CoronaVirus: Vipimo vya mara ya pili ya RC Mghwira vyaonesha hana maambukizi ya COVID19

CoronaVirus: Vipimo vya mara ya pili ya RC Mghwira vyaonesha hana maambukizi ya COVID19

Taarifa zinaeleza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Anna Mghwira amepona ugonjwa wa #COVID19 aliothibitika kuwa nao mnamo Aprili 29, 2020

Imeelezwa kuwa majibu ya vipimo vya mara ya pili alivyofanyiwa Dkt. Mghwira yanaonesha hana maambukizi ya ugonjwa huo (negetive)
Alishakua hana hata kabla hajapima wanazingua tu!
 
Maabara si inapima vitu fake, kamati report yake ya uchunguzi ilikabidhiwa lini?


Active Mind
 
Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Tusitishane Bure Tuchape Kazi
 

Ni ubwege uliopitiliza kuamini mtu akwambie anatangeneza product fulani kwa kutumia kitu fulani, halafu aiuze product hiyohiyo ambayo ametumia akili kufikiria, ametumia fedha na muda kuzalisha.

labda hilo.jani ni moja ya items zilizo changanyiwa kwny dawa yao, lakn main iterm inayofanya wanacho kidai kama kweli inatibu, hawawezi kukisema.
 
Habari watanzania wote, upendo na amani vitawale.

Usiku saa 2, taarifa ya habari ya Azam TV, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kasema yeye alikuwa na maambukizi ya Corona baada ya kupima, na alianza kutumia majani ya mmea ambao ni ule wa Madagascar wanautumia, alikuwa anatafuna na akataja jina lake kwa kichanga unavyoitwa, na akasema ni mchungu, na hiyo mimea iko mingi Moshi, na akapima mara nyingine amekutwa negative, yaani hana maambukizi, nimepata matumaini sana sana kusikia hilo. Yaani furaha imenijaa.

Ningeomba serikali yangu sikivu, ifuatilie kwa ukaribu sana mmea huo tena kwa speed kubwa sana, Mungu tusaidie. Mama Anna atusaidie tuujue vema huo mmea.

Mungu mbariki Mh. Rais wetu, John Pombe Magufuli, Mungu ibariki Tanzania.
Mashine iliyokupima mwanzo unaonyesha uko covid 19 positive ilikuwa unasoma kwa makosa kwa mujibu wa Mh Rais, kwa maana hiyo vipimo vikiwa positive means negative.
Kwa Sasa mashine bado haijafanyiwa marekebisho hivyo Basi Kama umepima Tena ikaonyesha negative means positive. Nashauri subiri upime Tena mashine ikishafanyiwa marekebisho ili upate majibu sahihi
 
Tuache kubeza, kapona, tunamshukuru Mungu, katuambia kapona kwa jani hilo, basi na wengine watumie.
Dhihaka nyingiiiii zisizo na tija za kazi gani
 
Back
Top Bottom