Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

Nakumbuka mtikila alitaka kukwepa kumlipa jamaa flani baada ya mahakama kutoa hukumu. Mahakama ikatoa hukumu tena kama hatamlipa jamaa chini ya masaa 24 akamatwe na afungwe miaka 3 na kulipa. Mtikila alilipa faster siku iyoiyo.
Mamb ya kisheria na amri ya Mahakama ni magum sio ya kufanyia mzaha.
 
KIsheria hukumu ni sawa lakini si haki. Hivi mtu anawezaje kudai ana thamani ya mabilioni wakati hizo hela yeye mwenyewe hana?

Sheria inapaswa kubadiilishwa ili kuondoa,mianya ya kukomoana kwq mgongo wa sheria . Sheria itamke tu kama mtu akitiwa hatiani alazimike kukanusha yale aliyoyasema na pia kulipa gharama za kesi tu.
 
Analindwaje? Acha kudanganyana na wenzio yapelekwe mashtaka mahakamani na ushahidi uwepo siyo maneno maneno tu. Sisi tuliamininishwa Makonda ni mbaya sana. Tunashangaa anadunda tu mtaani.
 
Nani kamuongelea Makonda. Mbowe kaanza kuhangaika leo? Kila kitu lazima mumuingize Mbowe sijui kwa Nini. Makonda tangu apigwe Chini ubunge Hakuna mtu mwenye time naye maana watu waliridhika kakosa vyote.
So adhabu alishapata? 🤣🤣🤣🤣 Kwa style hii kweli ccm itatawala milele na watu hawatakuwa na woga.
 
Mwanaharakati huru Cyprian Majura Musiba yupo katika hali ngumu kwa miaka 12 ijayo kama wazalendo uchwara watashindwa kuanzisha harambee kulipia michango ya fidia ya mabilioni ya shilingi , maana followers / mashabiki wake wote wa majukwaa ya mitandaoni wa 'mute'
 
Kimsingi sijui mahakama ili calculate vipi gharama za mdai mpaka kuja na kiasi hicho walichotaka Musiba alipe..
 

Huwezi kufuta fidia kwenye kesi za madai hasa kuchafuliwa jina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…