COVID-19: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atangaza ongezeko la Wagonjwa Wapya 196. Visa vyafikia 480

COVID-19: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atangaza ongezeko la Wagonjwa Wapya 196. Visa vyafikia 480

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ametangaza Ongezeko la Wagonjwa Wapya wa Corona Nchini 196. Tanzania Bara Wagonjwa 174 na Zanzibar 22. Amesema kuwa visa vya maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Tanzania vimeongezeka na kufikia 480.
Mimi nilidhani ni idadi ya vifo kumbe maambukizi jamani viongozi wangu huu ungonjwa kama taarifa zinatolewa kiufadhaa hali tuliyonayo isingekuwa hivi tangu tarehe 22 mpaka Leo vijana na watu wazima na watoto hawachuwi taathari hata kidogo watu hawanawi tena mikono hawavai barakoa ndoo moja ya Maji kutwa mzima hapa Dukani kwangu haiishi
 
Shida kubwa sana kwa Tanzania ni kuwa tuna kiburi. Tunadhani kuwa tupo sahihi kuliko wenzetu huko duniani.

Nasikitika tumejiangamiza wenyewe kwa kutokufuata taratibu! Oneni aibu hii! Tunakuwa wageni wa nani kwa ujuaji wetu huu! Tutamlaumu nani? Tutaomba wapi msaada kwa upuuzi wetu?

Mimi wewe na yule kesho hatuijui kutokana na kujiona wajuaji!
 
Papaa Mobimba,
Hii ni serikali ya hovyo kuwahi kutokea. Inawaza kuchakachua tu. Haijalishi ni matoleo ya uchaguzi, taarifa za corona nk. Kama ilivyokuwa kwa uchunguzi wa serikali za mitaa, ndivyo itakavyokuwa uchaguzi mkuu mwaka huu dalili zimeshaanza kujionyesha
 
Back
Top Bottom