Dada yangu anaishi na bwana huu mwaka wa 4 hawajafika nyumbani kutambulishana wala kulipa mahari

Mambo mazuri hayataki haraka. Kwani dada anapokuja nyumbani anasemaje kumhusu shemeji yako? Je, huyo shemeji yako hana wazazi wake au ndugu zake? Iliwahi kutokea Shemeji akaozwa marehemu(Maiti) na mahali pengine binti akaangua kilio cha mbwa koko baada ya kukataliwa na wakwe licha ya kuwa aliishi unyumba fake na kuzalishwa na marehemu. Lolote laweza kutokea-chukua tahadhari.
 
Ukisikia Punga ndilo hili

Komaa na maisha yako

Achana na mashine ya dada
 
Wacha hizo wewe! Kwani lazima walipiwe mahari? Mwache ale RAHA wewe!
 
Hujapenda style yao ipi!? Unajua mpaka style wanayotumia!? Kwahiyo unamuonea wivu dada yako? Chunga sana...unakoelekea kubaya.
 
changamoto yako inafanana na changamoto ya jamaa yangu

yeye mdada alifukuzwa kwao, akamchukua akampangia, kama mwaka kapata mimba kajifungua

kaenda kwao, jamaa ajawah enda kumuona mtoto wala kutuma ndugu zake kule ukweni wanamuuliza mama wa mtoto mipango ikoje

mama akiwasiliana na mchizi hana mpango wa kwenda zaidi ya kumwambia ikipita mwezi/miezi arudi waendeleze maisha bila kujitambulisha
 
Ipo siku atalipia gharama
 
Wewe ina kuhusu nini sasa ??

Mpaka katika huo umri bado tu haujajua kuwa katika maisha kuna baadhi ya mambo ni binafsi Kwa mtu na watu wengine hampaswi kuyaingilia ,

Unaanzaje kuyaingilia mahusiano ya dada !?
Jamaa mashamba Sana

Hawa ndo uwa wanasubiri mgao kwenye mahali
 
Kwani kwenye vikao vyenu si mlikubaliana msilipe mahari? Mahari for what?
Mwache mwamba ajipatie mke bure bure
Ishu siyo mahali.
Kujitambulisha muhimu na heshima.
Mimi nimepanga sitapokea mahari ya kuolewa binti yangu.
Simuuzi binti yangu.
 
Alifanya hivo binti yangu mwenyewe, nilimzuia kuja nyumbani hadi afike mme wake nimfaham yeye. Alileta ubishi akataka kulazimisha, mama yake akamsitua kuwa siku ukija baba yako atakupa fumbo za kutosha, baadae mme wake alikuja kujitambulisha.


Kitendo alichofanya dada yako ni ujinga wake mwenyewe, sisi wanaume tunapata uharaka wa kujitambulisha iwapo mwanamke pia anasisitiza hilo. Picha ya huko kwao mwanamke anayeitoa ni mwanamke. Kama dada yako alimwambia mwanamme kuwa haupo uharaka unataka shemeji yako afanyaje??

Mwenye shida ni sister yako, hata hivo yuko prone sana kwa maisha hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…