Unawachukia wasukuma?! Na wengine wakichukia kabila lako wewe na watu wake itakuwaje?! Epuka migogoro ya dini na ukabila...ni hatari Sana...Kuna nchi na jamii zimesambaratika kwa mambo hayo...TZ tuna bahati hatuna migogoro ya dini na ukabila inayojitokeza wazi...hata wakati wa Mwalimu Nyerere wako wachache waliokuwa wakisema upenyoni watu wa mkoa wa Mara wanapendelews...
Wapi nimesema nachukia Wasukuma?! Nimesema nachukia Wasukuma au nimesema "
wanaokera zaidi ni wale walioapa kutetea kila kitu kwa sababu tu Rais ni Msukuma mwenzao"!! Na hapa KATU siwezi kuwa mnafiki... NAWACHUKIA SANA WATU WANAOTETEA WANASIASA KWA SABABU TU WANAWATETEA WATU WA MAKABILA YAO!!
Na kama nawe unamtetea Magufuli na serikali yake kwa kila jambo kwa sababu tu nyote ni Wasukuma, then SHAME ON YOU!!
Btw, unataka kujifanya umesahau hata vipeperushi na ujumbe wa sauti ambavyo vilisambazwa na Gwajima, ambao
Channel 10 wanahabarisha:-
Sambamba na kipeperushi hicho, askofu Gwajima pia ametoa ujumbe wa sauti unaompongeza Mhe. Rais na kuhamasisha wasukuma kurejesha utamaduni wao wa zamani wa kutumia lugha yao, kusaidiana katika shida na raha na kuwataka wasukuma kuunda vikundi kwenye mitandao ya kijamii vya watu elfu mbili (2000) kwa lengo la kufuatilia watu wanaomtukana Rais na kuwashughulia.
Habari kama hiyo pia iliandikwa na
Nipashe kwamba:-
Katika taarifa yake hiyo, Kamanda Wambura alisema Askofu Gwajima pia ametoa ujumbe wa sauti wenye ujumbe wa kumpongeza Rais na kuhamasisha Wasukuma kurejesha utamaduni wao wa zamani wa kutumia lugha yao, kusaidiana katika shida na raha na kuwataka waunde vikundi kwenye mitandao ya kijamii vya watu 2,000 kwa lengo la kufuatilia watu wanaomtukana Rais na kuwashughulikia.
Sasa mimi na huyo Msukuma Gwajima sijui ni nani anayechochea ukabila!
Na ukweli wenyewe ndo huo... hata hapa JF wapo wengi tu wanaounga kila kauli ya Rais na yale kutoka serikalini sio kwa sababu wote hao ni wana-CCM ambao siwezi kuwalaumu sana, au kwa sababu wanakubaliana nae kwa yote hayo, bali wanafanya hivyo kwa sababu tu Rais ni Msukuma mwenzao, PERIOD!!
but coming to the point ya Corona hakuna anayebisha kuhusu hatari ya Corona...ila baadhi yet hatpendi exaggerations na lawama zisizo na maana..watu wamekaa mkao wa kulaumu tu mamlaka Kila kukicha...yaani watu wamekaa kuangalia makosa tu..halafu hata uzalendo haupo kabisa..eti watu wanaisifu Kenya sijui Mara Rwand na kadhalika...na Wala hawajui kinachoendelea huko Rwanda, Kenya na kwingineko kuhusu maoni ya raia wa huko..Relatively Tanzania we are doing better katika vita hivi ila Tatizo ni mzaha wetu sisi wanachi...katika mitaa mingi ya Dar watu wanafanya mzaha kwa kutozingatia maslekezo..ingewekwa lockdown hapa Nina hakika malalamiko yangekuwa ya kutisha...
You're very fuuny!!
Kuna ndugu yangu mmoja hapa, moja ya vichwa adimu sana hapa JF kwa jina
Kataskopos anafahamu kwamba huwa najitambulisha kama "Beberu" na pia kama "Kibaraka wa Mabeberu"... si ndivyo mnavyotuita sie wakosoaji!!
Kama ndugu yangu huyu anakumbuka, niliwahi kumwambia kwamba hakuna Jukwaa ambalo nakosa ujasiri wa kuchangia kama Jukwaa la Kenya... WHY?!
Kule yakiandikwa maovu kuhusu Tanzania, na kama naamini kabisa haya ni maovu ya serikali, ki ukweli nakosa kabisa nguvu ya kuchangia kwa sababu naona ni kama "washing my own dirty linen in public"!!
Wakati mwingine huwa natamani mada iondolewe kule Jukwaa la Kigeni na kuletwa kwenye local forums ili niwatandike vizuri... matokeo yake naishia kuwa msomaji na kuondoka, huku wakati mwingine nikiwachana Wakenya wakati najua kabisa kwamba wanachosema ni sahihi!!!
Hata hivyo, nitakuwa mjinga sana, tena mjinga niliyepitiliza eti niache kusema ukweli kwamba Magufuli na serikali yake wamefanya mambo ya hovyo kabisa ku-handle issue ya coronavirus ukilinganisha na majirani zetu, hususani Uganda na Rwanda!!!
Na sio nitakuwa mjinga bali nitakuwa mpumbavu nikisema Rais Magufuli na serikali yake wamefanya "a great job" ku-handle issue ya corona ukilinganisha na majirani zetu!!
Na nitakuwa mnafiki nisipopongeza jitihada za Uganda na Rwanda ambao hadi leo hakuna confirmed death! Nitakuwa mtu wa ajabu nisipopongeza juhudi za Kenya na Uganda ambao kila moja wamefanya testing kwa watu zaidi ya 15K huku Rwanda ikiwa imefanya zaidi ya 7K... Tanzania?!
Na kama kuna kipindi ambacho nimechangia sana kule Kenyan & International Forums against ALL GOVERNMENTS duniani and their leaders (Including Magufuli) zilizoleta mzaha kwenye issue ya coronavirus, basi msimu huu ndo nimechangia sana, na nitaendelea kuchangia!!
Isitoshe, hata nyie wenyewe wala sio kwamba ni Wazalendo kwa maana wala allegiance yenu haipo kwa taifa/nchi bali ni watiifu kwa watu na serikali!!!
Serikali na taifa, ni vitu viwili tofauti na mzalendo wa kweli ni yule asiyeona taabu kuikosa serikali ikiwa anaamini serikali inafanya mambo yanayoweza kuligharimu taifa!!
Kwamba, hatujui kinachoendelea huko tunakosifia, wewe tueleze basi manake niliwahi kuwapa changamoto mtaje ni kipi kinachooendelea huko unachoweza kulinganisha na maisha ya watu!
Ingawaje sikuwa mfuasi wa lockdown lakini niliwahi kuwapa changamoto mnitajie ni wangapi wamekufa huko Rwanda, Uganda na Kenya kutokana na njaa iliyosababishwa na lockdown... hakuna hata mmoja aliyetoa hilo jibu zaidi ya kuishia kusema "Hamjui kinachoendelea huko!"