Huyu mama kama alidhamiria..?
amelala yuko tungi, au yuko UswissAsubuhi yote hii unatuambia usiku mwema!
Kweli, inafikirisha Mkuu.View attachment 1390616
Nimejaribu kuwaza na kuchambua jinsi huyu Dada aliyebainika kuwa na virusi vya Corona, nimejiuliza maswali mengi sana.
Baada ya kufuatilia kwa kina nimeambiwa jina lake ni Isabela Mwampamba, umri wake ni miaka 46.
Simulizi ya safari yake ndio jambo kubwa limenifanya niwaze sana na kujiuliza maswali ambayo sisi Watanzania tunapaswa kuwa makini, na kujiridhisha kama gonjwa hili limeingia kwa bahati mbaya ama mpango maalum? Kwenye hili sitanii hata kidogo.
Tunaambiwa huyu Dada aliondoka nchini Machi 3, 2020 kwenda Rwanda. Hatuambiwi alikwenda Rwanda kufanya nini?
Baada ya kukaa Rwanda siku 2 Machi 5, 2020 aliondoka kwenda Brussels Ubelgiji, akiwa huko alikwenda Stockholm Sweden, akiwa huko alifikia nyumba iliyokuwa na mgonjwa wa Corona.
Akaondoka hapo kwenda Norway ambako pia amekaa siku kadhaa hadi Machi 14, 2020 alipoondoka huko kurejea nchini kwa kupitia tena Rwanda na kisha akaingia kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA.
Simulizi ya huyu Dada inasema baada ya hapo hakwenda nyumbani Arusha bali aliamua kwenda kulala hotelini kwa madai alikuwa ameanza kujishtukia.
Akiwa hotelini alijiona hayupo sawa ndipo akaenda Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru ambako baada ya sampuli kupelekwa Dar es Salaam ndipo ikathibitika kuwa ana virusi vya Corona hiyo jana Machi 15, 2020.
Kinachonisumbua mimi, mzunguko wote huu hatuelezwi alikuwa anafanya shughuli gani? Najiuliza hivyo kwa jinsi Ulaya ilivyotikiswa na Corona unawezaje kwenda huko ukaishi kwenye nyumba yenye mgonjwa wa Corona na bado ukarejea nchini kwako ambako umeambiwa ugonjwa haujaingia bila hata kusema hayo yote ili tahadhari ichukuliwe mara baada ya kushuka kwenye ndege?
Ni bahati mbaya kweli au ni mpango maalum ulipangwa ili Tanzania nayo itangazwe duniani kuwa imepatwa na Corona?
Najiuliza hivi, ni bahati mbaya kweli kwamba huyu Dada alianzia safari yake Rwanda?
Najiuliza ni bahati mbaya kweli kwa huyu Dada kwenda kuumwaga upupu Kilimanjaro na Arusha kwenye kiini cha utalii wa nchi yetu?
Hivi ni bahati mbaya kweli mtu atoke safari aende kujipiga quarantine hotelini ambako kuna muingiliano wa watu wengi? Kwa nini hakwenda nyumbani kwake na kuwaambia jamaa zake waondoke au atengewe chumba chake kama ilivyokuwa huko safarini Ulaya alikofikia kukiwa na mgonjwa wa Corona?
Nimejiuliza zaidi kwamba labda kwa kutokuwa na mgonjwa wa Corona kulionewa donge na hivyo ikatengenezwa namna ya kutuweka kundi moja?
Kwa mawazo haya, nakumbuka jambo moja tu, Watanzania tunapaswa kuwa makini kuliko wakati mwingine wowote.
Kwa kuwa ni janga la dunia basi nasi tuungane na dunia kujihadhari na Corona. Tuepuke mikusanyiko isiyo ya lazima, tuepuke kugusana, tuepuke kubusiana, tunawe mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na tutumie viua vijidudu yaani sanitizers.
Kama sio lazima tuache safari hata kutembeleana nyumba kwa nyumba, tukae ndani tutulie. Tuwakinge Wazee na watoto wetu sana kwa sababu hawa ndio wameonekana kupatwa na madhara makubwa ya ugonjwa huu ambayo ni kifo.
Inaelezwa mpaka sasa Corona imesababisha vifo zaidi ya watu 5,000 na watu zaidi ya 150,000 wameugua. Hili ni balaa kubwa, tusichukulie poa hata kidogo.
Lakini pia ukijijua umeambukizwa tafadhari usiambukize wengine, hayo ni mauaji. Nenda Hospitali wataalamu watajua cha kufanya.
Ni hayo tu lakini kwa kweli imeniuma ugonjwa huu kuingia nchini mwetu kwa mtindo huu.
Usiku mwema.
Jotham Mugishagwe Jr.
Ilala, Dar es Salaam.
Machi 15, 2020.
