Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

Wale jamaa kule alikokuwa anachapisha magazeti yake tena tunasikia ilikuwa bure mbona wamemuacha mtu wao? 😁
 
Hivi una akili kweli wewe???
Unajua maana ya kuchafuliwa?
Wewe unapaswa kuwa kundi moja na Sukuma gang
Kuchafuliwa maana yake ni defamation. Yaani kuvunjiwa heshima yako kwa jamii kwa kumkashifu kwa maneno yasiyo ya kweli au ya matusi. Hivyo huyo aliyekuvunjia heshima unampeleka mahakamani kumdai akulipe fidia (damages). Ni kesi ya madai (civil case) na ni ndogo sana, siyo ya jinai.

Mtu huyo kama akikupiga makofi au ngumi au bakora au risasi, kesi hiyo inakuwa ni kubwa na yakijinai. Adhabu ya kumpiga mtu makofi au bakora haiwezi kufika hata shilingi million moja au kifungo cha kuzidi mwezi mmoja. Sasa iweje umtukane Mwembe au mtu ye yote yule uhukumie shilingi bilioni 9? Hapo lazima kuna dosari kubwa aidha ya hao majaji waliotoa adhabu hiyo au ya sheria zetu tulizozitunga kupitia kwa wabunge wetu. Kuna haja ya kurekebisha sheria hiyo ya adhabu kwa kosa la defamation na kuiwekea kikomo cha juu kisichozidi shilingi million 50! La sivyo inaacha mwanya wa ufisadi: hizo billion 9 nusu yake au zaidi zikagawiwa kwa hao majaji na mawakili walioendesha hiyo kesi. Tuliona mgawo wa mabilioni ya pesa za kesi ya escrow baada ya hiyo hukumu.
 
Point yangu ni kwamba Hakuna usawa wa sheria, ni nadharia tu. Ndio maana umesema mwenyewe huwezi kumlinganisha membe na Rais , kwa maana hiyo kisheria Membe na Rais sio sawa.

Ndio maana Musiba kapigwa bilioni Tisa maana kamchafua Waziri wa mambo ya nje mstaafu, mbunge mstaafu , mfanyabiashara nk.
Sheria tumezitunga wenyewe kupitia wabunge wetu. Ni sisi wenyewe tuliamua kumpa rais upendeleo huo. Tutakapoona unatumika vibaya tunayo madaraka ya kuuondoa kupitia marekebisho ya hiyo sheria au hiko kifungu cha katiba.
Mawaziri pamoja na Membe hawana huo upendeleo wa kisheria wala tusiwaogope kuwasema kwa kuogopa mahakama itatuhukumu kuwalipa makumi ya mabilioni kama ilivyofanya kwa Mwembe. Tukemee hiki kitendo cha mahakama cha billion tisa kama fidia ya matusi aliyotukanwa Mwembe! Kwa mwendo huo kama Membe angekuwa amepigwa makofi au bakora na Msiba nadhani hukumu ingalikuwa kifungo cha maisha.
 
Uko sahihi lakini naomba niongeze kitu hapo, hayo hayo matusi au maneno ya uongo ambayo naweza kutukanwa mimi au wewe ujue fidia yake siyo sawa na kama akitukanwa mtu kama Membe au Rostam
 
Mahakama Kuu ya Tanzania imempa siku 14 za kazi mmiliki wa Gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba na wenzake watatu kumlipa Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu, Benard Membe TZS bilioni 9.92 kama fidia ya kumchafua kupitia vyombo vya habari.

View attachment 2588944

Mahakama imetahadharisha deni hilo lilipwe ndani ya muda vinginevyo hatua zaidi zitachukuliwa.

Hakuna bima ya kiki😂
 
Hi Dunia usipokuwa na akiba ya maneno utahangaika Sana.
Bonge la quote! Binadamu sisi muda mwingi jeuri, kiburi na majivuno ndivyo hutuponza. Tunajisahau kuwa Nguvu au uwezo huzidiana!

