COVID-19: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atangaza ongezeko la Wagonjwa Wapya 196. Visa vyafikia 480

COVID-19: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atangaza ongezeko la Wagonjwa Wapya 196. Visa vyafikia 480

Nimeona mahala hapa hapa JamiiForums kuna Uzi umeanzishwa ukimnukuu Mmoja wa Wataalam Wizara ya Afya Dokta Tumaini Haonga akijimwambafai kuwa kwa sasa hawatangazi tena Idadi ya Waathirika wa COVID-19 kwakuwa hakuna Cases mpya na kwamba wengi wanapona na wamepona. Je, hii taarifa ya sasa ya Premier Majaliwa inatoa au inatoa Ujumbe gani Kwetu Watanzania hasa juu ya Serikali na Udhibiti wa hili Janga baya lililoko sasa Duniani? Tumuamini nani hasa kati yao?
Huyu hapa afisa Programu na Mmoja waJumbe na Wataalam wa Jopo Maalum la kupambana na Covid-19 toka Wizara ya Afya Dokta Tumaini Haonga akihojiwa :
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ametangaza Ongezeko la Wagonjwa Wapya wa Corona Nchini 196. Tanzania Bara Wagonjwa 174 na Zanzibar 22. Amesema kuwa visa vya maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Tanzania vimeongezeka na kufikia 480.

Waziri Mkuu akinukuliwa, amesema...

''Kuanzia Aprili 23 - Aprili 28,2020 tumepata wagonjwa wapya wa Corona 196 ambapo kati ya hawa Bara wapo 174 na Zanzibar 22 ambao Waziri wa Afya Zanzibar ameshawatangaza, hii inafanya jumla ya visa vya Corona Tanzania kufikia 480 kutoka 284 ambavyo vilitangazwa Aprili 22''
Vifo?
 
MATAGA wanasema hiyo ni ndogo sana ukilinganisha na watanzania milioni 55, wanasema tuchape kazi ili serikali ipate kodi.
... kwa kipindi hicho cha Aprili 23 - 28; ni wastani wa maambukizi 40 kila siku kwa waliopimwa; wasiopimwa ni wengi zaidi! Duuh! Siku nyingine 5 zijazo tutafikia 100 kwa siku and so on! Wakuu hii kitu ni hatari kuliko inavyochukuliwa! Tunaelekea uelekeo wa Italy na Spain hivi hivi tukiona!
 
Asante kwa updates. Ila vifo mmeamua kumute. Wamepona wangapi ?We need information kamilifu. Mmepima wangapi,wagonjwa wangapi,vifo and waliopona. Tunataka full package.
 
Huyu Mchungaji Gwajima akijitokeza kwa nguvu zooote akawa anasema kuwa nchi za jirani wamekataza waumi kwenda kanisani Lakini wanapigwa na CORONA Wakati Tanzania hawajakatazwa kanisani wanaenda Lakini Hakuna maaambukizi akakazia juuu ya Kenya na Rwanda kuwa kanisani hawaendi na kupigwa wanapigwa wanapigwa Sana na hata robo ya maambukizi hatujawafikia

Sasa ninakuhitaji huku gwajima utoleee ufafanuzi, inawezekana nyie wachungaji wa kirokole ndio mmemzunguka huyu kiongozi na kumdanganya had hali imefika huku

Kwa taarifa iliyotolewa Leo na waziri Mkuu inaonesha kuwa tumeipita mbali Kenya na tuko juuu Sana kimataifa Yote ya Africa tuko top ten na Africa mashariki tunaongoza ebu njooo utoleee ufafanuzi gwajima umetuletea mkosi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom