Dada wa kazi ni mchoyo sana, nifanyeje?

Dada wa kazi ni mchoyo sana, nifanyeje?

Paa

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2015
Posts
1,462
Reaction score
2,935
Yupo dada wa kazi hapa home,

Chai anaiva wote tukishatoka kwenda kwenye majukumu huko, na anaamka mapema kabisa saa 12, tukirudi jioni tunaikuta kwenye chupa

Mchana hapiki kwasababu sote tunakua hatupo home (hapa sina tatizo)

Shida inakuja usiku, anapika chakula kidogo sana... yaani hata akitokea mgeni tunakosa chakumpa ili ale. Sababu yake anayotoa ni kua mgeni atoe taarifa mchana kabla hajaja ili share yake iwekwe

Anatujali tu sisi hapa wa nyumbani lakini si mkarimu kwa wageni

Ninachompendea anajua kupika sana, chakula chake kizuri

Nifanyeje abadilike?
 
Mpe taarifa kama kutakuwa na mgeni anaye kuja,kusudi aweke share yake.Maana akipika chakula kingi utamsema hana bajeti,anatumia vitu vibaya.

#MPE TAARIFA KUWA KUNA WAGENI,SHARE YAO AIWEKE.
 
Kwa maana hiyo inaonekana hata hicho chakula nyinyi binafsi Kama familia hakiwatoshi!, ila ni Jambo la kuongea naye msiache ajikadirie yy mwenyewe,lazima afahamu kiasi Cha kuwatosha wenyewe kwa kumuelekeza na kuhusu mgeni si ni Jambo la kumpa taarifa tu...
 
Uchoyo wake upo wapi sasa hapo au kuna kitu kingine amekunyima na hausemi?

Pia yupo sahihi mgeni akitaka kuja atoe taarifa hali ya maisha ya sasa yanaenda na bajet

Ila swala la kumwaga chakula hapana bora kupika kwa kiasi hatakama ni chai ni vyema iandaliwe ya kiasi maana kufuru sio nzuri huwa ina nyima riziki.
 
Anajali uchumi wenu. Anapika kinachowatosha mnataka kibaki ili muanze, oh dada utakula kiporo basi...
 
YUKO vzr BINTI SASA wageni wa kuja kuja tu kama chafya wakome mjini hapa na akipika kingi lazima kitabaki ILI asbuh akile kipolo mtoto wa watu MWISHO wa siku awe na kitambi kama madancer wa twanga pepeta
 
Piga chini huyo anakupanda kichwani. 😀 😀

Ila hata mimi ukijakwangu bila taarifa utakunywa glasi ya juice na maji tu,maana ndio havikosekani kwenye friji. Kuhusu msosi utanisamehe kidogo.

Siwezi kula chini ya kiwango changu eti kwasababu umekuja bila taarifa, alafu ushee na mimi shea yanu, NOP.
 
Piga chini huyo anakupanda kichwani. [emoji3] [emoji3]

Ila hata mimi ukijakwangu bila taarifa utakunywa glasi ya juice na maji tu,maana ndio havikosekani kwenye friji. Kuhusu msosi utanisamehe kidogo.

Siwezi kula chini ya kiwango changu eti kwasababu umekuja bila taarifa, alafu ushee na mimi shea yanu, NOP.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]ni kweli maana wageni wengine wanakuja ghafla tu kama chafya na wanataka wale sijui wanadhani kupika ni starehe[emoji849]
 
Mpe angalizo kwamba kuna wageni aina ya ngosha hawanaga taarifa na wakifika ni lazima wakandamize, hawana cha mswalie mtume....
 
uyo dada safi sana natamani wife ajifunze kwake

maana anapikia ukoo familia ya watu 4

nshaongea nmechoka

na kiporo uwa halagii nakomaa nacho ,,,,,[emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom