kingabdiel
Member
- Mar 7, 2008
- 31
- 2
Unapata wapi nguvu ya kuutangazia umma wa Watanzania kwamba hawa ndugu zetu ni hatari??? Mamlaka unayatoa wapi Musiba???
Maana ya mtu hatari katika usalama wa taifa ni wewe wa kutoa hiyo hukumu na maamuzi ya kuwaita wenzetu Hatari???
Naombeni msaada ni nani huyu? Anapata wapi mamlaka na nani amemtuma?
Samahani JF niliiacha hii habari hewani bila kuiimarisha kwasababu huyu jamaa alinichefua sana, nasema ukweli nilifika hatua ya kufikiria kuukana utaifa wangu wa Tanzania. Polisi wanamuacha huyu? Vyombo vya habari mnaripoti mtu kama huyu really na mnaona ni taarifa ya kawaida tu....???
View attachment 701577
Nafikiri ni wakati wa kutilia maanani hizo tuhuma,kwani ni mbinu na biashara ya wakoloni mambo leo kudhoofisha nchi nyingine kwa kutumia watu wenyewe wa nchi hizo. HOJA ZIJIBIWE KWA HOJA tusitoe mashambulizi binafsi. Wahenga walisema " lisemwalo lipo kama halipo basi laja" tukumbuke" Ignore the messenger but receive the message"
Mhe Zito anataka kutuaminisha kuwa mtoto wa waziri wa ulinzi hawezi Kufanya makosa ?, ni hoja duni sana .kwani nafikiri kuwa kama motto wa kiongozi hafanyi makosa ,kiongozi mwenyewe anafanya ? Anataka kutuaminisha nini? Anajijengea ukuta kuwa kuna watu Fulani hawakosei, kwanini?
Mfano,
Kipindi cha uchaguzi mkuu 2015 kuna mtia nia mmoja wa uraisi wa chama Fulani alinuuliwa akisema…Yeye anafaa kuwa raisi wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu WAMAREKANI WANAMTAKA YEYE” na huyo alikuwa ni Waziri.