COVID-19: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atangaza ongezeko la Wagonjwa Wapya 196. Visa vyafikia 480

COVID-19: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atangaza ongezeko la Wagonjwa Wapya 196. Visa vyafikia 480

sikiliza BBC swahili ya jana usiku wamemaliza kila kitu
Hao BBC ndio wanao pima hao wagonjwa hapa nchini mkuu au na wao ni moja kati ya wataalam wa afya hapa nchini kwetu hadi wawe na hizo data sahihi?
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ametangaza Ongezeko la Wagonjwa Wapya wa Corona Nchini 196. Tanzania Bara Wagonjwa 174 na Zanzibar 22. Amesema kuwa visa vya maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Tanzania vimeongezeka na kufikia 480.

Vifo vingine 6 vya wagonjwa COVID-19 vimeongezeka na kufanya jumla ya vifo kufikia 16 Tanzania, wagonjwa waliopona wamefikia 167. “uzushi wa kwamba kila kifo ni cha corona sio sahihi kuna magonjwa mengine yanayoua”

Waziri Mkuu akinukuliwa, amesema...

''Kuanzia Aprili 23 - Aprili 28,2020 tumepata wagonjwa wapya wa Corona 196 ambapo kati ya hawa Bara wapo 174 na Zanzibar 22 ambao Waziri wa Afya Zanzibar ameshawatangaza, hii inafanya jumla ya visa vya Corona Tanzania kufikia 480 kutoka 284 ambavyo vilitangazwa Aprili 22''

Kea hiyo walisubiri mpaka BBC watangaze jana kwamba takwimu hazitolewi ndio watoke mafichoni? This is non sense.
 
Idadi ya waliokufa hakuna.
Bado hatujaambiwa waliopona (kama mkuu alivyosisitiza)

Bado hatuambiwi jumla ya watu waliofanyiwa vipimo.
Na je vipimo ni kwa mtu mwenye dalili peke yake?
Hatua nzur kwa kuujuza umma taarifa hizi
Tuliopo hapa inaelekea laki tano, Tupia majina 20 Tu yaliyowazi Kwa Maana ya wahisika wenyewe wametangulia Mbele za haki Kwa ugonjwa wa Corona, kama hakuna nyamaza, Maana yake unataka wafe wengine Tu, mnaoandika kudai waongezeke wafu na wagonjwa nyie mnaahadi nyingine siyo? Nyinyi hamguswi na Corona siyo? Ona aibu basi mkuu
 
Bora walivyoshinikizwa kutangaza. Well, takwimu zaweza kuwa sio sahihi 100% lakini walau unawapa watu tahadhari kuwa hatupo salama.
 
Hao BBC ndio wanao pima hao wagonjwa hapa nchini mkuu au na wao ni moja kati ya wataalam wa afya hapa nchini kwetu hadi wawe na hizo data sahihi?
pamoja na utetezi, nieshapoteza uaminifu kwa serikali na sitoweza kuiamini tena katika hili janga
 
Kutokana na babu yetu Zinjanthropus kuwa wa asili ya Afrika mashariki basi kuna miongoni mwetu bado hatuja evolve vya kutosha

Huwezi wewe leo umepewa dhamana ya uraisi halafu janga kama hili unachukua likizo na wala huifupishi

picresized_1353113519_7283200914_69d9a02761_b-1.jpg

Asante mzee Zinjanthropus tutaendelea kukukumbuka
 
Kuna uwezekano hizi data zimechakachuliwa...

Chukua figure yao then zidisha kwa factor ya 1.40 ili kupata data kamili...

480*1.4 = 672.

Kwangu mimi hili ndilo jibu sahihi.
Nini kimekusuma kuja na hitimisho hilo?
 
Mimi nilidhani ni idadi ya vifo kumbe maambukizi jamani viongozi wangu huu ungonjwa kama taarifa zinatolewa kiufadhaa hali tuliyonayo isingekuwa hivi tangu tarehe 22 mpaka Leo vijana na watu wazima na watoto hawachuwi taathari hata kidogo watu hawanawi tena mikono hawavai barakoa ndoo moja ya Maji kutwa mzima hapa Dukani kwangu haiishi
Mimi hapa ofisini kwangu kuna mteja kaja akagoma kunawa mikono nakusema korona imeshaisha Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom