#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

Status
Not open for further replies.
ruhi, Kwa sababu umesema wewe sio daktari basi hamna tabu.

Kuambukiza kwa njia ya hewa maana ni kwamba hicho kirusi hakihitaji mtu kutema mate wala kukohoa , inatosha tu kupumua kwa mtu ila pumzi yake ikimfika mwengine aambukizwe..

Sasa kirusi cha hakipo hivyo..ndo maana wanasema corona haimbukizwi kwa njia ya hewa.

Korona ni mpaka mtu akohoe au apige chafya yale maji maji yanayoruka ndo yanabeba virusi. Sio kwa kule kupumua tu.

Sasa hizo chembe chembe za maji ndo huwa zinaruka kutoka mdomoni au puani na kwenda sehemu nyingine kupitia hewani, KAMA AMBAVYO MTU ANAWEZA KUVIBEBA MKONONI MWAKE NA KUVIENEZA SEHEMU NYINGINE KWA KUSHIKA NA ULE MKONO WAKE..
KWA HIO SIO KWAMBA ETI CORONA INAENEZWA KWA HEWA AU KWA MKONO, HAPANA.

nadhani madaktari wataelewa vizuri zaidi




Sent using Jamii Forums mobile app
 
sio mita sita, sijaangalia hiyo ITV lkn kuna mahali nimesoma ni futi 10 ambayo ni mita 3
na uwe hodari kweli wa kuongea kwa kurusha mate
havidumu zaidi ya masaa 8 na huondoshwa kwa kunawa maji angalau kwa muda
 
Corvid -19 anakaa hewani tena sio kwa sekunda ni kwa masaa kadhaa.
Zaidi ya matatu, hivi nyie madaktari wa bongo data zenu mnazitoa wapi?
Ingekuwa wanakaa hewani kwa muda huo basi mataifa yaliyoendelea yangehimiza barakoa zivaliwe mwanzo mwisho na kila mtu, instead wanahimiza social distancing bila barakoa, and IT WORKS.
 
Nimeona huku mtaani watu wamekuwa na maoni tofauti juu ya suala hili kiasi cha kuzua mjadala mkubwa!Wengi katika kutetea hoja zao wamegusia maeneo haya:

1.Huduma zilizopo hospitali zilizotengwa kwa ajili ya Covid-19!

2.Tiba mbadala kama kujivukiza kama alivyoshauri Rais zinapatikana huko mahospitalini?

3.Kuzuia maambukizi kwa wengine NK!

Ukiwa kama mwana JF,leo yakikukuta utachukua hatua gani?
 
Yaani kuna mda mtu unajikuta una vimafua mara kama homa sio homa mara kicha kama kinataka kiume hakiumi au kuchoka lakini hauchoki kiviiilee mara koo liume haliumi sana yaani hali haileweki eleweki kabisa.

Wakati mwingine mtu unaamka mzima kabisa baada ya mda kidogo unajisiki hasira mpaka unatamani kumng'ata mtu bila sababu.

Mungu atunusuru kwa kweli maana hii hali kila kukicha inazidi kuwa sio.hata wale tuliokiwa tunawategemea ndio wasemaji wetu wa kutupa aptudate nao wameingia chaka.

Chukua tahadhari corona ipo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom