Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 25,968
- 36,044
Chama cha wananchi CUF kilikuwa ndio chama cha upinzani chenye nguvu zaidi hapa nchini na ilibaki kidogo tu kichukue nchi lakini yalitokea yakutokea hatimaye chama kikafa na kikapotea kabisa , ule mvuto au ushawishi uliokuwa nao kwa wananchi umepotea mazima , ndipo hapo Chadema kikajipenyeza na kuwa cha cha upinzani chenye mvuto na ushawishi mkubwa kwa wananchi.
Nasikitika kuona yanayoendelea nchini , viongozi wa ngazi ya juu wa chadema wenyewe kwa wenyewe hawaelewani na wanazodoana laivu kwa wananchi ni ishara tosha humo chamani hakuna amani tena wala mshikamano na dira ya chama ndio maana walishindwa kuyamaliza ndani ya chama na wakayaleta kwa wananchi kuzodoana na kunyoosheana vidole .
Ila yote haya nadhani mwenda zake kwa namna moja au nyingine amechangia kukididimiza na kukififisha hichi chama , hawa wengine walioingia madarakani ni kama wanakamilisha alichoanzisha mwenda zake.
Na kama na hiki chama kitapotea kwenye ramani , itachukua muda mrefu sana hapa nchini kupata chama cha upinzani chenye nguvu.