Dah, nahisi dunia imenielemea, nishikeni mkono

Dah, nahisi dunia imenielemea, nishikeni mkono

Acha ujinga mkuu, serious hata wewe hayo mauzo ya milioni 20 unaweza toa wapi ???
👉 Don't just speak kisa uonekane una type type tu.
👉Nina ki start up, nime ki fund kwa jasho na damu- unadhani kushawishi watu mchezo ehh🙄🤒
Sekta binafsi lazima ufanye kazi na utoke jasho; sijui huko kwingine
 
Oya nipe Pepsi 3 chap🤒
Hizo hapo, au unataka za chupa?
IMG_4715.jpeg
 
Kuna mwamba wangu mmoja hv yeye huwa haamin ushaur wa mtu bas kuna siku alikuwa anakataka kaeneo mjin kati aweke biashara, akaenda kwa wazee wa manispaa akaongea nao wakamwambia hapa utalipa kwa mwez milion 3 jamaa akasema sio kes bas akajitokeza mzee mmoja akamwambia kijana hapa hutopaweza coz,gharama ni kubwa na mzunguko ni mdogo, jamaa akajibu kama nilivyokuwa maskin hamkunishaul saiv nimepata pesa washaur mnajitokeza, sitaki ushaur wenu, nini cha kujifunza mtoa mada, kwanza jifunze kujiamin na kujipa iman ila ukisema kila jambo utake msaada matokeo yake ndio haya kuobwa i d broo hakuna msaada hapa humu wote jobless, kama mi mwongo utanipa mrejesho
 
Ndugu zangu, kaka zangu na dada zangu

Kutokana na kuwa maarufu kiasi Hapa JF, imenibidi nije na Id ya akiba,

Nahisi kabisa dunia imenielemea napambana na changamoto nyingi kwenye suala la kujitafutia riziki (kiuchumi)

Nahisi napambana hadi mwisho wa uwezo, lakini bado ngoma ngumu
Umri wangu ni chini ya miaka 27, elimu yangu ni bachelor degree katika masuala ya lishe, ila kutokana na ugumu wa Maisha na kujisomesha mwenyewe nikabidi niahirishe masomo mwaka juzi nikiwa nimebakisha mwaka na kidogo nihitimu, hii ni kutokana na kukosa ada nikaingia kupambana mtaani.

Nina uzoefu sana katika masuala ya ufundishaji hii ni kutokana na kufundisha baadhi ya shule kama part time teacher wa masomo ya sayansi kama (physics, chemistry, na biology,)

Pia ni mzuri kwenye uandaaji wa practicals na ufanyishaji usimamiz wake

Pia ni mzuri kwenye leadership skills na person management, pia bussiness management nahisi hii ni kipaji kutokana na kuwa kaka mkuu na kiongozi katika levels zote za kielimu nilizowahi kupita

Nina uzoefu kwenye maswala ya computer, excel na microsoft

Pia kwenye kazi za mikono ndipo sasa ninapo pambana, ni mpambanaji wa popote kambi.

Ndugu zangu huku mtaani usipopata wa kukushika mkono Maisha yako yanakuwa magumu sana, unaweza hisi umelogwa, au kama una laana au unaweza kukata hata tamaa ya Maisha.

Maana napitia kwenye kipindi kula ni kuotea, kodi na hata kuvaa shida.

Yani jua linapochomoza tunashukuru Mungu, lakini linapozama pasipo kuingiza chochote unahisi mwili na akili vinashinda unajikuta unakata tamaa kabisa.

Siyo hupambani lakini unajikuta unakosa kabisa yani.

Dada zangu, kaka zangu, mama na baba zangu, mimi ndugu yenu nipo hapa naamini huku kuna watu tofauti tofauti wanaoshughurika na ishu tofauti

Mimi naomba kushikwa mkono, maana ni kweli napambana lakini najikuta sielewi, hata siku hizi kazi tu ya duka hadi uwe na connections binafsi sina connections ya aina yoyote ile, na hata ninaona wanajiweza wengi wamenitolea nje.

Kama moyo wako unakupa kupenda nishike mkono mdogo wako, au mimi mwanao, nipo tayari kufanya kazi yoyote halali kwa nguvu zangu zote na kwa akili zangu zote, na nia yangu yote, pia nipo tayari kuwa mwaminifu .

Kwasasa nipo tayari kufanya kazi yoyote ile ile ila halali ilimradi mkono
Mkono uwende kinywani .

Mungu akubariliki wewe utakayewiwa, pia usinikejeli huwezi jua napitia changamoto gani.

Mengine nimeona si busara kuweka public.

Nawasiliana yangu ni 0656831684
Nimekutumia 700,000 kwenye simu yako hope itakusaidia
 
Back
Top Bottom