Tuko kwenye the lait traki
Hata waliompima wachunguzwe au vipimo vyenyewe ndo tatizo iweje mtu ambaye yeye mwenyewe amejihisi ni Mgonjwa vipimo visibaini kitu? Au alihonga wapimaji ili akajitenge eneo lenye hadhi aliyotaka yeye? na hawa Rwanda ni Rafiki zetu kweli wa kufa na kuzikakana?Hakika story yake inatia mashaka sana. Mamlaka husika zinapaswa kulichunguza hili kwa umakini zaidi
Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu alienda alikokwenda bwana yuleeHuyo alikuwa anajua, Na alikuwa anafanya Kwa maelekezo, hivyo asingefanya kinyume cha maelekezo, angekuwa mstaarabu angeeleza pale uwanja wa ndege lkn alitaka atomize maelekezo ya Kazi yke.
Huwa wanafanya Kwa maelekezo maana wanakuwa wanalipwa .
Nashangaa mnaosambaza picha za mgonjwa sijui jf ili mnalichukuliaje? Uyu mama ni mfanya bihashara mwaka jana nimekutana naye Sweden akiwa katika arakati zake za kutafuta marafiki ikizingatiwa shule yake nishule ya gharama kubwa ila yeye utoza karo ndogo sehemu kubwa ya karo ulipwa na wafadhili.
Nawashangaa kwanini msipige kelele Waziri mwenye dhamana asiondoke maana alituhakikishia kuwa mipaka yetu iko salama lakini hataki kusema kama hawana vifaa kabisa.
Niwaombe ndugu zangu kwa pamoja tufuate njia wanazotumia wenzetu kukabiliana na ugonjwa huu hatari niwaondoe wasiwasi kuwa dawa za ugonjwa zipo na wengi wanapona kwa dawa hizo ambazo zinapatikana katika maeneo mengi nchini.
Kule ilipoanzia China [emoji630] tayari wameidhibiti kwa kutumia vitunguu swahumu, machungwa, limao na maji ya moto.
Ombi jingine tusiwatishe watu wakafa kwa hofu kabla ya ugonjwa wenyewe. Kumbuka Africa kuna mafua ya kawaida kutokana na mazingira kama vumbi, hali ya hewa nk.
Sent using Jamii Forums mobile app
[/quoted]acha upumbavu mkuu ada 1m na nusu afu useme anatoza ada kidogo huyo alikuwa na mission zake nyingine Europe
never die with flu😷😷😷😷
Mgawanyiko uko hivyoKatoka nje ya nchi kafika hapa dar lets say kapanda Uber.kamwambukiza dereva abiria tuseme 10 watakaopanda Uber hiyo.
Au katumia gari ya nyumbani.amekuja dereva kumpokea dereva yule ataenda ambukiza walioko kwake.
Na yeye ataambukiza walioko kwake.kama ana watoto wanasoma shule wataambukiza wanafunzi wenzao nao wataenda ambukiza wazazi wao nao wataenda ambukiza wafanyakazi wenzao na wataenda ambukiza watoto wao nyumbani nao wataenda ambukiza wanafunzi wenzao shule,nao wataenda ambukiza wazazazi wao....mzunguko wa maambukizi unaendelea.
Kama aliyetoka nje ya nchi alimwambukiza house girl naye ataenda mwambukiza muuzaji dukani au gengeni naye ataenda ambukiza wa nyumbani kwao nao wataambukiza wenzao na watoto wao nao wataenda ambukiza wanafunzi wenzao n.k
Usije ukadhani wewe upo salama.ujue daladala ,train mwendo kasi,uber,boda na bajaji tayari zinaambukiza Corona watu muda huu.
Usibishe.anza kujikinga.wakati wa kujilinda sasa na kidhaa dhaa.
Hata mie nafikiri hivyo hivyo,alijihisi ni mgonjwa kilichorudisha huku ni nini na asitibiwe huko alikoutoa?choupa moting,
Huyu mama amekaa kwenye nyumba yenye mgonjwa wa corona, angekuwa na busara angeenda kupimwa kulekule Ubelgiji kujiridhisha kama yuko salama ndio aondoke otherwise angepaiwa matibabu kulekule.
Mzururaji tu we unajua kabisa mwenyeji wako anacorona afu unakubali kuingia ndani kwake nakuishi 2. Kwann alipogundua kuwa ameishi nyumba yenye mgonjwa kwanini asiende Hospital hukohuko achungunguzwe kabla haja safiri kuja Africa mi na muona pumbavu tu huyo dadaHivi ni mtanzania au? Mbona slizulula sana ana biashara gani?
Ndugu Mtoa mada; Usipate Hofu; Huyu dada ni Jirani yangu Arusha, (Njiro Corona, Block....) ndipo anapoishi; Lakini pia tumekuwa naye sana Huku Ughaibuni mara nyingi tuu;Hivi ni bahati mbaya kweli mtu atoke safari aende kujipiga quarantine hotelini