Crown vs Brevis

Crown vs Brevis

Kumbe yapo vizuri

Sent
Mkuu,

Muwamba ngoma siku zote huvutia kwake.

Na ukitaka uujue utamu wa ngoma, ingia uicheze.

Hakuna mtanzania atakayekuambia gari lake linakula mafuta mengi...daima aatalipigia kifua.

Gari siyo piki piki...Ukimuona mtu yupo mjini na Vitz kila siku, mpe heshima yake.

Watu wengi wanaokaa huko kwenye injini zinazozidi cc 2000 wanaumia maumivu makali sana ya mafuta, sema tu kila mtu anajua siri yake

Haya magari yenye injini kubwa kweli ni mazuri sana ila ili uyafurahie hakikisha uchumi wako kwa mwezi si chini ya 800,000 unayobakiwa nayo ukiwa umeshalipa pango, umeme, maji, mahitaji ya mwezi mzima ya familia na tahadhari pembeni.
 
Mkuu kwa Toyota hizo injini Power haipimwi kwa code au herufi.

Ngoja nikupe mfano kwenye injini za Petrol kuna code ya A, E, F, Y, M, J na S. Mfano kwenye A kuna 5A na 7A hizi zimetumika kwenye Corolla, Carina,Sprinter na ni 4-cylinder hazina turbo. Nyingine ni 3s, 5s, 3F, 2Y, 3Y

Injini za Toyota za 6-cylinder ni 1JZ,1G na 1M, 2M...
Ahsante chief kwa elimu nzuri
 
Mm natumia Crown huu ni mwaka wa tatu. Sipo hapa kupiga porojo
Sijasema unapiga porojo Kaka,but I assure you Crown non hybrid haiwezi kuwa na fuel efficiency ambayo ni the same to Carina believe me!

Crown ingekuwa na efficiency hiyo watu wangefanyia Uber😂😂😂-Sababu ina comfortability kubwa-why on earth can someone buy Carina or Ist and not Crown while they are having the same fuel efficiency with crown having more luxury features and power?Just a simple logical question I am trying to ask my self
 
Sijasema unapiga porojo Kaka,but I assure you Crown non hybrid haiwezi kuwa na fuel efficiency ambayo ni the same to Carina believe me!
Crown ingekuwa na efficiency hiyo watu wangefanyia Uber😂😂😂-Sababu ina comfortability kubwa-why on earth can someone buy Carina or Ist and not Crown while they are having the same fuel efficiency with crown having more luxury features and power?Just a simple logical question I am trying to ask my self
Hawa Jamaa walifanya tafiti kwa watumiaji wa Crown wakapata matokeo haya:-
Average fuel consumption Toyota Crown 2.5i V6 24V (200 Hp) 1999-2017
Consumption:
l/100km mpg(US) mpg(UK)
Urban 20.1 l/100km N/A
Combined 14.8 l/100km N/A
Сountryside 12.3 l/100km N/A
 
Hawa Jamaa walifanya tafiti kwa watumiaji wa Crown wakapata matokeo haya:-
Average fuel consumption Toyota Crown 2.5i V6 24V (200 Hp) 1999-2017...
Na Jambo la kuzingatia ni kwamba fuel efficiency ya gari jipya ni tofauti na Used car. Kupata fuel efficiency ambayo mjapani ali declare kwa brand new car kwenye the same car lililotumiwa 20yrs later ni nearly impossible!na majority yetu Ss watanzania hatu afford kuyanunua.
 
Before mtu hujanunua gari-tathmini ya kina juu ya matumizi,kipato nk.ni lazima yafanyike pamoja na kujiridhisha kupitia vyanzo mbalimbali vya taarifa juu ya gari husika otherwise tegemea changamoto.

I have a friend of mine Ana jamaa yake alinionyesha anaishi hapo sinza,huyu jamaa alishauriwa Subaru Forester twin turbo ina fuel efficiency kubwa ya up to 12km/liter na yeye Akaingia Kingi;mwenzi tu Chali kachemka na katafuta mti wenye kivuli Ka park kupunguza stress ya Wese! hii ilichangiwa na kutopata taarifa sahihi, hata brevis ukiwa mshamba utabadilishiwa lebo ya pale nyuma badala ya Ai300 unawekewa na mbongo lebo ya Ai250 ukafie mbali 😞😞 na wakikuona wa mndenyi utawekewa mpaka lebo ya 1.8L
 
Nina jamaa yang anafanya mishe mererani huko Mgodini. Yeye anatumia Mark-X na uendeshaji wake ni huo wa hapa na hapo tu yuko 80km/h! RPM zake ndo hizo 1-4 ila mnyama unafunguka hatari yani ukipanda ile gari kama una moyo mwepesi utaomba kushuka. Huwa akitimba mda anaotumia Moshi-Arusha hapo road ni 30mins tu.
Mmmh!
Huyo mtu anaweka roho yake rehani
 
Back
Top Bottom