Dakika chache kabla ndege haijaanguka unadhani abiria huwa katika hali gani?

Dakika chache kabla ndege haijaanguka unadhani abiria huwa katika hali gani?

KUNA SIKU TUNATAKA KUTUA JFK USIKU KIPINDI KILE CHA FAST JET PILOT KESHATOA MATAIRI NYUMBA TUNAZIONA HIZ HAPA SASA BWANA SIJUI KULIKUWA KUNA SHIDA GAN CHINI ILE TUNASHUKA TU PILOT AKAIRUDISHA NDEGE KWA KASI YA AJABU JUU TUKAANZA KURUDI JUU KWA KASI YAAN SIKU NDEGE NZIMA KELELE SASA ZIKAANZA MI MOYO UNADUNDA MAPAKA NAUSKIA KWENYE MGONGO NIMESHIKLIA SITI YA MBELE KWA NGUVU ZOTENIKASEMA YAAN HATA KAM NINGEOKOTWA MAFUVU YAMESHIKLIA SITI KUNA MNYAKI ALIKAA PEMBEN YANGU HAPA NASKIA TU OBABAAA FIJOFIJO KUNA MAMA ALIKAA SITI TOFAUTINA MUMEWE ANAPIGA KELELE JINA LA MUMEWE DINGI NIKASKIA ANAMJIBU WE MWANAMKE HEMBU KAA CHINI TULIA YAA ILIKUWA KIMWEU MWEU
Duuh Fast jet hadi JFK? Mlitisha!!
 
Nikikuwa natoka Joburg Oliva Tambo International Airport kulelekea mji mmoja wa Manzini, Swaziland pale kuna mwendo kama wa saa moja hv....
nakumbuka nilipanda ndege ya wastani mithili ya hizi za precision air lkn yenyewe ilikuwa ndogo kidogo, basi baada ya kama DK 30 kuruka...
tulikutana na upepo mkali balaa kitu kilitetemeka kikayumba kikaanza kwenda chini kwa speed...
pembeni yangu alikaa mzungu flani hivi anasoma novo nikamkata jicho nicheki reaction yake manake nilikuwa najisemea hawa rangi nyeupe wamezoea ndege.....
ile namcheki nikakuta kafunga novo yake amebana mikono kifuani kafumba macho,nikasema lelo ni leo kucheki abiria wengine nao nikaona wanaweweseka, jasho likanitoka paa mpaka kwenye pu.mbu baada kama dk7 hali ikatuli ndege ikarudi juu zaidi baadae tukataambiwa zilikuwa ni turbulence.....
nilitamani ndege itue nishuke fasta....
Kuna sehemu ukitoka Joberg kwenda Cape Town huwa kuna turbulence ya kufa mtu.
 
Mbaya sana
Tulipata msukosuko over Alps na KLM sitasahau

dege linatikisikaa mara likadrop altitude ghafla hiviii watu hoiii..tukakaa stable kdogo likadrop tena ahh acha tu ilikua experience mbaya sn cz walikua wanaserve vinywaji rubani akatangaza warudi kukaa kwanza
 
Hayo yote apo juu yanaweza yasitokee hata kidogo. Nulikutana na situation 1 mwaka 2014 nikitokea Abu Dhabi kwenda Bangkok (sitotaja jina la shirika la ndege) na ilikuwa usiku kama saa 8. Tulikuwa tumeshavuka kipande cha 1 cha Indian Ocean/Arabian Sea, tumeshavuka India/Hyderabad na sasa tumeanza kipande cha 2 cha Indian Ocean hili tuvuke kwenda Thailand mara ghafla ndege ikaanza kushuka wakati ikitembea pia na ikaendelea kushuka kwa kasi kubwa lkn ikisonga mbele pia. Abiria kwa bahati mbaya tulikuwa tumetangaziwa tufungue mikanda kitambo so almost psgs wengi walikuwa wamefungua mikanda na kilichotokea ni kwamba psgs ambao hawakufunga mikanda nikiwemo mimi tulibaki kama tunaelea hewani kwa sababu nakumbuka nilikuwa nasikia gap kati ya makalio na seat na hii ilitokea almost kwa psgs wote ambao walikuwa hawajafunga mikanda. Ndege ikashuka toka around 38,000ft mpaka 19,000ft kwa mda mfupi sana then ghafla ikaanza kupanda juu. Cha hajabu kwa mda huo mfupi hatukusikia sauti ya cabin crew yeyote zaidi ya kelele kidogo tu za psgs na mimi nilikuwa nashangaa tu kwa sababu nilianza kutetemeka baada ya incidence kuisha. Baadaye rubani akaomba radhi kwamba tulipita kwenye eneo lililokuwa na VACUUM na uwa inatokea once in a while so ndege ikakosa support ( infact alitumua lugha zao sijuhi aerofoil na maneno mengine I was no longer interested nilikuwa natetemeka tu). So that day nikagundua kwamba kumbe kufa ni very simple kwa sababu tayari ndege imeshashuka almost 50% ina maana in the next 2-3 minutes tungekuwa kwenye maji.
Duhh thats a lot of altitude poleni sn
 
