Coronavirus, Tanzania: Shule zote kuanzia za Awali, Msingi na Sekondari zafungwa. Mikusanyiko ikiwemo ya Kisiasa yasitishwa

Coronavirus, Tanzania: Shule zote kuanzia za Awali, Msingi na Sekondari zafungwa. Mikusanyiko ikiwemo ya Kisiasa yasitishwa

Warsha inawatu 10-50, kwa kiwango cha chini nazo zimezuiwa.
Hivi hatuoni umuhimu WA kutoa agizo ofisi zito watumishi waende nusu kwa siku na idadi ipangwe ya wahudumiwa kwa muda mmoja,
Restaurant na masoko yatajifunga yenyewe wala msilazimishe kwao.

Gaweni barakoa bure kila zahanati.

Vyuo navyo visitishe lecture lakini visifungwe Bali waendelee na consultations lkn malecturer ndiyo wajipangie ratiba kupunguza msongamano

Haiwezekan uzuie shughuli za kijamii na umma ukaacha lecture ambazo zinakusanya watu wengi zikiwa wazi.

Ofisi zisizo na ulazima zifungwe, hongera kwa JF lkn hata vyombo vingine vifutilie mbali vipi hasa vya michezo na mahojiano ambavyo havina ulazima

Tukiweza hayo, tutakuwa tumepunguza msongamano hats kwenye usafiri, maduka nk
Maana hakuna atakayenunua vitu kariakoo nawakati hajui atauza wapi na huenda baada ya baa hili being ya hivyo vitu itashuka


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya yote nikiri mimi ni miongoni mwa ninaomheshimu Magufuli na serikali yake pia nafurahishwa na jinsi alivyo mwepesi kwenye kufanya maamuzi mbalimbali bila ya kusita.

Kutokana na mlipuko wa Corona, dunia nzima inajaribu kujilinda kwa kufunga mipaka au kulazimishwa watu kutengwa kwa siku 14 baada ya kuingia kwenye mipaka yao. Inacho shangaza Tanzania tunahangaika na kuzuia mikusanyiko, kufunga shule wakati mipaka tumeiacha wazi. Kilichopo airports zote duniani ni temperature screening kwa kutambua udhaifu wa hili ndio maana nchi nyingi zimeamua kufunga mipaka au kulazimishwa wanaoingia wote kutengwa.

Kwanini kuna kigugumizi kwenye hili, hivi tunazuia UMITASHUMITA na mbio za Mwenge huku mipaka tumeiacha wazi tu, hizi ni akili gani, viongozi wetu wanaelewa risk wanayotuweka, hata tukisema wanalinda soko la Utalii ila ukweli hakuna watalii kwa kuwa karibia nchi zote za Ulaya na Marekani ambazo tunategemea watalii wengi zipo katika hali ya dharura, tunataka hadi ugonjwa uingia mtaani ndio tufunge mipaka?

Wapo ambao wanafikiri kufunga mipaka ni kuzuia pia bidhaa kutoka nje, si kweli, tunaweza kufunga mipaka huku tunaruhusu bidhaa kuingia kwa utaratibu maalum, Uarabuni wanategemea chakula chao chote kutoka mataifa mengine na wamefunga mipaka, hivi tunasubiri hadi ugonjwa uingie mtaani uathiri hadi watu wanaotegemea kufanya kazi asubuhi wapate mlo wa mchana tuwaambie wajifungie ndani? Naamini wahusiki wanapita humu, wajue tumechoka ulegelege wao kuchukua maamuzi ya kufunga mipaka, athiri zote zitazokuja ugonjwa ukisambaa tutawabebesha wao.
Ni kama mwanamke anaficha matiti uchi anaachia
Wengine wanaficha macho huku msela anakula mzigo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasubiria kusikia yafuatayo;
1. Viwanda vilivyoajiri maelfu zifungwe, sijui nini kitatokea.

2. makanisa na misikiti visiruhusiwe kukusanya watu kwa ibada, sijui utaratibu gani utaruhusiwa.

3. masoko yafungwe watu tuwe tunanunulia bidhaa nyumbani kwa wauzaji, huko dar sijui itakuwaje..

4. tuombee sana ugonjwa usifike dar es salaam maana kuna hatari ya kupoteza ndugu zetu nawaza sana hapa.

5. waajiriwa wasiwe wanaonana ana kwa ana makazini, ziletwe mitambo za kufanya kazi badala ya watu ...ajira zife tu.

6. kumbi za starehe na ma-bar n.k yafungwe tukose vinywaji vya kupata mahali pamoja.

7. nawaombea sana kwa Mungu wale wote wenye roho mbaya ambao hawapendi wengine wapate mema, watenda dhambi nawaonea huruma.

8. harusi, birthday, misiba, mahafari nk zipigwe marufuku, watu wafanye kwa namna nyingine hayo mambo yao

Mungu alisema tusimlilie yeye bali tujililie sisi wenyewe na familia zetu, baadae akasema duniani mnazo dhiki lakini jipeni moyo, naiombea serikali kuendelea kuchukua hatua ambazo inahisi zitapunguza uwezekano wa kuleta hatari na taharuki

"huu si wakati wa kulumbana upinzani na watawala shithole person"
 
So kwa sisi wapendwa, Je tuendelee na ibada zetu ndefu na mikesha!!
 
Kuna kitu hakipo Sawa hapa.

Yani kisa mtu mmoja ndo wakoseshe mamilioni ya watoto kwenda Shule?

Muibane Serikali Yenu vizuri, Kuna Kitu nahisi hakisemwi.....

Anyway Ngoja niwai dukani Sijui ndo pharmacy nikannue Sanitizer!
 
Hali ni mbaya sana na wana haki
Atakaepata corona atalipiwa mortgage miezi mitatu
Nafikiri hali itakuwa mbaya zaidi miezi ijayo kama hali itaendelea kuwa hivi
Tupeane moyo tu Mkuu hakuna lingine


Sent from my iPhone using Tapatalk
Are U in the US mkuu?
 
Back
Top Bottom