Daladala za Mbezi kupitia Manzese, Fire hadi Mnazi Mmoja zimeanza kazi rasmi

Wanaondesha usafiri katika jiji la Dar Ni vilaza kupitiliza. Wanarudisha mabasi bila kua na vituo.
Foleni zisizo za muhimu zinarudi Tena.
Hivi hapo jiji wanaona shida gani kuajiri watu wenye akili?
Wabunge wapo, wakuu wa wilaya wapo, mkuu wa mkoa yupo lkn wanashindwa kukaa na kuja na kitu chenye kuleta unafuu kwa maisha yetu.
Baada ya kukosa ubunifu wanawaandama dada utamu.
 
Hivi kulikuwa na ulazima wa kujenga vituo vya mwendokasi ambavyo vinakubali magari ya aina fulani tu?
 
Kundi dogo la watu wachache sana linaiangamiza nchi. Mimi sijui huwa wanachoweza ni kitu gani, probably flying to other countries na kufanya matamasha.

Huyu aliyeshika usikani was good kwa kukata utepe tu, haya mengine mnamuonea tu "they" can't do no shit!!
 
Watu walikuwa wana acha gari zao wanaingia kwenye mwendokasi kwenda makazini
Kusimama kwa usafiri huu gari ndogo zitaongezeka barabarani kuelekea mjini ukichanganya na hizo daladala foleni zitaanza kuwa kawaida tena
 
Bado kwa mtu mwenye akili atatumia mwendokasi. Maana hiyo daladala kwa muda itakayokaa foleni na kupiga debe, utatumia masaa hadi mawili. Ni bora usubiri tu mwendokasi.
 
Acha kufichaficha, sema mwana mama Muislam
 
Mkuu, kuna jamaa mmoja si wa bara hili jeusi ni wa huko mbali huko.

Huyo jamaa baada ya stori mbili tatu akaniambia "... nyie waafrika mpo hapa duniani na matatizo ni sehemu ya maisha yenu, haitakiwi kumaliza shida miongoni mwenu na serikali zenu hazipaswi kumaliza shida zenu".

Aliendelea... " Serikali ikimaliza shida zenu bado mtaisumbua na kulalamika..."

Kwenye hili la daladala tayari wanatengeneza tatizo ili baadaye waje walitatue kwa njia ya kujibinafsishia miradi hiyo.
 
Bomu lingine ni hii njia nane ya Kimara, Stop Over hadi Kibaha

Ile barabara ya kati ilisemwa ya mwendokasi ila cha ajabu haina vituo

Mpaka leo haina matumizi yoyote mwendokasi za Mbezi na Kibaha zinatumia vituo vilevile vya daladala

Kuishi Tanzania ni laana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…