Kwa ambao hamjawahi kupanda ndege huu sio uzi wenu. Nyie anzisheni uzi wa bodaboda na hiace maana ndege hazidondoki kwa ghafla zikiwa juu sana.

Nyie wa bodaboda hatua yenu ni moja tu dreva akikosea kinachofwata ni baaaaaang na hapo mnakuwa hamna miguuu pua nk.
Acha dharau dogo
 
Kwa ambao hamjawahi kupanda ndege huu sio uzi wenu. Nyie anzisheni uzi wa bodaboda na hiace maana ndege hazidondoki kwa ghafla zikiwa juu sana.

Nyie wa bodaboda hatua yenu ni moja tu dreva akikosea kinachofwata ni baaaaaang na hapo mnakuwa hamna miguuu pua nk.
[emoji3][emoji3][emoji3]ninecheka!
Anyway,sitaki hata kuwaza!
Ilishawahi kutokea,sikumbuki hata niliwaza nn!
Acha kabisa
 
Kuna huyu rubani wa bombadier tunatoka Mbeya tunarudi Dar aliachia kama sekunde 3 tu ikashuka chini.
Aisee kuna binti mmoja alinikumbatia kwa uoga na wakati huo mi mwenyewe kiroho kinadunda balaa.
 
Kuna huyu rubani wa bombadier tunatoka Mbeya tunarudi Dar aliachia kama sekunde 3 tu ikashuka chini.
Aisee kuna binti mmoja alinikumbatia kwa uoga na wakati huo mi mwenyewe kiroho kinadunda balaa.
Huu mchezo upo ATCL kuna rubani hufanya haya na si mara moja.
 
Ni hali inatisha sana MKUU,,

Siku moja nipo kwenye Qatar airways,,

Natoka Qatar naelekea saudia.


Tukiwa angani umbali wa futi kama 30000 hivi kutoka usawa wa bahari.

Nusu saa baada ya ndege kuruka.,,

Ilikuwa kama nataka kupitiwa na usingizi hivi,,

Maana nilikuwa nimechoka sana,,baada ya kukaa muda mrefu pale Doha international airport kusubiri kuunganisha ndege.
Nilikaa zaidi ya masaa 7...lounge,, kusubiri connection.

Basi nikiwa kausingizi kama kananipitia hivi ,,,,

kwa mbaali nikasikia mtu anapayuka kwa sauti ,,
ALAH AKBAR!!! ,

ALAH AKBAR.!!

Nilishtuka usingizini nikakuta ndege kama inatetemeka fulani hivi,,

Mithili ya gari inayolazimisha kupita kwenye korongo.

Kumbe yule muarabu nae alikuwa yupo usingizini ni kama alikuwa anaota fulani hivi.

Nae aliposhtuka kukuta kumbe ni really basi akazidisha kelele,

ALAH AKBAR!!

ALAH AKBAR!!

Hata kufanya wale wahudumu wa ndege kukimbilia alipo yeye.,,

Basi alizua taharuki Kama dk 2 hivi ,

Kwa watu wote waliiomo mle ndani especially wale waliotoka usingizini,,

Ilikuwa kelele tupu mle ndani,,

Mimi tayari nilikuwa nahisi boxer niliyovaa inaanza kuwa nzito.,

Na kilichoongeza uzito wa boxer sikijuwi.,

Baada ya kelele kutulia na ndege kutulia,,,

Ndipo nilipokigunduwa kilichoongeza uzito wa boxer ,,

Ila Itabaki kuwa siri yangu..

Ila mkuu asikwambiye mtu, hizi ndege tunapanda lakini mashaka matupu.

Ndy maana sisi mabaharia tunaamini usafiri ulio salama ni meli pekee,,

Na sio

-- ,ndege,

--Train.

--Gari.
Wewe si baharia Karenga
?[emoji16]
 
Back
Top Bottom