#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

Status
Not open for further replies.
Unampa dawa kutibu zile symptoms anazoonesha.
Mfn kukohoa, mafua, za maumivu, mashine ya kupumulia, kupandisha body immune n.k

Yaani mwili unarahisishiwa halaf wenyewe ndio unafanya mashambulizi ya kuua wadudu.

Ukishindwa sasa ndio maturubai na
hawa watuView attachment 1425972
Dah!
Hawa nao watakua wanasubiri tenda?
 
Corona inaambatana na dalili kama vile maumivu ya kichwa, mafua makali, kikohozi, homa kali,maumivu ya koo pamoja na kupumua kwa shida.

Hivyo basi hivyo viambata ndivyo vinavyotibiwa ili kupunguza kasi ya mashambulizi yanayopelekea kinga ya mwili kushuka. Ni sawa na ilivyo kwa maambukizi ya H.I.V, hakuna dawa inayotibu H.I.V ila wanatibu magonjwa nyemelezi ili kupunguza kasi ya mashambulizi yanayopelekea kinga ya mwili kushuka kwa haraka.
 
Corona inaambatana na dalili kama vile maumivu ya kichwa, mafua makali, kikohozi, homa kali,maumivu ya koo pamoja na kupumua kwa shida.

Hivyo basi hivyo viambata ndivyo vinavyotibiwa ili kupunguza kasi ya mashambulizi yanayopelekea kinga ya mwili kushuka. Ni sawa na ilivyo kwa maambukizi ya H.I.V, hakuna dawa inayotibu H.I.V ila wanatibu magonjwa nyemelezi ili kupunguza kasi ya mashambulizi yanayopelekea kinga ya mwili kushuka kwa haraka.
Asante
 
Wakuu.

Wanasayansi ndio kwanza wanaanza kukidadavua na kukielewa kirusi hiki kipya ambacho kimepewa jina la Corona virus 2.

Mengi kuhusu kirusi hiki bado kujulikana ila kama adui dhidi ya mwili wa binadamu kinashambulia:

1. Njia za hewa na mapafu
Huu ndio uwanja mkuu wa mapambano ambapo adui huyu anaushinda mwili na kuleta kifo.
Kirusi hiki kinaingia kwenye chembe chembe za mwili kupitia vipokezi viitwavyo ACE 2 ambavyo ni vingi zaidi kwenye njia za pumzi na chembe chembe za mapafu.

2. Utumbo mwembamba.
Kiungo hiki pia kina chembe chembe zenye ACE 2 nyingi hivyo kuruhusu mashambulizi na ndio sababu kuhara ni moja ya dalili za Covid-19.

3. Figo.

4. Maini.

5. Mishipa ya damu(arteries).

5. Ubongo.

6. Macho.

Mashambulizi hayo yanatoa vidokezo vya kwanini wenye maambukizi ya HIV, wagonjwa wa pumu, kisukari, moyo na pia waliozeeka ni wahanga rahisi wa Covid-19.

Kwa uchache kirusi kinaupiga mwili wa mwanadamu kuanzia nyayo hadi utosini.

Mengi hayajagunduliwa bado kuhusu kirusi hiki lakini yanayojulikana tayari yanadhihirisha kuwa huyu ni adui mwenye nguvu anayepaswa kukabaliwa kwa umakini mkubwa, nguvu na rasilimali pia.

Kwamba adui huyu atabadilisha mifumo ya maisha yetu kijamii, kiuchumi na kisiasa ni jambo ambalo lazima tulitarajie.

See ScienceMag.org
How corona virus kills.
 
Nahisi bado hatujamwelewa vizuri adui huyu ndo maana kila mtu anajaribu lwake. Jana nmeskia ata kujamba kunaambukiza Corona kwa mgonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sisi tunaolazimika kusafiri mara kwa mara, hofu imetutanda kweli kweli! Ujasiri wote kwisha. Ni mwendo wa kuishi tu kwa imani maana hatujui kesho yetu.

Huu ugonjwa ifikie wakati uishe tu ili maisha yaendelee. Kujikinga na mambo mengine yakiwemo 'maombi' bado hayaondoi kabisa uwezekano wa kuambukizwa.
 
Kuna Mahusiano kati ya kuharisha na tatizo la kiafya.
 
Wakuu naomba tusaidiane hatua za kuchukua unapohisi dalili za korona. Dawa gani unapaswa kutumia kama tiba ya awali kabla hujafika hospital. Naona kila mahali wanasema unatibu dalili, naomba kujua dawa nzuri kwa hizo dalili mfano dawa nzuri ya mafua hayo, dawa nzuri ya kikohozi hicho, dawa nzuri ya pneumonia, jinsi ya kushusha joto la mwili nk.

Nauliza hivyo kwa tahadhari tu maana unaweza kuhisi dalili, ukachukuliwa sampuli ikatumwa dar es salam mpaka majibu yanatoka si inabidi uwe unatumia dawa?

Unaweza kwenda kupima kwenye vituo vidogo vidogo sijui wanaangalia nini nasikia wanapima joto tu, wanaweza kusema haumwi hivyo wasikuchukue sampuli ila wewe bado unajisikia dalili.

Siombei ila inaweza tokea hospital zikazidiwa na wagonjwa wale wanaojisikia vizuri itabidi wajihudumie majumbani badala ya kuongeza msongamano hospitali.

Nimesoma sehemu Fulani kwamba Kama Hali yako haijawa mbaya unaweza kujitenga nyumbani na ukajihudumia na ukapona bila shida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili la kumkimbilia Mungu ili atunusuru na janga hili la ugonjwa wa Covid-19 ni jambo jema sababu hakuna ubishi kuwa Mungu ni Alfa na Omega. Na hakuna lisilo shindikana kwake.

Lakini pia ni Mungu huyu huyu ambae anatupa akili na uwezo wa kukabiliana na majanga hivyo tunapokuwa na elimu au maarifa ya kukabiliana na janga lolote ni lazima tuzingatie kwa umakini.

Serikali imefunga shule na vyuo, na ikazuia mikusanyiko ya sunday schools na madrasa. Ila ibada za siku kama ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili nafikiri bado sijasikia kama kuna tamko lolote.

Kuna mchungaji mmoja huko USA alipuuza ushauri wa wataalamu kuhusu kuzingatia kukaa mbali kwa mita 1.5 hadi mbili na kilichofuata ni kupata maambukizi na kufariki.

Hivyo kama maambukizi yanazidi kushika kasi basi hata kwenye ibada kwenye nyumba za kuabudu inabidi ukaaji uzingatie kukeep social distancing. Au ikibidi mikusanyiko kama hii isitishwe mpaka hali ya huu ugonjwa itapokaa vizuri.

Rais wa Marekani kwa kiburi aliacha kusikiliza ushauri wa wataalamu na akawa analazimisha watu kuwa ugonjwa huu unaweza kutibiwa na Chroloquine. Wataalamu walimkatalia na kwa kiburi chake inasemekana wagonjwa wengi waliopewa Chloroquine walifariki.

Mpaka jana dawa pekee ambayo imeonekana kuwa ina uwezo wa kutibu Covid -19 ni Remdesivir japokuwa wanasubiri approval toka FDA.

Hivyo wataalamu wetu wawe mstari wa mbele kuwapa elimu watanzania namna ya kujikinga na janga hili ili tusijekujikuta tumeelemewa na wagonjwa.

Sababu mpaka sasa rate ya wagonjwa wanaopona na wanaoambukizwa ni kama uwiano hauko vizuri. Maana mpaka sasa walioruhusiwa ni 11 na vifo 10 lakini reported cases ni kubwa 254.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom