Daima iangalie ndoa katika mtazamo wa kibiashara

Issue sio awe mwanamke masikini unachotakiwa uangalie ana offer nini kwako bila kujali ni masikini au Ana hela anaweza akawa masikini but akawa ni nzuri kwenye kutoa ushauri na kumanage matumizi mazuri ya fedha hapo nyumbani na pia akawa mama mzuri wa watoto wako lakini pia kwa Huyo mwenye hela hiyo hela yake inaweza ikawa yenye manufaa kwake sio kwako zingatia hilo au unasemaje Natafuta Ajira
Ni kweli kabisa, tunahoji mwanamke anaongeza value gani kwenye maisha ya mwanaume wengi wanafikiri tunawaza mchango wa kifedha tu. Value inaweza kuwa money management, amani, connection, kukusupport kwenye hustle zako mfano anajua unafanya biashara fulani akairusha status au insta kukutafutia wateja, kukutia moyo n.k
 
Unajua kwanini wazee wetu waliishi umri mrefu na wa furaha? Ni kwa sababu mtazamo wao kimaisha ulikua tofauti na sisi. Waliishi maisha simple tu.

Mfano, pale kijana anapofikia umri wa mtu mzima, anapewa mke na ardhi ya kulima ili aweze kulisha familia yake.

Mke nae aji mikono mitupu, ndugu zake wanampa mali na baadhi ya vitu vya kuanzia maisha maisha mfano jiko na vyombo vingine vya jikoni.

Mke hajali mali za mwanaume wala hana agenda zake mfukoni. Lengo lake ni kutengeneza maisha yao yeye na mumewe.

Asubuhi wanaenda shambani, watalima pamoja. Mwanamke anashughulika na shughuli nyepesi mfano kupanda mbegu wakati mwanaume anawajibika na shughuli ngumu mfano kukata visiki.

Hakuna mwanamke alieingia kwenye ndoa mikono mitupu. Kila mwanamke aliingia kwenye ndoa na mindset ya kutengeneza maisha na mumewe kuanzia chini bila matarajio makubwa na presha kwa mumewe. Hakuna mwanaume alioa mwanamke liability.

Jambo zuri pia pamoja na mke kumsaidia mumewe kutengeneza familia bado hakumvunjia heshima vile vile alimuona kama kichwa na kiongozi wa familia. Ndio maana hata maisha ya wazee wetu yalikua marefu na ya furaha.

Lakini kwenye jamii yetu ya leo narrative imebadilika. Kuna upumbavu umepandikizwa vichwani mwa watu kwamba mwanamke anapokubali kuolewa au kuingia kwenye mahusiano anamfanyia favor mwanaume.

Leo hakuna mwanamke anaetaka kuanza na mwanaume kuanzia chini, mwanamke anaingia kwenye ndoa mikono mitupu akishapata access ya mali zako tu ilo ni bomu linalosubiri kulipuka.

Wanawake wa kisasa wapo smart kuliko wanaume linapokuja suala la ndoa. Wanaangalia future yao kwanza hawapelekeshwi na hisia. Wapo makini zaidi na kipi watakachonufaika kutoka kwa mwanaume.

Ukweli ni kwamba ndoa ni biashara na wanawake wanaujua huu ukweli ndio maana wanautumia kuwaendesha wanaume wajinga ambao hawajua ndoa ni nini.

Sheria ya ndoa, mahakama na jamii kwa ujumla imewarahisishia wanawake kazi katika kutimiza hii azma yao. Mchezo mzima umesukwa kumpendelea mwanamke..

Wanaume tumeishi kwenye ujinga kwa kipindi kirefu ni wakati wa kusema hapana. Tunatakiwa kuanza kuiangalia ndoa katika jicho la kibiashara kama wanawake wanavyofanya.

Angalia zaidi future unapotafuta mke, angalia utanufaika vipi kifedha kutoka kwake, angalia kwa namna gani anaweza kutoa financial support kwenye familia, ana ujuzi gani, anamiliki nini, anakuja kwenye ndoa na nini n.k

Mfano wewe ni mfanya biashara kuna binti mmoja hapo ofisini kwako ni machachali sana kwenye suala la mauzo output yake ni kubwa sana kwenye biashara zako. Chukua uyo weka ndani awe mkeo, mbinu na kismati chake kwenye mauzo ni ni muhimu sana kwa biashara zako.

