Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

WAKILI MSOMI AFAFANUA : HUKUMU HII YA MADAI ITAMZONGA MWANAHARAKATI HURU CYPRIAN MUSIBA KWA MIAKA 12



Mwanasheria msomi wakili Emmanuel Augustino anasema Je sheria inasemaje ikiwa mwanaharakati huru Cyprian Majura Musiba akishindwa kulipa kufuatia hukumu ya Mahakama Kuu

Inawezekana Cyprian Majura Musiba hana hela , hilo halijalishi anatufahamisha mwanasheria msomi.

Hukumu hii ya Mahakama Kuu inaishi miaka 12 hivyo hata kama leo mwaka 2023, Cypria Musiba hana hiyo fedha basi Bernard Carmillus Membe anaweza kusubiria siku Musiba akiibuka kiutajiri ndani ya miaka yote 12 tangu hukumu kukaziwa .

Hivyo deni hilo Cyprian Musiba alilowajibishwa nalo kupitia hukumu hii atakuwa anatembea nayo shingoni hadi atekeleze wajibu wa kulipa fidia kama madai (decree) ya Mahakama Kuu ilivyoamuru .

Namna nyingine ni kumfunga mdaiwa Cyprian Majura Musiba kama mfungwa wa kimadai ambapo Benard Membe pia inawezekana ....

Mwanasheria msomi anaturejesha katika mfano wa hukumu ya kesi ya madai ktk mahakama ya biashara namba 80 / 2006 aliyoamua jaji F. Werema kuhusu kesi ya madai ya Euro Africa Bank (T) Ltd dhidi ya Wolfgang, Christine Springer & wenzake walipe deni .... sasa kabla ya miaka 12 kuisha mwaka 2018 wadai walirudi mahakamani mbele ya Jaji Mruma, madai ya Euro Africa Bank Tanzania Ltd yaliwasilishwa tena ..... na Euro Africa Bank Tanzania Ltd wakapewa invoice ya gharama za matunzo gerezani watoe shs. 300,000 kila mwezi kwa magereza ili mdaiwa aweze kutunzwa gerezani ..

Hivyo kwa Cyprian Majura Musiba anaweza kuwekwa gerezani kama mfungwa wa kimadai huku akilipiwa gharama za gerezani na Bernard Membe baada ya Mahakama kusikiliza utetezi wa Cyprian Majura Musiba kuwa hana uwezo wa kulipa madai ....

Mfungwa wa madai ikitokea kwa Cyprian Musiba ni tofauti na mfungwa wa jinai gerezani hivyo hatatumikishwa kazi za wafungwa wa jinai kama kazi za kulimishwa mashamba, kupasua mawe n.k ....
 
Musiba asipotuaga kwa pressure ataishia kuwa chizi, siku hizi nikiitazama ile sura yake namuona hayuko na amani, moyo wake mzito.

Angefanya atleast public apology angeweza kusamehewa na wale aliowakosea, ili apate amani, kwani nao ni binadamu pia, kuliko kukaa kwake kimya huku akiteketea ndani kwa ndani.
Yes upo sahihi, naamin angekaa kwa aman na angesamehewa! Tatizo ni hawa walinda legacy humu wanampump!!
 
Nakumbuka Mtikila alitaka kukwepa kumlipa jamaa fulani baada ya mahakama kutoa hukumu. Mahakama ikatoa hukumu tena kama hatamlipa jamaa chini ya masaa 24 akamatwe na afungwe miaka 3 na kulipa. Mtikila alilipa faster siku iyoiyo.
 
Back
Top Bottom