza kwani nimepata taarifa kwamba unaweza kwenda hospital wakakuweka Quarantine na wagonjwa wa Corona ili usubirie vipimo vikaja negative ila ukaipatia hapo kwenye kumsubiri vipimo/ majibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nimetokewa na iyo hari over two weeks now, ila nilichoamua kufanya leo ni kujifusha tu ndio naona niko poa sasa ila tatizo limebaki kooni yaani kama nimepaliwa na mate ivi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom