Cyprian Majura Musiba ni nani na anatumwa na nani?

Cyprian Majura Musiba ni nani na anatumwa na nani?

Ameitisha press conference na kutaka vikosi vya usalama viwashughulikie bila huruma Mange Lissu,Mbowe,Maria Sarungi,Zitto na wengine WANNE kwa madai ya kuhatarisha usalama wa nchi na kutumiwa na CIA na FBI
Hana kazi anatafuta huruma ya Magu na Bashite
You are not serious! Hivi kila mtu anaweza kuitisha press bila kibali na akaongea lolote bila kuwa na proof na bado dola ikamwacha tu aende zake kwa mkewe?
Yeye yupo hapo mitaa ya ilala na posta anamangamanga kusaka ugali tena wa kuomba kwa kina bashite, amewaona wapi aliowataja wakitumika na vyombo alivyovitaja na kwa lipi hasa hadi vyombo hivyo vitake habari za hapa?
Kwani marekani ina mpango wa kuja kututawala? Hebu vyombo husika vimhoji aseme vizuri ili kama yeye ni nabii titto mwingine tujue!
Au anahamisha goli baada ya Trump kuiwakia tz na china? Mtajichambua kama kitumbua!
 
BAKAYOKO ndio mtu wakwanza aliyepswa kuwa hapo ktk hii list ...na vijana wake.. zero ..DAB .mambo baadae. na defao...maana Hawa ndio wanaohusika na upoteaji wawatu hovyo ..na miili ya watu waliokufa kuokotwa katika fukwe achilia mbali wengine kudiriki kupigwa risasi hadharani na anguko kuu la uchumi lilopo nchini ...


yaani hiyo list ndio hatari kabisaaa kwa usalama wa hili taifa ..
lasivyo mtoa mada atakuwa ametumwa tu
 
Sijaona Tuhuma za Maana Hapo..Na Ajue Adui namba Moja Kwa Taifa hili ni CCM..Mleta Mada Umeuliza Swali..Jibu lake ni rahisi..Katumwa na CCM..na ndiyo Maana Anatuhumu Viongozi wa Vyama lakini CCM wote kwa Mtazamo wake ni Malaika..
 
Mkuu hapo #1 tangu lini FBI wakawa shirika la kijasusi? Hii inakupa quality ya uzi mzima kuwa bwana Musiba ni Jogoo toka mashambani kuwika mjini ni kwa nadra sana.
Anaweza akawa na wazo zuri nyuma ya pazia ila akawa na poor presentation kutokana na wrong perception ya baadhi ya aliowataja. Pia, kwa kuanika hivi,ndo kaharibu kama ile issue ya madawa ya kulevya. Hii ni issue nyeti na sio ya kuropoka ovyoovyo tuu.
 
Wanaomfahamu, hivi huyo Musiba ni mtu mwenye akili timamu au ndiyo wale walio katikati ya watu wazima na wendawazimu?
 
Kama wasiojulikana hawapo basi hamna bandiko hapo
 
Kwani huyu Musiba ni nani vile..........halaf mbona kama kuna watu wanapanick mapema hivi kweli Mbowe ni mtu Hatari?Tundu lissu aliyepigwa ni hatari? sasa waliompiga je? Chama kinachoshambuliwa na silaha ndo hatari......ama kweli.....lakini muda huu ulikuwa ni wa kukaa kimya kutafakari na kujiongeza na si muda wa kugeuza cheusi chekundu nakuongea vitu vya ajabu.....la sivyo watu wana akili sana kuliko baadhi wanavyodhani
 
Nimelazimika kuangalia hii video.

Kwanza nimecheka sana. Siwezi kumbishia Bwana Msiba maana anaweza kua na sababu zake hata kama ni za kipumbavu ila bado anaziamini kua ni sababu.

Nilichogundua elimu ndogo na uelewa mdogo bado ni changamoto katika jamii yetu, kama huyu alikua mtangazaji na mwandishi wa ha ari basi hii nchi ina matatizo makubwa.

Kwanza Musiba anaonekana hajui au hana ufaham kabisa tofauti kati ya FBI na CIA. Anaituhumu FBI lakini kimantini ni CIA kama kweli anachokisema kiko hivyo, FBI haifanyi kazi za ujasusi na haivuki mipaka ya Marekani, hawa ni polisi wa Marekani na sio taasisi ya kijajusi nje ya Marekani.

Pili, Musiba hata maneno ya kawaida tu yanamshida kuyasarufisha, Uasi yeye anasema ni Uhasi.

Little learning is very hazardous. Stupidity is still common among Tanzanias.
 
Back
Top Bottom