Dada yangu ana mtaji wa wa Milioni 30, unamshauri afanye biashara gani?

Dada yangu ana mtaji wa wa Milioni 30, unamshauri afanye biashara gani?

Wenye mtaji hawana mawazo. wenye mawazo hawana mtaji.

Wenye mawazo na mtaji wanaogopa kuingia uwanjani kutekeleza mipango yao.

Biashara sio kwa kila mtu. akae kwa kutulia atajua wito wake uko wapi.

Mill 30 hizo aanzishe biashara endelevu iwepo had miaka 40 mbele.
 
Ungetaja location
Mfano yupo DSM

Baada ya hapo ungemuuliza interest zake yeye ni zipi.

Then ndo ungempatia ushauri mzuri.

Kwa kuanza mwambie aanze na mtaji mdogo na baadae atakuwa anakuza biashara taratibu .

Mfano anaweza akaanza na 10M including Facilities Kama frame , leseni n.k

Ila anza na kujua yupo wapi .
 
Anunue kiwanja rufiji hapo anapata kama hekari 5 hadi 10 barabarani halafu aendeee kutafuta hela zingine baada ya miaka mitano! Rufiji aisee! Nawakumbusha Rufiji ni Pwani! Mkoa mpya hapo pwani itakuwa shangwe! Wandengereko hawajastuka bado
 
Kuna watu wa ovyo watakuja wakianza kusema wanaupendo kwa huyo dada etu😁

Biashara, atoe million 10 tu afanye biashara ya kununua mazao kipindi hi hi then anauza baadae.

Mfano Kwa sasa shambani kilogram 1 ya maharagwe ni 1500 ili hali majuzi tu hapo, dukani ilikuwa elfu nne kilogram 1
 
Biashara za ku type kwenye simu..
Mtu akiomba mawazo yako, mpatie if possible, ishu ya kusema biashra za kutype sijui nini , hiyo siyo case yako.

As long as umesha msaidia mawazo kadhaa, mwenye maamuzi ya mwisho ni yeye mwenyewe mwenye mtaji wake, yeye ndo atachuja na kuona kama inawezekana kufanya kwa eneo alilopo au laa!
 
Back
Top Bottom