Daktari wa Kichina afariki akimuokoa mama aliyekuwa anazama majini Kigamboni

View attachment 3374554

Tumempoteza daktari bingwa wa dawa za usingizi hospitali ya taifa Muhimbili. Dr.Zhang Junqiao amefariki juzi tarehe 15/06/2025 huko Kigamboni baada ya kuzama majini wakati akimuokoa mwananchi aliyekuwa anazama. Siku ya tukio Dr.Zhang alimuona mwananchi akizama na yeye kuamua kujitosa majini kumuokoa. Alipomfikia alimpatia jaketi lake la kuogelea na yeye kwa kuwa ni mzoefu akaogelea bila jaketi. Raia aliyekua akizama alifanikiwa kuokolewa, lakini maji yalimzidi nguvu Dr.Zhang akazama na kupoteza maisha.

Dr.Zhang alikuwa daktari Bingwa wa Dawa za Usingizi na Ganzi (Anesthesiologist), raia wa China aliyekuwa anafanya kazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Dr.Zhang alikua alikua na shahada ya udaktari wa binadamu (Bachelor of Medicine) Shahada ya upasuaji (Bachelor of Surgery), shahada ya umahiri katika matibabu ya ndani (Master of Internal Medicine) na shahada ya umahiri katika dawa za usingizi (Master of anesthesiology). Pia alikua na cheti cha ithibati ya kimataifa cha kuhudumu kama daktari bingwa wa dawa za usingizi katika nchi zaidi ya 100 duniani (NMLE).
.
Dr.Zhang atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuhudumia jamii ya watanzania, pamoja na umahiri wake kufundisha njia mpya za dawa za usingizi na ganzi. Atakumbukwa pia kwa ucheshi wake, uchangamfu wake na passion yake katika kazi. Dr.Zhang amekufa kishujaa akijaribu kuokoa maisha ya Mtanzania mwenzetu aliyekua akizama. Huu ni upendo wa ajabu. Dr.Zhang amefariki akiwa na umri wa miaka 38. Tumuombee pumziko la amani.!

Malisa
Kwa profile yake huyu alikuwa jasusi tu. Anyway Rest easy dr.
 
Hakika Inasikitisha sana. Najiuliza maji yalimzidije akazama?

Sijawahi kuogelea kwenye bahari lakini nimeogelea ziwani na mtoni. Tukiwa vijana wadogo ( umri wa miaka 12- 13) tulikuwa tunaogelea maji yenye kina kirefu, mara 3 ya kimo chetu bila life jacket na tumewahi kumwokoa kijana mkubwa kuliko sisi ambaye alikuwa hajui kuogelea.

Haya maji ya baharini ni tofauti na ya ziwani au mtoni? Au Dr hakuwa na uzoefu wa kutosha? Au kuna mkondo wa maji yanayotembea baharini ?

Sijui nini kilimkuta huyu Dr najaribu kuwaza tu kwa sauti? Alikuwa wa pekee kwa kweli amekufa akiokoa maisha ya mtu
Siku zote tatizo la baharini ni mkondo unaokuwa chini (current) ambao unakuvutia chini zaidi au kukupekeka bahari ya kina. Usione maji yametulia juu chini kuna movement kubwa sana tu ya maji katika baadhi ya sehemu. Kama hapo kivukoni ndio kabisa, kutokana na wembamba wa hiyo sehemu.

In fact, hapo kivukoni kina mkondo mkubwa tunaweza hata kutegesha mradi wa Hydro Electric Power, yaani tuaweka turbines za kuzalisha umeme
 
Mkondo wa chini unakuvuta kwenda wapi, mbali na eneo hilo au kwenda chini ?
 
Mara nyingi ni vyote viwili. Uzito wako unachangia kuvutwa chini.

Mikondo ya aina hii pia iko kwenye maziwa yaliyo lift valley. Kwa mfano kule Mbeya, Matema Beach, Ziwa Nyasa. LIle ziwa lina valley na cliff face ukisogea mbele, ambako kuna mkondo mkali. Watu wengi sana wanakufa wakiwa wakiogoelea na kusogea mbele ndani ya ziwa, kwa kuwa hata ukiwa fundi wa kuogelea huwezi kushindana na mkondo huo. Maziwa kama haya ya Lake Nyasa ni vema kuogelea kandokando ya ziwa, ni hatari sana kwenda ndani - yaani kuna cliff ambayo huioni kwa juu, na ukifika ukingoni mwa hiyo cliff utavutwa

Lake Nyasa liko hivi

1750259493058.png
 
Udogoni nilinusurika kufa maji nikaokolewa.

