Daktari Bingwa: Kuna kilevi kwenye kinywaji cha “energy”

Amazing Side of the Life ni kwamba Unywe usinywe energy drinks, sijui uwe vegetarian, sijui ule unakula Pork au nyama nyekundu, sijui uwe mlevi, mvutaji nasema hivi KIFO KIKO PALE PALE.
Tena unaweza kuta mvutaji sigara akaishi miaka mingi kuliko vegetarian..! So Kuna siri kubwa sana kati ya Mungu na Uhai wa viumbe vyake.

Yaani wakati hata kabla hujaja duniani Mwenyezi Mungu anajua kabisa utaishi miaka mingapi hiyo ni siri hapo Nimeongelea mambo ya Rohoni.

Ila ya mwilini ndo haya tunayopigana kila siku usile hiki kula kile, fanya mazoezi haya...
Ishi maisha yako yanayokupa furaha ilimradi usimkufuru Muumba wako( kwa wale wa Imani).
 
Mkuu nasikitika bado hujaelewa hoja. Hebu rudia tena kusoma utaelewa maudhui yaliyomo kwenye munakasha huu.
 
energy ni dawa lakini jamaa zangu wanaifanya kama juice ya miwa tu😁😁.

kwenye lebo yake kuna maelezo ya onyo makini kabisa,kwamba haishauriwi kwa mjamzito,mtoto na mwenye zuio la matumizi ya cafein,na kwa asiye na vigezo hivyo hapo juu asizidishe chupa mbili kwa siku,asinywe muda mfupi kabla ya kulala.

sasa ndio hapa unasoma mtu alikuwa anapiga chupa 5 kwa siku😁😁,unawaza ana nia gani na walioandika hilo angalizo hapo juu,wafukuzwe kazi ama???

by the way hii ni solution muhimu sana kwa wenzangu wakemia wa counter😁😁,zina uwezo mkubwa sana wa kukata makali ya spirit mbali mbali,zikawa na test kama juice tu.
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Juzi niliongea na daktari bingwa anayemiliki hospitali kubwa jijini kuhusu chanzo cha uraibu unaosababishwa na kinywaji cha energy. Daktari huyu alinihakikishia kwamba kinywaji chochote kinachosababisha uraibu lazima kinakuwa na kilevi au dawa za kulevya.

Jibu hili lilinifanya nifikiri sana kuhusu kinwaji cha energy kinachotengenezwa na matajiri wakubwa wawili hapa nchini. Madhara ya kinywaji hiki yamewahi kufanyiwa utafiti na madaktari wa hospitali ya Muhimbili ambao waliwahi kumfanyia upasuaji wa mishipa ya moyo iliyoziba mgonjwa mmoja mraibu wa energy ambaye alikuwa akigida sio chini ya chupa 5 za energy kwa siku.

Napenda kuelekeza lawama zangu kwa matajiri hawa wawili wanaowaua raia kimyakimya huku serikali ikiwa imekaa kimya imejikita kwenye ukusanyaji wa kodi wakati afya za wapigakura zinadhurika. Dawa za kulevya na vilevi vinavyotiwa kwenye kinywaji cha energy zina madhara makubwa kuliko uvutaji wa bangi au sigara.

Bangi imepigwa marufuku hapa nchini. Watengenezaji wa sigara wanaandika onyo kwenye paketi ya kila sigara: uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako. Ni kwanini serikali haiwahimizi hawa matajiri wawili waandike maandishi kwenye chupa za energy:….unywaji wa energy ni hatari kwa afya yako….kama ilivyo kwenye sigara? Ina maana wameamua kuwaacha wapigakura wauawe na matajiri halafu mwaka 2025 nani atawapigia kura?

