Daktari wa Kichina afariki akimuokoa mama aliyekuwa anazama majini Kigamboni

Daktari wa Kichina afariki akimuokoa mama aliyekuwa anazama majini Kigamboni

View attachment 3374554

Tumempoteza daktari bingwa wa dawa za usingizi hospitali ya taifa Muhimbili. Dr.Zhang Junqiao amefariki juzi tarehe 15/06/2025 huko Kigamboni baada ya kuzama majini wakati akimuokoa mwananchi aliyekuwa anazama. Siku ya tukio Dr.Zhang alimuona mwananchi akizama na yeye kuamua kujitosa majini kumuokoa. Alipomfikia alimpatia jaketi lake la kuogelea na yeye kwa kuwa ni mzoefu akaogelea bila jaketi. Raia aliyekua akizama alifanikiwa kuokolewa, lakini maji yalimzidi nguvu Dr.Zhang akazama na kupoteza maisha.

Dr.Zhang alikuwa daktari Bingwa wa Dawa za Usingizi na Ganzi (Anesthesiologist), raia wa China aliyekuwa anafanya kazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Dr.Zhang alikua alikua na shahada ya udaktari wa binadamu (Bachelor of Medicine) Shahada ya upasuaji (Bachelor of Surgery), shahada ya umahiri katika matibabu ya ndani (Master of Internal Medicine) na shahada ya umahiri katika dawa za usingizi (Master of anesthesiology). Pia alikua na cheti cha ithibati ya kimataifa cha kuhudumu kama daktari bingwa wa dawa za usingizi katika nchi zaidi ya 100 duniani (NMLE).

Dr.Zhang atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuhudumia jamii ya watanzania, pamoja na umahiri wake kufundisha njia mpya za dawa za usingizi na ganzi. Atakumbukwa pia kwa ucheshi wake, uchangamfu wake na passion yake katika kazi. Dr.Zhang amekufa kishujaa akijaribu kuokoa maisha ya Mtanzania mwenzetu aliyekua akizama. Huu ni upendo wa ajabu. Dr.Zhang amefariki akiwa na umri wa miaka 38. Tumuombee pumziko la amani.!

Malisa
Tasnia ya Afya imegubikwa na majonzi mazito baada ya mwamba kuondoka
Hasara kwa taifa, hasara kwa Tasnia

Jajajanja arts The Mongolian Savage unadunda ardhi ya Mola hii
 
Maji hayana mjuzi
Udogoni nilinusurika kufa maji nikaokolewa.

Nilikua na Fred tukaendesha baiskeli zetu akanipeleka kwenye bwawa kubwaa sikua nimewai kuogelea ages 9

Mzee nikanasa kwenye tope nikanywa maji mengi nikaja vutwa kutoka nje kamuliwa maji..for sure zaidi ya week mbili Mimi sisikii vizuri

Mpaka Leo issues za kuogelea Mimi ni MPENZI MTAZAMAJI EVEN IN SWIMMING POOL #SIOGELEI SIOGII 🥺
 
Samahani unaweza ukainisha na miaka yao walivyosoma ili tuone maana kusema wamesoma hivyo na wana uzoefu kazini hesabu zinagoma mkuu au huko nje unaweza soma vitu viwili kwa wakati mmoja?
Wewe unataka ligi mimi naongea ninacho kijua. Unaweza kuwa ulisoma zamani ukaona ni ngumu kwa sasa hilo lipo na wapo.

Ningekutajia na majina lakini siyo ustaarabu na sioni sababu kufanya hivyo.

Wewe unaweza kuwa mtu mzima kama mimi tuliosoma muchs-udsm zamani lakini vijana wapo wamesoma hizo leveal kuanzia kibaha, russia, muchs-udsm, russia, india.
 
Nataka niwaonye wale wote wanaocheza na maji especially baharini.
Humo Kuna mauzauza mengi sn usicheze na bahari hata kama ni mjuzi wa kuogelea kiasi gani.

Heshimu bahari.
 
Rip
IMG-20250618-WA0038.jpg
 
Udogoni nilinusurika kufa maji nikaokolewa.

Nilikua na Fred tukaendesha baiskeli zetu akanipeleka kwenye bwawa kubwaa sikua nimewai kuogelea ages 9

Mzee nikanasa kwenye tope nikanywa maji mengi nikaja vutwa kutoka nje kamuliwa maji..for sure zaidi ya week mbili Mimi sisikii vizuri

Mpaka Leo issues za kuogelea Mimi ni MPENZI MTAZAMAJI EVEN IN SWIMMING POOL #SIOGELEI SIOGII 🥺
Pole mkuu
 
Back
Top Bottom