Crown vs Brevis

Crown vs Brevis

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Mkuu kwa nchi za Tropiki kwenye joto jingi naona Kama 20W-50 SI mbaya Kama inavyoenezwa
Samahani....unadhani joto la nje hata kama lipo nyuzi 50, je linaweza likazidi joto la engine wakti inafanya kazi ya kupanda milima....??[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Samahani....unadhani joto la nje hata kama lipo nyuzi 50, je linaweza likazidi joto la engine wakti inafanya kazi ya kuoanda milima....??[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
Mkuu mm nime-google tu nikakutana hiyo pweinti usinipopoe mawe
 
Mkuu kwa hesabu zako hizi cc 2000+ utegemee monthly revenue ya 800k? Labda unakaa mwenge ofice mikocheni vinginevyo utapaki gari sana tu!
Mkuu hapo nilimaanisha income ya mwezi mzima, utoe matumizi yote ya msingi..kwa mfano

*kodi ya nyumba kwa waliopangisha.
*umeme
*maji
*matumizi ya chakula cha mwezi mzima kwa familia.
*mahitji ya watoto shuleni mwezi mzima
*mahitaji ya mke
*dharura..

Ukisha toa hayo mahitaji, angalau ubakiwe na 800k ambayo inaelea hewani...hii labda ndiyo uitumie kwa mafuta ya hizo engine zinazozidi cc 2000 ndiyo utafurahia gari
 
Mkuu kwa nchi za Tropiki kwenye joto jingi naona Kama 20W-50 SI mbaya Kama inavyoenezwa
Unategemea na gari utaitumia wapi , ukikaaa makambako huko Kuna Siku unaamka temp no minus celcius , 20w -50 itaumiza engine yako, Ila kwa altitude za dar na pwani inaweza isikuletee shida
 
Inategemea unaishi vipi na unalipwaje Ila Kwenye Magari inapendeza Sana kama unapata vijisent nje ya mshahara hapo utafurah Zaid pia usiache kumiliki gari eti kwavile unalipwa pesa kidogo...
Hii inaweza kuwa ngumu kuapply, umesema vizuri sana kwamba si sahihi kutumia hela ya mshahara kununua mafuta ya gari, kwa sababu itakuwa sawa na kwamba unamrudishia hela huyo aliyekulipa mshahara ufanye kazi yake, hii ni kweli, lakini unaposema tena tusiache kumiliki gari kwa sababu ya kulipwa mshahara kidogo.

Nadhani hii inakuwa mchanganyiko, ni waajiri wachache sana waliostaarabika wanaolipa hela ya usafiri out of mshahara kwa wafanyikazi wao, wengine wengi wanakulipa mshahara tu, sasa kutoa hela ya mafuta kwenye mshahara ni jambo baya kabisa,

mimi nadhani magari tuwaachie wenye nafasi zao, wale wenye vipato vikubwa na marupurupu, ni mbaya sana kuweka mafuta ya vibaba halafu na wewe unaingia mjini na gari yako, yaani huwezi hata kuwasha AC kwa kuhofia kuishiwa mafuta na ni mbaya saana kuzimikiwa gari njiani kwa kuishiwa mafuta
 
Hii inaweza kuwa ngumu kuapply, umesema vizuri sana kwamba si sahihi kutumia hela ya mshahara kununua mafuta ya gari, kwa sababu itakuwa sawa na kwamba unamrudishia hela huyo aliyekulipa mshahara ufanye kazi yake, hii ni kweli, lakini unaposema tena tusiache kumiliki gari kwa sababu ya kulipwa mshahara kidogo, nadhani hii inakuwa mchanganyiko, ni waajiri wachache sana waliostaarabika wanaolipa hela ya usafiri out of mshahara kwa wafanyikazi wao...
Umeongea vizuri lakini hapo mwisho, kwa nini mtu ukubali gari likuzimikie mafuta barabarani...? Huo ni ujinga uliopitiliza...

Wakati mtu anawasha gari lake nyumbani,si anaona gauge inasoma vipi?

Wale wanaoendesha magari kwa ajili ya show off ndiyo wanaodhalilika....hataki kukubaliana na hali kuwa gari halina mafuta, na mfukoni hana hata buku 2..

Gari kama halina mafuta ya kwenda na kurudi safari uliyoipanga, liache nyumbani panda daladala..
 
Mkuu hapo nilimaanisha income ya mwezi mzima, utoe matumizi yote ya msingi..kwa mfano

*kodi ya nyumba kwa waliopangisha...

Simply, kipato kinapaswa kuanzia 1M plus kwa mwezi ili uweze kumudu gari yenye 2000 cc?

Unaweza ukawa sahihi au sio sahihi, Mie natumia 200k kwemye mafuta kwenye gari langu kwa mwezi na Income yangu sio kubwa sana ila ni kama 870k per month ukitoa Bills nabakiwagwa kama 600k.

Nikitoa 200k ya mafuta nabakizaga 400k alfu hapo natoa 200k inaenda saving so inategemea matumizi yako yakoje kiujumla ila kama hna matumizi rough hata uwe una salary ambayo ni 2M per month ila haitatosha
 
Back
Top Bottom