Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

Whatever you call it. Makonda hawakuwahi kaa hata kituo cha polisi. Acha kulala.

Nani kamuongelea Makonda. Mbowe kaanza kuhangaika leo? Kila kitu lazima mumuingize Mbowe sijui kwa Nini. Makonda tangu apigwe Chini ubunge Hakuna mtu mwenye time naye maana watu waliridhika kakosa vyote.
 
Sasa hivi ata nauli ya kwenda Kwao Tarime Kusalimia hana. Da kweli Heshimu watu Sponsa Ufariki😭

Kwa haraka haraka jamaa Hana hata Mia, ndio maana anaomba mchango kutoka kwa wasamaria wema.
 
Membe kaenda kukazia hukumu bado shangazi..

Je wale jamaa wa changia Musiba waliishia wapi?

Walipata bei gani? Zilienda wapi?
deni alifungi mtu watakamata mali zake ambazo hana kitu, 😁😁😁😁😁😁
 
Potelea pote , atimue mbio tu , naye Membe ni binadamu anaweza kumsamehe akiona mpaka ameamua kukimbia .

Ila namuonea huruma huyu bwana maana hata asipolipa simuoni kuishi kwa amani maana vitisho nje nje .

Yeye angebaki kuwasema akina Lissu, Mbowe, Zitto na Maalim hao ni wavumilivu, ila akaenda kumgusa kachero mbobezi, hapo ndipo alipokosea.
 
Mahakama Kuu ya Tanzania imempa siku 14 za kazi mmiliki wa Gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba na wenzake watatu kumlipa Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu, Benard Membe TZS bilioni 9.92 kama fidia ya kumchafua kupitia vyombo vya habari.

View attachment 2588944

Mahakama imetahadharisha deni hilo lilipwe ndani ya muda vinginevyo hatua zaidi zitachukuliwa.
Huyu chawa bado yupo?
 
Ukikosa Mali, wanakuweka kizuizini kwa gharama za mdai mpaka ulipe hicho kiasi.
uwezo wa musiba kulipa ni elfu 20000 kila mwezi , na atatekeleza hilo kikamilifu tuone kama atawekwa kizuizini
 
Watachukua Mali zake zote na kupingwa mnada na Madalali wa mahakama, Kama kiasi hakitoshi Basi, atatawekwa kizuizini mpaka pesa yote ilipwe. Nadhani Membe shida yake sio hiyo pesa bali anahitaji jamaa akae ndani hata Mwezi mmoja.
Nimeona barua yono inasambaa after hizo siku kazi anayo
 
Back
Top Bottom