Nilikua na Fred tukaendesha baiskeli zetu akanipeleka kwenye bwawa kubwaa sikua nimewai kuogelea ages 9

Mzee nikanasa kwenye tope nikanywa maji mengi nikaja vutwa kutoka nje kamuliwa maji..for sure zaidi ya week mbili Mimi sisikii vizuri

Mpaka Leo issues za kuogelea Mimi ni MPENZI MTAZAMAJI EVEN IN SWIMMING POOL #SIOGELEI SIOGII 🥺
Bruh mm hata kuyasogelea maji zaidi ya kwenye ndoo hapana,

Baharini, huko swimming kazi yangu ni kukaa na kuwaangalia Ila mm hapana, ni hapana,

Apumzike kwa amani daktar
 
View attachment 3374554

Tumempoteza daktari bingwa wa dawa za usingizi hospitali ya taifa Muhimbili. Dr.Zhang Junqiao amefariki juzi tarehe 15/06/2025 huko Kigamboni baada ya kuzama majini wakati akimuokoa mwananchi aliyekuwa anazama. Siku ya tukio Dr.Zhang alimuona mwananchi akizama na yeye kuamua kujitosa majini kumuokoa. Alipomfikia alimpatia jaketi lake la kuogelea na yeye kwa kuwa ni mzoefu akaogelea bila jaketi. Raia aliyekua akizama alifanikiwa kuokolewa, lakini maji yalimzidi nguvu Dr.Zhang akazama na kupoteza maisha.

Dr.Zhang alikuwa daktari Bingwa wa Dawa za Usingizi na Ganzi (Anesthesiologist), raia wa China aliyekuwa anafanya kazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Dr.Zhang alikua alikua na shahada ya udaktari wa binadamu (Bachelor of Medicine) Shahada ya upasuaji (Bachelor of Surgery), shahada ya umahiri katika matibabu ya ndani (Master of Internal Medicine) na shahada ya umahiri katika dawa za usingizi (Master of anesthesiology). Pia alikua na cheti cha ithibati ya kimataifa cha kuhudumu kama daktari bingwa wa dawa za usingizi katika nchi zaidi ya 100 duniani (NMLE).

Dr.Zhang atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuhudumia jamii ya watanzania, pamoja na umahiri wake kufundisha njia mpya za dawa za usingizi na ganzi. Atakumbukwa pia kwa ucheshi wake, uchangamfu wake na passion yake katika kazi. Dr.Zhang amekufa kishujaa akijaribu kuokoa maisha ya Mtanzania mwenzetu aliyekua akizama. Huu ni upendo wa ajabu. Dr.Zhang amefariki akiwa na umri wa miaka 38. Tumuombee pumziko la amani.!

Malisa
Buriani
 
Aisee

Bachelar of Medicine
Bachelar of Surgery
Mmed internal medicine
Mmed anasthelogy

Halafu ana umri wa miaka 38

Kweli sisi bongo tunapoteza sana muda shuleni kwa elimu hizo zote angekua babu kama angesomea Bongo.

R.I.P specialist
Halafu CCM wanasema tunafuata Sera za china Sasa miaka 38 amesoma kila kitu Huku Tanzania 38 Ndio Kwanza bachelor
 
View attachment 3374554

Tumempoteza daktari bingwa wa dawa za usingizi hospitali ya taifa Muhimbili. Dr.Zhang Junqiao amefariki juzi tarehe 15/06/2025 huko Kigamboni baada ya kuzama majini wakati akimuokoa mwananchi aliyekuwa anazama. Siku ya tukio Dr.Zhang alimuona mwananchi akizama na yeye kuamua kujitosa majini kumuokoa. Alipomfikia alimpatia jaketi lake la kuogelea na yeye kwa kuwa ni mzoefu akaogelea bila jaketi. Raia aliyekua akizama alifanikiwa kuokolewa, lakini maji yalimzidi nguvu Dr.Zhang akazama na kupoteza maisha.

Dr.Zhang alikuwa daktari Bingwa wa Dawa za Usingizi na Ganzi (Anesthesiologist), raia wa China aliyekuwa anafanya kazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Dr.Zhang alikua alikua na shahada ya udaktari wa binadamu (Bachelor of Medicine) Shahada ya upasuaji (Bachelor of Surgery), shahada ya umahiri katika matibabu ya ndani (Master of Internal Medicine) na shahada ya umahiri katika dawa za usingizi (Master of anesthesiology). Pia alikua na cheti cha ithibati ya kimataifa cha kuhudumu kama daktari bingwa wa dawa za usingizi katika nchi zaidi ya 100 duniani (NMLE).

Dr.Zhang atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuhudumia jamii ya watanzania, pamoja na umahiri wake kufundisha njia mpya za dawa za usingizi na ganzi. Atakumbukwa pia kwa ucheshi wake, uchangamfu wake na passion yake katika kazi. Dr.Zhang amekufa kishujaa akijaribu kuokoa maisha ya Mtanzania mwenzetu aliyekua akizama. Huu ni upendo wa ajabu. Dr.Zhang amefariki akiwa na umri wa miaka 38. Tumuombee pumziko la amani.!

Malisa
Dah sasa alieokolewa CV yake ikoje ? Anyway nnachowaza ni dhambi Mungu anisamehe.
 
Tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa ehhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh Nchi yanguu

Yaani DR wa kawaida kabisa akitoka nje anafanya kazi Muhimbili ila mwenye level sawa na yeye hata Hospitali ya kati China hugusi but mlolongo wa viambatanishoooooooooooooo

MIMI NITAPIGA KELELE JUU YA AJIRA ZA WATANZANIA WAPO WENYE SIFA ILA HAWAAJIRIWI KWANINI
PUMBAVU
 
Back
Top Bottom