Sijawahi kuona nchi ya ajabu na isiyojali afya za wananchi wake kama hii nchi ya kusadika na kufikirika, Tanzania. Watawala wanataka wafe watu wangapi ndipo wachukue hatua? Inasikitisha na inahuzunisha sana.
wacha wajinga wajiue wenyewe,,,wewe unjua kabisa bangi mbaya unavuta,ulevi mmbaya unalewa,umalaya ni kifo unaendelea kunyanduana mpaka unapata ukimwi,sigara inaleta cancer unavuta,kuendesha gari speed ni hatari unaendesha,uvivu ni umaskini,unaendekeza usingizi,kula ovyo ni hatari,unafuga kitambi,,,,,acha mufe tu,,,mnailaumu serikali bure!!!!! kwani unavofanya uzinzi serikali imekulazimisha?? kwani unavonunua energy kuna shinikizo la serikali???? acheni hizo mambo"mtakufa sana"
 
Kwanini serikali isizuie utengenezaji wa hizi energy zinazoua watu kila kukicha? Mbona wanazuia bangi na kuwaacha Mo na Bakhresa waendelee kuwaua raia wasiokuwa na hatia? Sio vizuri na haipendezi hata kidogo.
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Juzi niliongea na daktari bingwa anayemiliki hospitali kubwa jijini kuhusu chanzo cha uraibu unaosababishwa na kinywaji cha energy. Daktari huyu alinihakikishia kwamba kinywaji chochote kinachosababisha uraibu lazima kinakuwa na kilevi au dawa za kulevya.

Jibu hili lilinifanya nifikiri sana kuhusu kinwaji cha energy kinachotengenezwa na matajiri wakubwa wawili hapa nchini. Madhara ya kinywaji hiki yamewahi kufanyiwa utafiti na madaktari wa hospitali ya Muhimbili ambao waliwahi kumfanyia upasuaji wa mishipa ya moyo iliyoziba mgonjwa mmoja mraibu wa energy ambaye alikuwa akigida sio chini ya chupa 5 za energy kwa siku.

Napenda kuelekeza lawama zangu kwa matajiri hawa wawili wanaowaua raia kimyakimya huku serikali ikiwa imekaa kimya imejikita kwenye ukusanyaji wa kodi wakati afya za wapigakura zinadhurika. Dawa za kulevya na vilevi vinavyotiwa kwenye kinywaji cha energy zina madhara makubwa kuliko uvutaji wa bangi au sigara.

Bangi imepigwa marufuku hapa nchini. Watengenezaji wa sigara wanaandika onyo kwenye paketi ya kila sigara: uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako. Ni kwanini serikali haiwahimizi hawa matajiri wawili waandike maandishi kwenye chupa za energy:….unywaji wa energy ni hatari kwa afya yako….kama ilivyo kwenye sigara? Ina maana wameamua kuwaacha wapigakura wauawe na matajiri halafu mwaka 2025 nani atawapigia kura?

Sijawahi kuona nchi ya ajabu na isiyojali afya za wananchi wake kama hii nchi ya kusadika na kufikirika, Tanzania. Watawala wanataka wafe watu wangapi ndipo wachukue hatua? Inasikitisha na inahuzunisha sana.
dawa nyingi za binadamu zina kilevi.
 
Hata sio masikini bali umasikini wa akili. Wanaokunywa mo kwa wingi, sungura unaweza kukuta kutwa anachoma hata 5000 kunywa hivyo vidude ambayo hiyo 5000 inaweza nunua chakula kizuri akala. Wengi boda boda, mafundi ujenzi n.k
Mafundi ujenzi wanavinywa sana hata sielew kwanin
 
Pitia haya mambo
Kilevi ni nini ?
Stimulants ni nini ?
Depressants ni nini ?

Hata Kahawa ni Stimulant...

Baada ya hayo kila kitu kikizidi hakifai na sio vizuri kuwa tegemezi wa chochote kile
 
Kuna siku nilikuwa hospital Fulani hivii ina jina kubwa tuu Dar kuna mtoto alikuwa anakunywa energy kapewa na mama yake,
Aisee, Doctor alivyo ona alifoka sana.
Nataka kusema hata sisi wazazi tulinde kizazi chetu kuna kama sie tumeshindwa kujilinda.
Kweli kabisa mkuu; kuna baadhi ya wazazi vilaza wanaoharibu afya za watoto wao kwa kuwalisha vyakula na vinywaji vya ajabu halafu wakishapata madhara wanaanza kuilalamikia serikali.
 
Azam Energy:
Ingredients. Carbonated Water● Sucrose● Glucose Syrup● Acidity Regulators (Citric Acid● Sodium Citrate)● Taurine● Preservatives (Sorbic Acid● Benzoic Acid)● Caffeine (0. 03%)● Artificial Sweetener (Sucralose)● Vitamins (B3● B6● B12)● Glucuronolactone● Inositol.
 
Back
Top Bottom