Daisle Ulomi aliwahi kuwa askari, jeshi la polisi linapaswa kuwa na majibu

Daisle Ulomi aliwahi kuwa askari, jeshi la polisi linapaswa kuwa na majibu

Hii nchi Kila kitu siasa . Mmeambiwa mtu kapata ajali ya pikipiki na hospitali wamethibitisha hilo watu mmekazana kauwawa kauwawa haya pelekeni ushahidi mahakamani basi ili hao wahusike wawajibishwe .
 
Kama juzi masawe nae katapeli gari na milioni 95 za watu akajificha na kutoa taarifa kuwa ametekwa wakina boni Yai mbio mtandaoni kumbe wanampigania tapeli. Tuwe makini wahalifu wanajificha kwenye ishu za utekaji kufanya mambo Yao.
 
Kuwatetea polisi na single maza ni kazi ngumu sana kwa sasa.
Binafsi naona kwenye upoti ndio ngumu zaidi hasa haya matukio ya kusitisha uhai na kwakuwa wamepewa jukumu la kulinda raia na Mali.

Jukumu zito na nyeti labda wapeleke vipanga wawe polisi(kama wazee WA njiwa WA 2010 kurudi kizani) na kuwainulia maslahi.

Lasivyo kuna magumu mengi yanakuja
 
Hili nina uhakika nalo kuwa Daisle Ulomi alikuwa askari wa Jeshi la Polisi Tanzania ila sina uhakika kama aliachana na hiyo kazi(Hapa ndipo swali lilipo kuhusu kifo chake, Ulomi kauawa) maana ni siku nyingi sijaonana naye ila ufahamu wangu na hata kiapo naweza thibitisha kuwa Daisle ulomi alikuwa askari wa jeshi la polisi Tanzania.

N.B; Nilikutana na Daisle Simon Ulomi at Tumaini university Dar es Salaam College(Tudarco).

He was a good brother, sikutegemea km kuna siku atauawa kikatili hivi.

Pumzika kwa amani kamanda DView attachment 3178324
Tanzania ni shimo la wachinjaji sasa.

Mungu atusaidie
 
Hii nchi Kila kitu siasa . Mmeambiwa mtu kapata ajali ya pikipiki na hospitali wamethibitisha hilo watu mmekazana kauwawa kauwawa haya pelekeni ushahidi mahakamani basi ili hao wahusike wawajibishwe .
Kaka hapa taarifa zina kosa ushirikiano aisee ndio maana unaona kuna minong'ono,
Ajali alipata lini na mwili ulipelekwa lini na Taarifa ya mwili kupatikana imetolewa lini?

Smatifoni pia zinatoa mwanya WA Taarifa kujipinga.

Ulishawai kupotelewa na ndugu au jamaa yako WA karibu?
 
Hiyo ajali aliipata mwenyewe na eneo gani? Na alipata ajali ya aina gani? Kuna mastory mengi buana
Ukiwa TISS ukiamua kuacha kazi basi inabidi ukimbie nchi kama alivyofanya Chahali ,ukisema ukomae nchini lazima wakurestishe in PC either Jambazi Sugu auawa ,utakutwa mtaroni ,kisimani au ajali ya bodaboda.
 
Kwa mtanziko huu jukwaani Tumwamini nani?Dini yangu inanifunza kwAmba Akikujieni mtu na Habari yoyote basi ichunguzeni kwani mnaweza kumdhuru mtu ambaye hakustahiri"kwa mujibu wa mafunzo hayo nimechagua kukaa pembeni sitomshutumu yoyote sio Polisi,Ccm,wala marehemu kwani wabongo tuna chanzo kinaitwa nimesikia'
 
Kwa mtanziko huu jukwaani Tumwamini nani?Dini yangu inanifunza kwAmba Akikujieni mtu na Habari yoyote basi ichunguzeni kwani mnaweza kumdhuru mtu ambaye hakustahiri"kwa mujibu wa mafunzo hayo nimechagua kukaa pembeni sitomshutumu yoyote sio Polisi,Ccm,wala marehemu kwani wabongo tuna chanzo kinaitwa nimesikia'
 
Binafsi naona kwenye upoti ndio ngumu zaidi hasa haya matukio ya kusitisha uhai na kwakuwa wamepewa jukumu la kulinda raia na Mali.

Jukumu zito na nyeti labda wapeleke vipanga wawe polisi(kama wazee WA njiwa WA 2010 kurudi kizani) na kuwainulia maslahi.

Lasivyo kuna magumu mengi yanakuja
Mkuu una hoja lakini nadhani tungetangulia kuzuia vilaza wanaoingia bungeni kutunga sheria mbovu. Polisi na TRA wanatekeleza sheria zisizo rafiki ndo maana lawama haziishi. Vipanga kuwa polisi haitasaidia kama sheria zitaendelea kubaki hizihizi.
 
Kaka hapa taarifa zina kosa ushirikiano aisee ndio maana unaona kuna minong'ono,
Ajali alipata lini na mwili ulipelekwa lini na Taarifa ya mwili kupatikana imetolewa lini?

Smatifoni pia zinatoa mwanya WA Taarifa kujipinga.

Ulishawai kupotelewa na ndugu au jamaa yako WA karibu?
Nakuhakikishia ukienda amana au mwananyamala hospital au hata muhimbili mochwari utaoneshwa maiti za ajali nyingi tu ambazo hazijafuatwa na ndugu zao kutambuliwa au zimetelekezwa. Sasa kwanini kwa huyu ulomi ionekane ni maajabu?
 
Wale mliokuwa na mashaka kuhusu maelezo yangu nadhani tuhitimishe mjadala;
Screenshot_20241219_193225_Facebook.jpg
 
Utata ni tarehe ya kifo na taarifa ya polisi kuwa kimya tangu 11.12.2024 alipopelekwa hospital Mwananyamala mpaka 16.12024. Kwa nini Polisi walikaa kimya wakati taarifa za kupotea zilishazagaa kwenye mitandao na taarifa ilikwishatolewa polisi. Simu, vitambulisho vyake vipo wapi. Waliomuokota ni nani. Alipata ajali wapi. Kwa maelezo aliondoka mchana saa 6 ambapo haiwezekani watu wasishuhudie tukio kweupe.
Walikuwa wanatunga uongo
 
Back
Top Bottom