HAKUNA AIJUAYE KESHO.
 
Hana shida ya pesa hiyo... anazo nyingi zaidi ya hiyo. Hicho ulichokizungumza ndio lengo lake na jopo lake kina JK
Sidhani Kama Membe yupo serious na hizo pesa , Bali anataka kumfundisha adabu Musiba na kutoa fundisho kwa wengine wenye dharau na uchawa uliopitiliza.
 
Enzi za ufalme wa Kayafa😁😁😁
View attachment 2591169
Thamani ya hayo matusi ndiyo shillingi billioni 9 kwa Mr Membe. Zitto Kabee na January Makamba ambao nao walitukanwa hivyo hivyo, bila shaka nao wataenda kufungua kesi ya namna hiyo hiyo ili nao walipwe hiyo billioni 9 kila mmoja. Jumla zitakuwa billioni 27. Huyo Musiba atauza hadi figo zake zote na bado hatamaliza hilo deni!!

Yaani hiyo hukumu haina weledi wo wote. It's utopia of the highest order. Ndiyo maana wakati mwingine mama hubidi aingilie huu muhimili. Mshahara wa waziri kwa mwaka hauzidi million 48 (after taxes). Kwa miaka 100 ni billion 4.8 na kwa miaka 200 ni billioni 9.6. Sasa kwa mjibu wa mahakama zetu na sheria zetu, ukimtukana waziri, tena waziri mstaafu inabidi umlipe mishahara yake ya miaka mia mbili!!
 
Uko sahihi lakini naomba niongeze kitu hapo, hayo hayo matusi au maneno ya uongo ambayo naweza kutukanwa mimi au wewe ujue fidia yake siyo sawa na kama akitukanwa mtu kama Membe au Rostam
Mimi na wewe tutalipwa sana sana million moja. Kwa nini iwe hivyo wakati mshahara wako au wangu unamzidi huo wa waziri? Why?
 
Sheria hizi siyo kwetu sisi tu, hata sehemu nyingine nyingi pia ni hivyo hivyo. So ni wewe kuiaminisha mahakama kuwa unastahili damage kubwa kwasababu kadhaa na kadhaa then mahakama itapima kama kweli unastahili hiyo fidia ama lah.

Mhhh, hebu tutajie hizo sababu za kweli ambazo mahakama yenye akili timamu utai convice ulipwe fidia kwa kutukanywa TSh 9,000,000,000,000? Sawa na pesa ya kujenga Mloganzila hospìtal au Mkapa Stadium tatu?

Sababu pekee ni kuwa tutagawana hizo pesa sawa kwa sawa.
 
Au Auze Figo na Maini Na Moyo apeleke Hela ya Watu
 
Thamani ya hayo matusi ndiyo shillingi billioni 9 kwa Mr Membe. Zitto Kabee na January Makamba ambao nao walitukanwa hivyo hivyo, bila shaka nao wataenda kufungua kesi ya namna hiyo hiyo ili nao walipwe hiyo billioni 9 kila mmoja. Jumla zitakuwa billioni 27. Huyo Musiba atauza hadi figo zake zote na bado hatamaliza hilo deni!!

Yaani hiyo hukumu haina weledi wo wote. It's utopia of the highest order. Ndiyo maana wakati mwingine mama hubidi aingilie huu muhimili. Mshahara wa waziri kwa mwaka hauzidi million 48 (after taxes). Kwa miaka 100 ni billion 4.8 na kwa miaka 200 ni billioni 9.6. Sasa kwa mjibu wa mahakama zetu na sheria zetu, ukimtukana waziri, tena waziri mstaafu inabidi umlipe mishahara yake ya miaka mia mbili!!

Hukumu Ni Adhabu Hukumu ni Fundisho Kwako Mkosaji na Wengine! Mahakama Iko Sahihi! Atafute Bwana Wapeleke Hela ya Watu
 
Back
Top Bottom