Tuendeleee..........
Nilienda town nikachukua viraba vya mazoez vya buku 8 haikuwa njumu kabisa ila ni raba nyepesi ambazo ni nzuri kwa kuchezea mpira kwa sisi ambao tulikuwa tunacheza kujifurahisha.
Siku ile ile nilianza kwenda chuoni kwaajili ya mazoez.
Baada ya tizi nikachukua baiki yangu kurudi magetoni njiani nilikuwa nakokota huku nikichat na Mercy na akanambia anaendelea vizur na safar na yalikuwa yamebak kama masaa mawili au matatu wafike. Siku ile nilichoka sana nikaamua kuoga then nikaenda kijiweni kula ili mambo yasiwe mengi.
Baada ya kula nipo zangu geto Mercy fek kanichek kaniuliza nipowapi nikamjibu home akasema anakuja kwani ana kitu cha kuongea na mimi.
Nikajiuliza huyu dem anataka nini ila nikasubr aje nimsikilize.
Hazikupita hata dakika mtu huyu hapa, kachoma ndani kanikuta kitandani naye akakaa pembeni yangu. Nikamkaribisha, nikamuliza nambie kuna mpya gani. Kaniuliza ni hatua gani nitachukua endapo atanithibitishia kwamba Mercy anatembea na Dokta nikamjibu mimi ni mwanaume na nishaanza kujifunza kuwa mvumilivu na kuhimili changamoto za mahusiano.
Mercy fek akatoa cm akafungua gallery akanionesha picha, alichukua cm ya Dokta akapiga picha chat za Dokta na Mercy. Chat zilikuwa zinaonesha Dokta alikuwa anamuliza kuhusu safar na kumtakia safar njema.
Mercy fek akanambia hakutaka kupiga zile texts mbya zaid za kiniumiza lakini it's true Mercy wangu alikuwa ananicheat silently.
Nilimkatisha asiendelee kuongea na nikavuta pumzi ndani kwa nguvu na kuitoa nje ili nitafute relief angalau. Mercy fek akaanza kama kuleta pigo za kutaka dudu ya yuyu nikamkata jicho elekezi na hapo alinielewa na akaahirisha mpango wake. Akavunga vunga pale anasikiliza mziki then akasepa zake nikabak alone. Siku ile pia nililia kisa Mercy, lakini mwisho wa siku nikaona hata nifanyaje wa kuokoa penz letu sio mimi hali ni Mercy kwahyo ikabidi nirelax tu nisiwe na makuu kwani hata kama ningegaagaa chini isingesaidia kitu.
Nikajikaza kitandani ghafla simu ikaita alikuwa Mercy,nikapokea kinyonge sana. Akanambia kafika nikampa pole basi nikamwambia apumzike ili aniache nilale zangu pia. Usiku ule ulikuwa mbaya sana maana niliandamwa na ndoto za kijingajinga sana nikaona dalili za kupata shida ya afya ya akili japo sikulitilia maanani sana hilo swala kwa muda ule.
Kesho yake niliamka nikafua fua pale, nikapika tea nikapiga.
Mercy alipiga cm tukaongea kwa muda kidogo nikajikuta naanza kuongea sana kumsihi Mercy asiruhusu mapenz yetu yavurugike. Mercy aliniuliza kwani kuna shida gani? Umeona nini mbona unanihubiria sana kuhusu kuwa muaminifu? Nikaona hili ni swali ya kizushi namimi nkampunch nkamwambia hakuna shida ila awe tu makini asije kuniharibia future yangu.
Asee pamoja na kuwahi kupitia katika mahusiano kadhaa kabla ya Mercy lakini nikiri wazi kwamba Mercy aliuteka sana moyo wangu na sikuwa na la kufanya ila hatma yangu ilikuwa mikononi mwa Mercy.
Siku zilienda likizo ikaisha na Mercy akawa anakuja siku hiyo yani anarud chuoni. Siku hiyo Mercy alinambia kwamba atachelewa kufika kwasababu gari imepata shida njiani kwahyo watafika usiku around saa tano, akanambia haina haja ya kwenda kumpokea kuna anko wake ataenda kumchukua stand na atalala kwake.
Mmmmh nikaona hapa tayari gari imekata break kwenye mteremko sitaweza kuikontrol labda niichome mtaroni.
Kiukweli sikuridhishwa na majibu ya Mercy nikamwambia hapana mimi nitakuja kuchukua nitakuja na bodaboda asiwaze wala kumsumbua anko wake.
Mercy kweli aliwahi kunambia ana anko wake pale mjini na siku moja moja alikuwa anaenda kuwasalimia.
Nilimganda sana Mercy mwisho wa siku akakubali niende kumpokea. Kwasabb alikuwa kanambia jina la gari hasi nikawaza niwahi mida ya saa4 niwepo around ili akishuka anikute pale. Ilipofika saa3 na dk45 nilimpigia boda tukasepa stand.
Cha kushangaza nilipofika stand nikakaa kama dk 20 ile gari ikaingia.
Mercy alivoshuka alistuka sana alivoniona akaniuliza umefika mda gani hapa? Dereva kakimbiza sana gar ndomana nimefika kabla ya muda nilokuelekeza.
Nikampokea sikutaka tuongee sana pale, tulipanda boda tukapotea. Njiani cm ya Mercy iliita kama mara tatu hivi na sms ziliingia kadhaa. Lakini sikutaka kumuuliza Mercy kuhusu hizo cm na sms.
Hii ndo ilikuwa siku rasmi Dokta alianza kuonesha ROHO mbaya mpaka ikapelekea kuandika Uzi huu na kuupa jina hilo.
See you............
===
Muendelezo soma
Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy