Jukwaa la @JamiiCheck.com limechambua kuhusu unywaji wa vinywaji vya kuongeza Nguvu (Energy Drinks) unavyoweza kuwa na Athari kwenye Mwili wa Binadamu
Dkt. Anthony Gyunda, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani na Figo wa Hospitali ya Muhimbili – Mlonganzila anasema “Baadhi ya madhara ya Matumizi yaliyopitiliza ya kinywaji hicho ni kuathiri Uzazi, vinapunguza Madini muhimu ya kuzalisha Mayai kwa Wanawake na Mbegu za Kiume, hivyo inaweza kusababisha tatizo la Ugumba na Utasa kwa Vijana ambao ni watumiaji wakubwa.”
Magonjwa mengine ni Shinikizo la juu la Damu, Maumivu ya Kifua, Sonona, Kifafa, Kichaa, Uraibu pamoja na Figo kushindwa kufanya kazi
Soma
KWELI - Matumizi Makubwa ya Vinywaji vya kuongeza nishati (Energy Drinks) husababisha Madhara kwenye Figo
#FactsChecking #FactsCheck #JamiiCheck #HakikiHabari #PublicHealth #JamiiForums
View attachment 2918675