Approach marriage with business mindset

Wanadamu tunalipa gharama za kutoka kwenye makusudi ya Munhu
 
Uko sahihi

Sahihi.
Ni sababu mwanamke kamwe Hawezi kuwa mwanaume
Wakati wanapigania usawa hawakuwaza kwamba haki sawa inaenda na wajibu sawa. Hawakujui stress, presha na ugumu wa kuwa main character

Walienjoy haki sawa bila wajibu sawa kwa muda mrefu mpaka siku za karibuni walipoanza kukutana na uhalisia wa haki sawa/wajibu sawa, ndio wamekua wakali

ooh wanaume wanakwepa majukumu, saiv hakuna wanaume na blah blah kibao.

How comes mtu unataka kuhudumiwa na kupewa hela ya bure wakati umepewa access zote kutafuta hela kuanzia elimu, ajira, uhuru, kumiliki mali n.k
 
Asubuhi wanaenda shambani, watalima pamoja. Mwanamke anashughulika na shughuli nyepesi mfano kupanda mbegu wakati mwanaume anawajibika na shughuli ngumu mfano kukata visiki.
Hayo ndio maisha niliyokua nikiyaona home na kwa majirani. Kuna muda wanawake wakikomalia kuhudumiwa kwa kila kitu huwa hainiingii. Mama zetu walihusika lwnye uzalishaji mali wa familia. Leo ke akitoa buku jero yake kununua sukari utajua hujui
 
Wakati wanapigania usawa hawakuwaza kwamba haki sawa inaenda na wajibu sawa. Hawakujui stress, presha na ugumu wa kuwa main character

Walienjoy haki sawa bila wajibu sawa kwa muda mrefu mpaka siku za karibuni walipoanza kukutana na uhalisia wa haki sawa/wajibu sawa, ndio wamekua wakali

ooh wanaume wanakwepa majukumu, saiv hakuna wanaume na blah blah kibao.

How comes mtu unataka kuhudumiwa na kupewa hela ya bure wakati umepewa access zote kutafuta hela kuanzia elimu, ajira, uhuru, kumiliki mali n.k
Beijing ilileta shida tupu
 
Naona kila siku kwenye mitandao ya kijamii zinaletwa mada zenye mrengo wa kuipiga vita taasisi ya ndoa. Kwa namna dunia inavyokwenda naona kama kuna hatari kubwa sana ya taasisi ya ndoa kusambaratika na kufa kabisa, hakutakuwa tena na Watu watakaooana katika jamii.
Kwa Sasa imeanza kujengeka hisia kwamba ndoa siyo kitu kizuri.
Ndoa sio kitu kizuri tena, kwani uongo?
 
Saiv mwanamke anataka nafasi ya mwanaume, privilege ya mwanamke lakini hataki kubeba wajibu wa mwanaume wala wa mwanamke, ni vulugu mechi
Yaani haya mambo yanachanganya acha tu mkuu. Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya wanawake nowadays kwenye ndoa wanataka kuchukua nafasi ya wanaume halafu waendelee kuonekana wanawake. Yanatukata sana haya hawajui tu
 
Ila mleta mada hajaipinga nfoa bali anatukumbusha wanaume juu ya muelekeo wetu kwenye ndoa.

Nakubaliana na mtazamo wake kwa zaidi ya 90%. Ndoa ni biashara ya kuishi pamoja, lazima mwanaume azingatie uwezo wa uzalishaji wa mwanamke anayetaka kumuoa.

Kuoa mwanamke tegemezi ni chanzo kikuu cha kuvunjika ndoa nyingi. Ndoa nyingi zinavunjika sababu ya utegemezi wa mwanamke na wala sio usaliti kama wengi wanavyodhani.
Wakati mwingine wasio tegemezi nao wanakuwa na viburi vya pesa... Heshima na utii unapungua... Ila wapo baadhi yao ambao wanajiona kama supporters kwa waume zao. Ndoa zao zinakula mema aisee
 
Mpango wa Mungu katika familia ni mwanaume uwe main provider, mwanamke awe mlezi mkuu.

Hata katika kutoa adhabu: Adam alipewa adhabu ya kula kwa jasho na Eva kuzaa kwa uchungu - kila mmoja kulingana na majukumu yake ya msingi.

Unapotaka kuoa angalia mwanamke mwenye past safi (bikira), mwenye uwezo wa kuwa mlezi mzuri wa familia. Wajibu wetu kama wanaume ni kuhudumia familia, kuilinda na kuwa viongozi.

Mwanamke si provider, in fact dunia ilianguka (dhambini) siku Adam alipomruhusu mwanamke kuchukua nafasi yake kama provider na kiongozi.

Tuishi humo.
 
Back
Top Bottom