A
Anonymous
Guest
Kila siku asubuhi natumia usafiri wa daladala kutoka Igawilo kwenda katikati ya mji, jijini Mbeya. Kero kubwa tunayokumbana nayo ni baadhi ya daladala kutokufuata njia zilizoandikwa kwenye vibao vyao. Kwa mfano, gari lenye route ya Igawilo – Soko Kuu mara nyingi huishia Kabwe badala ya kufika Soko Kuu kama ilivyoainishwa.
Wakati mwingine abiria tunaelekezwa kushuka Kabwe na kupanda gari lingine kwa gharama zetu, na wakati mwingine madereva na makondakta hukataa kabisa kutupeleka hadi mwisho wa route waliyoitangaza. Hali hii hutusababishia usumbufu, kuchelewa kufika kazini au kwenye shughuli nyingine, pamoja na kuongeza gharama za usafiri.
Nimewahi kuwasilisha malalamiko haya kwa mamlaka husika zaidi ya mara tatu, lakini hadi sasa hakuna hatua zinazoonekana kuchukuliwa. Tatizo linaendelea kujirudia kila siku na limekuwa kero ya muda mrefu kwa wananchi wanaotegemea usafiri huu.
Ninaomba mamlaka zinazosimamia usafiri wa umma zifuatilie suala hili na kuhakikisha daladala zinafuata njia zilizosajiliwa na kuacha tabia ya kukatisha safari katikati ya njia bila sababu za msingi. Wananchi tunastahili kupata huduma ya usafiri inayozingatia taratibu na haki za abiria.
Pia soma ~ LATRA: Tumeanza kufunga ving'amuzi vya VTS kufuatilia Daladala zinazokatisha ruti na kuzidisha nauli